Kauli za viongozi wakuu wa CHADEMA kuhusu 'Waraka wa siri' uliosambazwa kumhusu Zitto Kabwe

Kauli za viongozi wakuu wa CHADEMA kuhusu 'Waraka wa siri' uliosambazwa kumhusu Zitto Kabwe

Nataka nione kama " Kapuya"Ataomba Radhi.Hakuna Kiongozi wa CCM aliyewahi kuomba radhi.

Humjui Kapuya wewe... tena anaweza akasema "mnasema niombe radhi kwani nimewatia nyie!??" kumbukeni ishu ya ndege ya jeshi...
 
Dr.W.Slaa kiburi siyo maungwana muombe radhi Zitto ili swala liishie nje ya mahakama.

Kuna mahali huwa napata matatizo na akili za baadhi ya watu! Mmeshikilia Dr Slaa aombe radhi! Radhi ya nn hasa? Huu ni upuuzi kung'ang'ania radhi! We kaa na CCM yako mambo ya ndani ya CDM waachie wenyewe.
Hivi kulikuwa na ulazima gani kurugenzi ya usalama ya CDM kuuchapisha mnaouita waraka wa siri kwenye mitandao wakati vikao vya ndani vipo? Kuna sababu gani mpaka mtake huyu amwombe radhi yule huyu aseme yule? Nyuma ya hii ripoti kuna nini hasa. Ukinusa kwa mbali unakuta kuna kitu zaidi! Hofu, wasiwasi na kutokujiamini kwa baadhi ya watu kunapelekea haya kutokea sasa.
Mi niseme tu ya ngoswe mwachie ngoswe! CCM ijikite zaidi kutimiza ilani za chama chenu. Kuitikia vibwagizo vya CDM ni kuzidi kuua chama chenu.
 
Last edited by a moderator:
Na ndio nilisema hakuna mtu anataka kuambiwa habari mbaya, lakini ni vizuri kuambiwa habari mbaya ili uchukue hatua stahiki. Na muungwana atamshukuru mleta habari hata kama ni mbaya.

Mfano, kuna taarifa za misiba na hata sasa hivi ukiangalia uzi wa taarifa ya kifo cha Dr Mvungi kuna watu wamebonyeza 'like'. Ina maana hao watu wameipenda hiyo taarifa, wameshukuru kupewa taarifa za msiba ili wajiandae kwa maziko etc?
Mtu akileta taarifa ya msiba atapewa like kwakuwa atakuwa ametoa taarifa sahihi na halisi
Usichanganye madesa mkuu hizo ni hadithi mbili tofauti

Nisawa na mtu akikupa taarifa nyumba yako inaungua moto, huna budi mumshukuru
Lakini sio mtu anakuzushia vitu halafu unamshukuru
 
Viongozi Chadema wazipiga kavukavu kwenye mkutano wa Mbowe






Na Mussa Juma na Peter Saramba, Mwananchi


Posted Jumapili,Oktoba27 2013 saa 7:2 AM


Mwigamba amekuwa mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha tangu mwaka 2009, akiwa pia Mjumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Kaskazini, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Mkoa, Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chadema.



Kauli ya polisi


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameona hakuna kosa la kisheria lililotokea hasa kutokana na malalamiko yaliyofikishwa kwao dhidi ya Mwigamba ya kukichafua chama kwenye mitandao.


“Hili suala la mitandao ni kubwa na lina taratibu zake sasa kusema tu umechafuliwa na iwe kesi nadhani uchunguzi unahitajika kwao, sisi tumeona haya ni mambo yao wanaweza kuyamaliza wao ndiyo sababu tulimwachia, Mwigamba,” alisema Sabas.


Kosa analodaiwa kufanya Mwigamba


Akizungumzia sakata hilo jana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kwamba Mwigamba alibainika kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Jamii Forums uliokichafua chama hicho, akieleza haikuwa mara yake ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya hivyo na kwamba walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu.


“Kilichotokea ni hicho, vijana wa Red Brigade ndio waliomtoa ukumbini, baada ya kumbaini kukichafua chama, kwani laptop yake baada ya kuchunguzwa na wataalamu wetu walijiridhisha ni yeye ndiye aliyetuma ujumbe huo,” alisema Lema.


Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alitaja tuhuma zinazomkabili Mwigamba kuwa ni pamoja na kusema uongo, kupotosha taarifa za chama na kuchonganisha viongozi kupitia mtandao wa kijamii ya Jamii Forums.


Katika andiko lake kwenye mtandao, Mwigamba anadaiwa kuwatuhumu viongozi wa juu wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Wilbrod Slaa kuwa wamechakachua katiba ya chama hicho kuhusu ukomo wa nafasi za uongozi ili kujinufaisha binafsi.


Golugwa alisema kuwa baada ya kubanwa kwenye kikao, Mwigamba alikiri kuandika na kurusha taarifa hizo kwenye mitandao, lakini alipotakiwa kukabidhi kompyuta yake ili ichunguzwe na wataalamu wa mawasiliano wa chama hicho aligoma, hali iliyozua tafrani kati yake na walinzi wa chama hicho (Red Brigade), waliolazimika kutumia nguvu kumdhibiti.


Purukushani zilivyotokea


Habari zaidi zinaeleza kuwa katika harakati za kutaka kumnyang’anya Mwigamba kompyuta yake, mwenyekiti huyo wa Chadema mkoani Arusha alianza kushambuliwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, kabla ya kufanikiwa kumdhibiti.


Zinaeleza kuwa katika tukio hilo kulitokea pia kurushiana maneno na matusi ya nguoni kati yake na viongozi wengine wa chama hicho akiwamo Lema.
 
Hawa watu wamevaa sura za bundi. Wamejua ujumbe umefika ht wakiomba radhi haina shida. Ile taarifa si wamesema ipo tangu mwaka 2008 makao makuu ya chadema??
 
Dk slaa ni mnafiki unagonga like kwenye waraka halafu unaleta maelezo eti we r with u zitto shame on u hii conspiracy thery

Dr slaa.
Inasikitisha kwa kweli. Kama ile ripoti haikutoka Chadema,na Chadema haina tatizo na Zitto. Kwanini zito alienda Polisi kufungua kesi huku akidhani wahusika ni Chadema??
Na kama ripoti hakutoka Chadema, Kwanini msikae na zitto mumueleze aache siasa uchwara?

Nye vijana kila wakati mnakurupuka kama mnakimbizwa na siasa zenu mbofu. Nilifikiri hamna ubongo.
Kama mnafuata upepo sasa jitambue. Hii ni kwa wote wenye fikra fupi fupi.
 
Dr. Willbrod Slaa " hatuna tatizo hata kidogo na Zitto Kabwe. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wetu, kama kuna tatizo jambo ambalo ameleta tutamaliza kwa mujibu wa taratibu na tutaendelea na kazi na umoja wetu"

" waraka huo mchafu umeandikwa na viongozi wa CCM na kutoka idara nyeti ya serikali" chama kitapata taarifa zao na kuanika majina yao na nafasi zao

Edwin Mtei " haya mambo hayatubabaishi, tunajua ni uongo uliotungwa ili kutugombanisha" ..."kesho unaweza kusikia Zitto amehongwa hiki au kile. Keshokutwa ukasikia Slaa amehongwa hiki baadaye Mbowe amefanya hivi. Lengo kutuvuruga"

Mabere Marando " andishi hili ni feki. Nimeliangalia andishi lote. Nimejiridhisha kwamba limetengenezwa na watu wasiotakia mema chadema"

Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na akaweka kwenye blogu yake. Viongozi wengine waka 'like' kwenye jamii forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM?

Zitto facebook page

Zitto ni mnafiki haeleweki ni kama popo mnyama au ndege? bora ahame
 
Kama ni kweli Zitto ameandika kwenye facebook yake na akafanya hiyo conclusion KUANZIA LEO NA MIMI NINAUNGANA NA WATU WANAOMTILIA MASHAKA KATIKA HARAKATI ZA VYAMA VINGI...
 
wapi mnafiki na kiherehere Ben Saanane?? kwenye mabandiko kama haya anakuwa hana hela ya kuingiza Chanaga United
 
Last edited by a moderator:
Hebu tupe hiyo maana mpya ya
kubaka...Teh the the nyinyi wayu mnalaana za kila aina...Utakuwa na
virusi vikali sana vya mzee Kapuya..

Hahahaaa mimi nishawabaka sana 'Panzi'
 
jaman mnageuza sehem hii kutokua sehem ya great thnkers.mbona tunajadili kwa ushabiki wa vyama.tujadili hoja kwa hoja.kuna mambo meng tutayafaham zaid.lakn kwa kutukanana,kuzodoana jf inashuka saman.na tunaoishusha n sisi watumiaj!
 
Dr.W.Slaa kiburi siyo maungwana muombe radhi Zitto ili swala liishie nje ya mahakama.

Magufuli alimuomba radhi Pinda na wamiliki wa Malori baada ya kukosea kuhusu suala la malori ambalo liliisababisha serikali hasara? maana pinda alipindua maagizo ya magufuli na hii inaonekana magufuli alitenda kosa
 
I love/hate you ZITO?...NILIJUA WEWE NI MTETEZI WANGU KUMBE UNAPULIZA NA KUUMA,,NILIJUA IKO SIKU UTANITOA KIFUNGONI,,KUMBE WEWE NI MMOJA WA MAWAKILI WA UPANDE WA MASHITAKA YANGU,,,,NILIJUA UKO TAYARI KUANZA SAFARI ILI NAMI NIKUFUATE,,,KUMBE UMERUDI HATUA KADHAA NYUMA,,,,,NILIDHANI WEWE NI KIJANA MSOMI UNAEJUA MAANA YA UKOMBOZI....KUMBE UMEISHIA KUSOMA VITABU VYA KIZUNGU VILIVYOJAA CONCEPTUAL FRAMEWORK AMBAYO HAIJAFAFANULIWA...KEBEHI KWAKO BAADA YA KUMBE 4 ZA MDARASA LA 7b,,je ni kweli kwamba bora kuwapotezea simba 100 walioizunguka nyumba yako kutaka kukumaliza kuliko muacha nyoka 1 uvunguni mwa kitanda???......
......tafakari ya leo "wasomi acheni kuringia videgree vyeni...mbona hata themometer ana degree kibaaao lakini haringi na anafanya kazi kwapani???"
 
Dr. Willbrod Slaa " hatuna tatizo hata kidogo na Zitto Kabwe. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wetu, kama kuna tatizo jambo ambalo ameleta tutamaliza kwa mujibu wa taratibu na tutaendelea na kazi na umoja wetu"

" waraka huo mchafu umeandikwa na viongozi wa CCM na kutoka idara nyeti ya serikali" chama kitapata taarifa zao na kuanika majina yao na nafasi zao

Edwin Mtei " haya mambo hayatubabaishi, tunajua ni uongo uliotungwa ili kutugombanisha" ..."kesho unaweza kusikia Zitto amehongwa hiki au kile. Keshokutwa ukasikia Slaa amehongwa hiki baadaye Mbowe amefanya hivi. Lengo kutuvuruga"

Mabere Marando " andishi hili ni feki. Nimeliangalia andishi lote. Nimejiridhisha kwamba limetengenezwa na watu wasiotakia mema chadema"

Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na akaweka kwenye blogu yake. Viongozi wengine waka 'like' kwenye jamii forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM?

Zitto facebook page

Dr. Slaa vs Zitto Kabwe, bora aondoke huyu zitto kabwe a.k.a kibaraka wa Lowasa kwanza madhara yake ni madogo pili hana mawazo ya mabadiliko zaidi ya kukibomoa chama, tatu hamfikii dr.slaa ktk siasa, nne ni corrupt na tano jimbo lake linamshinda ndio ataweza kuiongoza chadema iliyojaa watu wenye akili na wasomi. Mnafiki mkubwa Zitto Kabwe.
 
Back
Top Bottom