Kauli za viongozi wakuu wa CHADEMA kuhusu 'Waraka wa siri' uliosambazwa kumhusu Zitto Kabwe

Kauli za viongozi wakuu wa CHADEMA kuhusu 'Waraka wa siri' uliosambazwa kumhusu Zitto Kabwe

Mnachukia mkiona amani inarudi CDM? Na wiki ijayo tunayamaliza yote haya na kuibuka timu imara zaidi. Wenye majungu na uzushi watafute lingine, hili linaenda kwisha.
Asante kiongozi...
Hii ndio Chadema bhana..
 
Mnachukia mkiona amani inarudi CDM? Na wiki ijayo tunayamaliza yote haya na kuibuka timu imara zaidi. Wenye majungu na uzushi watafute lingine, hili linaenda kwisha.

Asante Dr,

Hakika hii taarifa yako imenipa amani sana moyoni,nawaombea mambo yaende sawa huko kwenye kikao

Ila jadilini suala la Mh Lema pia.
 
Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na akaweka kwenye blogu yake anayoenda kwa jina la Kilewo 2015 na Viongozi wengine waka ‘like' kwenye jamii forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM?

Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki, atawaumbua tu.
Hawawezi kuficha yaliyomo ndani ya vifua vyao, vitadhihiri tu.
Wanajaribu kuudanganya umma wa watz lakini wanaumbuka tu.
 
Sasa mi napata shida sana Lema na Yericko pia waajiriwa wa TISS Kama msemavyo?

Hivi Lema na Yericko kwa kauli hizi na ushabiki wao watapata adhabu gani? Maana kila Mwana CDM alisupport huu Uzi bila hata ya ushahidi!

Leo mnakula matapishi yenu wenyewe! Duu akili ni nywele kila mtu Ana zake

Mkuu naona uko makini sana kuyasema ya Chadema! Ila nadhani ubongo wako wa nyuma hautunzi kumbukumbu vizuri. Katika tofauti zilizotokea kati ya ZZK vs LEMA hakuna aliehusika na ule waraka wa kichina toka ccm. sasa ukisema kuwa Chadema inakula matapishi yake, hapo ndipo unadhiirisha kuwa akili za magamba zikoje.
YANGOSWE MWACHIE ..........................
 
ni kweli individuals hawawezi kuwa maadui wa cdm , bali adui mkubwa wa cdm ni mfumo mbovu wa ccm .
 
Dr slaa.
Inasikitisha kwa kweli. Kama ile ripoti haikutoka Chadema,na Chadema haina tatizo na Zitto. Kwanini zito alienda Polisi kufungua kesi huku akidhani wahusika ni Chadema??
Na kama ripoti hakutoka Chadema, Kwanini msikae na zitto mumueleze aache siasa uchwara?

Cha kushangaza zaidi Henry Kilewo kiongozi wa chadema aliibandika kwenye blog yake.

Je Henry Kilewo ni kiongozi wa ccm?
 
Last edited by a moderator:
'like' ni mbadala wa neno 'noted' au ishara ya kujulisha kuwa umesoma, umeona, umejiunga wala si lazima upende kilichoandikwa, hizi ni lugha za mitandao wala zisikuchanganye.
Mkuu umefafanua vizuri sana ila ni ajabu kuwa kuna watu na uelewa wao wanashindwa kulikubali hili. Dr ku like ilikuwa kuwafahamisha wengine kuwa ameisoma post hiyo na ndio maana hata akija hapa na kuikana ni kwa vile kaisoma.
 
Katibu mkuu wa chadema dk slaa amesema kuwa chadema hawana tatizo na zitto na wanamtambua kama naibu katibu mkuu wao,na suala la waraka ni njama za wabaya wao ccm na serikali kupitia idara nyeti yani tiss kasema wapo vigogo wenye majina mengi wamehusika watawataja hivi karibuni

Hivi kumbe Lema na Yeriko wako TISS. Asante kwa taarifa.
 
Asante kwa taarifa Dr. Slaa

Ila hii haihusiani na mambo ya unafiki wa posho.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Zitto CDM wamefanya yao na ujumbe umefika jipime mwenyewe ujisahihishe na uache unafiki wako wa kujifanya kila kitu unajua 'like' ya Dr ina maana kubwa sana, ila sasa nafikiri umejua kuwa huna nguvu sana ndani ya chadema kama ulivyokuwa unafikiri kwani umeisha kutetewa na magamba baadala ya makamanda wenzako pima na tena ikiwezekana jiulize nafasi yako naibu katibu wa CDM ili ikaliwe na mwingine ajenge chama.
Zitto na Dr Slaa mliopasha chadema hadi kufikia hapo ilipo lakini ujitenge nayo kwa sasa tuambie kama kuna kitu huridhiki nacho ndani ya chama ili viongozi wajipange na kurekebisha maana hakuna aliye mkamilifu. wasiwasi unawaingia wapenda mabadiliko pale ambapo askari mpigaji na hodari unapopendwa na maadui zako ???? jirekebishe jenga chama nchi inaliwa hii au unataka tuachíe CCM tena ili Kapuya awe Waziri Mkuu.
 
Katibu mkuu wa chadema dk slaa amesema kuwa chadema hawana tatizo na zitto na wanamtambua kama naibu katibu mkuu wao,na suala la waraka ni njama za wabaya wao ccm na serikali kupitia idara nyeti yani tiss kasema wapo vigogo wenye majina mengi wamehusika watawataja hivi karibuni
Huyu kikongwe wenu atawahadaa mpaka basi. CDM walidai wana mkanda wa walipua mabomu,leo tena kasema anawafaham atawataja! Punguzeni kutumia mirungi japo muwe na bongo zenye maono robo.
 
Back
Top Bottom