Ikiwa wewe umezaliwa Tanganyika basi ukifika hapa kisiwani jiandae na kero zifuatazo.
1. Kudaiwa leseni ya udereva Zanzibar (hata kama unayo ya huko kwenu).
2. Kukosa Uhuru wa kutumia kilevi hadharani,
3. Kukosa fursa ya kumiliki ARDHI.
4. Bullying (kuitwa CHOGO).
5. Uhuru wa kuabudu mashakani (ref. Uchomaji Moto nyumba za ibada)
Kuhusu leseni,sio kweli sana,kama upo kwa muda mfupi,ya bara inatumika vzr tu,nimekaa huko kwa miezi SITA.
Kuhusu. Kutumia kilevi,yapo maeneo,bar,mfano Ccm maisara pale gambe linapigwa sana.
Au fuoni lodge,mziki,pombe sana tu,
Yapo mpaka maeneo Kuna mbuzi katoriki.
Makanisa yapo sana,hata pale stone town,Kuna kanisa kubwa tu,kuhusu uhuru wa kuabudu au kubaguliwa,hayo ni matukio machache,hata bara po,miaka ya 90,waislam walivamia na kuvunja mabucha ya kitimoto ubungo.
Kuhusu kumiliki ardhi,wabara kibao wanaardhi,wamejenga lodges,majumba,nk.Zenj ni ndogo,inaingia Kagera hata mala kumi!!Dar ina watu wengi kuliko Zenj!!
Kuna mazuri mengi tu ya Zenj,kwanza ni watu waaminifu sana.
Wewe hujafika Zenj,