Kesho Mwanza CHADEMA itaifunika CCM sherehe za uhuru. Wakuu wa chama kuhudhuria

Hivi anaenda kwenye sherehe ya kitaifa au ya CCM?Hiyo bei aliyofika ni bei gani?
..kwani wenyeviti wa mitaa/ vijiji wangeongoza taifa la Tanzania au wangeongoza taifa la ccm? Siasa ni ajira wagombea wengi walitegemea kuishi kwa kutegemee uenyekiti leo hii hawana pakuanzia kwa kutii sauti ya mbowe alafu uyo uyo mbowe anaenda kujikomba kwa watawala wakati uku mtaani katengeneza tahaluki kwa wanachama
 
...anae ongoza kikao cha kamati kuu ni nani na alieteuliwa kuongoza ujumbe kwenda mwanza ni Nani? Ebu tumia iyo akili yako kubwa kutambua kosa la kamati kuu
Madhara yatokanayo na hilo kosa ni yapi?
Ikiwa watashiri sherehe za Uhuru then maisha yataendelea
 
Ccm mnaumia chadema kwenda kwenye sherehe za uhuru
...kwa mawazo ya namna hii ndo maana tunaitwa nyumbu...kwaiyo miaka 4 izo sherehe hazikuwepo? au chadema walikua wamesahu kama huwa Kuna sherehe za uhuru kwa miaka 4 😃
 
Ila kuna jambo, CHADEMA watoe ufafanuzi wa kilichowafanya kuhudhuria sherehe za Uhuru . Au kwavile ndiyo siku ya kuzaliwa Mwenyekiti wetu? Vyovyote vile uamuzi huu una sababu, zianishwe na chama Kwa wananchi.
 
Nimesikitishwa Jana kuona kamati kuu ya chadema ikitamka kwa kinywa kipana kwamba kesho 9/12/2019 mwenyekiti mbowe ataongoza ujumbe wa viongozi kusherehekea uhuru wa tanganyika ccm kirumba mwanza mbele ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania! Hivi kweli mbowe umesahau mwezi uliopita ulitangaza kususia uchaguzi wa serikali ya mitaa/vijiji ukisema serikali ya ccm imewaengua wagombea na kuwanyima haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa je leo nini kimebadilika? Mikutano ya kisiasa imefungiwa kwa miaka 4 kinyume cha katiba ya nchi bado huoni unasema unaenda kwenye uhuru!! Tukisema wamekufika bei kama ulivyokua unawatuhumu kina mrema utabisha?..ivi unakwama wapi ndg au kesi zimekufanya uchanganyikiwe sasa unatafuta huruma ya watawala kuomba poo! Bila kujali ni wanachama wangapi wameumia kwaajiri ya kutetea misimamo ya chama ulioitoa..usipobadilika utaongoza chama kikiwa dhaifu sana maana unataka kuwa mwenyekiti mwenye ndimi 3 nilizani umejifunza makosa ya 2015 ya kusomba mafuriko hewa.
Kwa hili wenye akili kubwa tutazidi kuipongeza CHADEMA, hata wewe CCM kima cha chini imekugusa.
 
..kwani wenyeviti wa mitaa/ vijiji wangeongoza taifa la Tanzania au wangeongoza taifa la ccm? Siasa ni ajira wagombea wengi walitegemea kuishi kwa kutegemee uenyekiti leo hii hawana pakuanzia kwa kutii sauti ya mbowe alafu uyo uyo mbowe anaenda kujikomba kwa watawala wakati uku mtaani katengeneza tahaluki kwa wanachama
Kama mlikua mnajua kuwa hao wenyeviti wanategemea hiyo kazi ili waishi kwanini mliwaengua wasigombee? Ungemshauri mwenyekiti wako atoe nafasi huru Kwa wote ili atakayeshinda apewe kazi. Mliwafukuza wote wa uoinzani halafu sasa mna laumu Chadema kukataa kushiriki uovu wenu.
Tumia akili kabla ya kuandika upumbavu hapa.
 
...kwa mawazo ya namna hii ndo maana tunaitwa nyumbu...kwaiyo miaka 4 izo sherehe hazikuwepo? au chedema walikua wamesahu kama huwa Kuna sherehe za uhuru kwa miaka 4 😃

Naunga mkono hoja post yako namba moja kwa 100%. Sioni ni kipi kimewafanya cdm washiriki hizo sherehe. Nilisema ni bora wangeomba kibali polisi kisha waongee na wananchi katika kusherehekea uhuru, na sio kujichanganya kwenye hafla ya serikali. Nimedharau sana uamuzi huu wa cdm. Mbona sisi tunaowakubali tumeridhika kabisa na wao kutoshiriki kwenye hayo mambo, wakati kukiwa na uhuni wa wazi kwenye demokrasia?
 
Nimesikitishwa Jana kuona kamati kuu ya chadema ikitamka kwa kinywa kipana kwamba kesho 9/12/2019 mwenyekiti mbowe ataongoza ujumbe wa viongozi kusherehekea uhuru wa tanganyika ccm kirumba mwanza mbele ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania! Hivi kweli mbowe umesahau mwezi uliopita ulitangaza kususia uchaguzi wa serikali ya mitaa/vijiji ukisema serikali ya ccm imewaengua wagombea na kuwanyima haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa je leo nini kimebadilika? Mikutano ya kisiasa imefungiwa kwa miaka 4 kinyume cha katiba ya nchi bado huoni unasema unaenda kwenye uhuru!! Tukisema wamekufika bei kama ulivyokua unawatuhumu kina mrema utabisha?..ivi unakwama wapi ndg au kesi zimekufanya uchanganyikiwe sasa unatafuta huruma ya watawala kuomba poo! Bila kujali ni wanachama wangapi wameumia kwaajiri ya kutetea misimamo ya chama ulioitoa..usipobadilika utaongoza chama kikiwa dhaifu sana maana unataka kuwa mwenyekiti mwenye ndimi 3 nilizani umejifunza makosa ya 2015 ya kusomba mafuriko hewa.
Kesho ni sikuku ya uhuru wa Tanzania au ccm ? kwa ni Tanzania Mbowe na wanachadema ni wananchi wa nchi gani? au kukataa ujinga wa ccm kwa akili yako ndo kuikataa Tanzania, nchi hii ina wajinga wengi sana
 
Nimesikitishwa Jana kuona kamati kuu ya chadema ikitamka kwa kinywa kipana kwamba kesho 9/12/2019 mwenyekiti mbowe ataongoza ujumbe wa viongozi kusherehekea uhuru wa tanganyika ccm kirumba mwanza mbele ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania! Hivi kweli mbowe umesahau mwezi uliopita ulitangaza kususia uchaguzi wa serikali ya mitaa/vijiji ukisema serikali ya ccm imewaengua wagombea na kuwanyima haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa je leo nini kimebadilika? Mikutano ya kisiasa imefungiwa kwa miaka 4 kinyume cha katiba ya nchi bado huoni unasema unaenda kwenye uhuru!! Tukisema wamekufika bei kama ulivyokua unawatuhumu kina mrema utabisha?..ivi unakwama wapi ndg au kesi zimekufanya uchanganyikiwe sasa unatafuta huruma ya watawala kuomba poo! Bila kujali ni wanachama wangapi wameumia kwaajiri ya kutetea misimamo ya chama ulioitoa..usipobadilika utaongoza chama kikiwa dhaifu sana maana unataka kuwa mwenyekiti mwenye ndimi 3 nilizani umejifunza makosa ya 2015 ya kusomba mafuriko hewa.
Unaelewa uliloandika au na Wewe mwenyewe utatafuta mtu akutafsirie maana ya andiko hili?
Malaria kichwani dawa yake inaitwa mseto!
 
Naunga mkono hoja post yako namba moja kwa 100%. Sioni ni kipi kimewafanya cdm washiriki hizo sherehe. Nilisema ni bora wangeomba kibali polisi kisha waongee na wananchi katika kusherehekea uhuru, na sio kujichanganya kwenye hafla ya serikali. Nimedharau sana uamuzi huu wa cdm. Mbona sisi tunaowakubali tumeridhika kabisa na wao kutoshiriki kwenye hayo mambo, wakati kukiwa na uhuni wa wazi kwenye demokrasia?
Mkuu kuna kitu hujakiona kitatokea au ndio kitaachwa jumla.
Jiwe kazoea kutoa maneno ya kashfa na matusi kwenye sherehe za kitaifa baada ya kuzibinafsisha kuwa za chama chake.
Sasa kamati kuu ya Chadema imesema itahudhuria maana yake na wapenzi na wanachama nao watahudhuria.
Sasa yeye alete za kuleta eti kumkashifu Mwenyekiti wa Chadema au Chadema yenyewe aone kilichomtoa kanga manyoya au mile cha mtema kuni!
Anaweza jikuta anazomewa na zaidi ya nusu uwanja mbele ya mabalozi na wageni wengine na tabia hiyo ikawa ndio mwisho.
Naamini watu wake watamshtua kuchunga mdomo LA sivyo asimlaumu mtu
 
..kwani wenyeviti wa mitaa/ vijiji wangeongoza taifa la Tanzania au wangeongoza taifa la ccm? Siasa ni ajira wagombea wengi walitegemea kuishi kwa kutegemee uenyekiti leo hii hawana pakuanzia kwa kutii sauti ya mbowe alafu uyo uyo mbowe anaenda kujikomba kwa watawala wakati uku mtaani katengeneza tahaluki kwa wanachama
Tatizo ni dogo,wewe sio mwanasiasa waache wanasiasa wafanye siasa. Hizi ni mbinu za kisiasa kama hawana mikutano ya hadhara,hata ya ndani tu imedhibitiwa hata ya wachaguliwa ni shida unafikiri ili kila mtz ajue cdm bado IPO ni mbinu gani zitumike?!?. Acha aende atambulishwe mbele ya halaiki hiyo hapo ndio utapata jawabu. Kwa sasa usilalamike ndg yangu
 
Kama mlikua mnajua kuwa hao wenyeviti wanategemea hiyo kazi ili waishi kwanini mliwaengua wasigombee? Ungemshauri mwenyekiti wako atoe nafasi huru Kwa wote ili atakayeshinda apewe kazi. Mliwafukuza wote wa uoinzani halafu sasa mna laumu Chadema kukataa kushiriki uovu wenu.
Tumia akili kabla ya kuandika upumbavu hapa.
... hahahaha kamanda punguza hasira utaharibu hoja yako nzuri...siasa ni sayansi Dr slaa alitufundisha
 
Back
Top Bottom