Kesho Mwanza CHADEMA itaifunika CCM sherehe za uhuru. Wakuu wa chama kuhudhuria

Kesho Mwanza CHADEMA itaifunika CCM sherehe za uhuru. Wakuu wa chama kuhudhuria

CHADEMA ndani ya hizi wiki mbili wamefanya makosa mengi sana ya kimkakati nafikiri kuna shida sehemu, japo wafuasi wao hawalioni nimeona hata humu kuna watu nilikuwa nawaona kama fikra huru kumbe wanafuata tu kinachosemwa na viongozi ila wacha tuone muda utaongea japo nimehudhunishwa sana na yaliyotokea. Kushiriki uhuru nikama kumpa endorsement kiongozi ulimpinga kwa miaka yote ya uongozi wake ajabu mwaka wake wa mwisho unamuunga mkono wacha tuone
Sikukuu za nchi zinahusikaje na mtu ambaye ni mpita njia tu ataondoka na nchi inabaki na maisha yataendelea.

No one is indispensable anywhere and no one is bigger than this country. State public holidays belong to the people and not an individual manifesting as a demigod.
 
..u can call me whatever you want.

..lakini hiki anachofanya Magufuli, kuzungumza lugha ya kabila lake ktk ziara ya kiserikali ni UKABILA.

Ukabila mnauona kwa wenzenu lakini kwenu hamuuoni. JPM sio mkabila Period! Wewe ni mkabila namba moja na chama chako.
 
Naunga mkono hoja, sielewi hata ni kipi kimewafanya waende kwenye hiyo sherehe, nilisema bora wangeomba kibali polisi cha wao kusherehekea na kuongea na wananchi, bila kushiriki kwenye hiyo ya kiserikali. Hata wakinyimwa kibali poa tu kwani hata wakienda kwenye hiyo hafla ya rais ndio wataongea na hao wananchi? Hakuna kitu kibaya kama upinge jambo kwa sababu fulani, kisha ushiriki tena jambo lile huku suluhu haijapatikana. Hapa viongozi wa cdm hatuwaelewi, wanataka kurudia kosa lile lile la kumpokea Lowassa na kumpa nafasi adhimu.
WAMEUNGA MKONO JUHUDI. KWANI TANGU WAMESUSA KUNA KITU KILIBADILIKA. KUMBUKA TANGU WALIPOMSUSA NAIBU SPIKA KUINGIA BUNGENI NA KUZIBA MIDOMO!
 
Tatizo ni dogo,wewe sio mwanasiasa waache wanasiasa wafanye siasa. Hizi ni mbinu za kisiasa kama hawana mikutano ya hadhara,hata ya ndani tu imedhibitiwa hata ya wachaguliwa ni shida unafikiri ili kila mtz ajue cdm bado IPO ni mbinu gani zitumike?!?. Acha aende atambulishwe mbele ya halaiki hiyo hapo ndio utapata jawabu. Kwa sasa usilalamike ndg yangu
....nashukuru umetoa ufafanuzi mzuri nimeanza kuelewa ndg yangu tatizo langu nilihitaji ufafanuzi kwa manufaa ya watu wengi uku mtaani kwasasa hatuivi chungu kimoja na watu wa ccm kwaiyo wakiona mwenyekiti wetu na ujumbe wake wanamsujudia mwenyekiti wao tutaonekana wote ni nyumbu wakati kosa ni la mbowe
 
Vyama goigoi halafu mviibie tena kura mbona hii haiingii akilini.
You people must be disproportionately foolish.
 
Sherehe za uhuru ni za Kitaifa aliyeleta uhuru ni Mwl Nyerere alituachia sherehe hizi na vyama vingi alisema pawepo mfumo wa vyama vya upinzani hili chama tawala kisije kubweteka.Mbowe akiwepo katika sherehe hizo nategemea akijitokeza will be applaused kwa umahili wake wa kutetea demokrasia isibakwe na wanaotetea ubinafsi.wa chama kimoja kinyume na RAI YA MWL NYERERE.
 
Acha ufala wewe. Ulisoma Ujerumani kwa akili ipi? Halafu soma aya ya pili kutoka mwisho wa huu utumbo wako. Mbona huyu ba..sha wako anahubiri ubaguzi wa wazi na kuwanyanyasa wengine kisiasa. Hii ndiyo amani unayoijua? Wewe kwako kuwa na amani ni kutokuwepo na vita? Sijui hata Ujerumani ulifikaje. Ipo siku tu wewe mtetea utataga.
Falah ni wewe mwenyewe usio weza kutenganisha siasa na "reality of life". Msingi mkubwa wa maisha ni uhai na maelewano ya kuishi pamoja katika jamii kwa kuzingatia utiifu wa sheria ambazo tumejiwekea sisi wenyewe. Hatuwezi Bungeni tukatunga sheria halafu mitaani tukazibomoa.

Nyie kwa upande mwingine ni watu ambao mnataka sisi tuishi maisha kwa "principles of the jungle", kwa hali hiyo hatuwezi uwiana. Lazima tutazipiga tu na hivyo kusababisha chaos ya maisha.

Nyie mna mawazo na fikra ambazo ni destructive kwenye society yetu. Ni fikra ambazo zimepitwa na wakati. Mmevamia mambo ambayo kwa undani wake hamyajui. Nyie mnataka kuleta mfumo wa siasa ambao hata nchi anzilishi za mfumo huo hazifuati tena mfumo huo. Sijawahi ona nchi baada ya uchaguzi kwisha kila siku wanasiasa wanaandamana kupiga siasa mitaani. Hiyo itakuwa nchi tena au ndiyo Banana Republic?

Hatuwezi kila siku tukapiga siasa na kuandamana kila siku. Kama wana siasa baadhi ya wanachama wa chama chenu ni wabunge ambao ni representatives wa chama chenu na wananchi walio wachagua Bungeni. Si wanawajibu wa kupigania hizo haki zenu Bungeni? Kuna sababu gani tena za kutala kila siku kuandamana mitaani kwa kitu ambacho mna watu wenu wa kuwafikishia malalamiko yenu?

Tukiruhusu kila siku watu wapige blaablaa mitaani tutakuwa na mda kweli wa kuweza fanya mambo ya maendeleo? Hasa tukizingatia mwenenodo wenu wa kugoma na kususia kila kitu, hiyo hali sio hali ya kistaarabu tena, ni hali ambayo ina mfumo tatanishi wa maisha. Tukiruhusu hayo mambo, yaendelee hatuta piga hatua ya maendeleo.

Lazima tuwe watiifu wa sheria zetu na heshima kwa viongozi wetu ambao wananchi wamewachagua kwa misingi ya kidemokrasia na kukubalika. Hatuwezi ishi maisha ya kiholela holela kama nyie vibaraka wa mabeberu mnavyo taka. Hayo maisha nendeni nayo kwa hao mabeberu wenu. Sisi hatuyataki.

Maisha ya maelewano yana principles zake. Bila amani jamii haiwezi piga hatua ya maendeleo. Off course vita nita ni adui wa maendeleo ya kijamii. Kaka mzima wewe?

Rais Magufuli ni mpigania Uhuru wa kweli wa maisha katika Bara la Afrika na hakuna mwingine. Mifumo yote ya maisha duniani ina kikomo chake ambacho kina sababishwa na physical Processes ambazo nazo zina tokana chemical and biological processes kwenye miili ya binadamu. Hiyo ni principle of humanity. Binadamu sio monotone bali ana elements za dynamism. Ukae ukijua "trottel".
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Ndiyo kwa sababu nyie hamna nia ya kuwa wapinzani wa kweli wa kisiasa. Nyie ni mchanganyiko wa malooser wa kutaka maisha ya mtelemko, watu wenye kisirani na Rais wetu na serikali yake na wazandiki wasio itakia mema nchi yetu.

Nyie sio wapinzani wa kweli. Nyie ni watu ambao ni waroho wakubwa wa madaraka ambao mko tayari kutumia njia zozote zile kinyama ili mradi mfikie malengo yenu. Na ndiyo maana kazi yenu kubwa ni kubuni uongo usio semekana zidi ya Rais wetu na serikali yake.

Kwa hali hiyo hampaswi kuwa katika jehazi moja na wazalendo wa kutaka amani a maendeleo ya nchi yao.
Vipi kiupande wako/wenu hamna hii ajenda ya kulazimisha kubakia madarakani?
 
Naunga mkono hoja post yako namba moja kwa 100%. Sioni ni kipi kimewafanya cdm washiriki hizo sherehe. Nilisema ni bora wangeomba kibali polisi kisha waongee na wananchi katika kusherehekea uhuru, na sio kujichanganya kwenye hafla ya serikali. Nimedharau sana uamuzi huu wa cdm. Mbona sisi tunaowakubali tumeridhika kabisa na wao kutoshiriki kwenye hayo mambo, wakati kukiwa na uhuni wa wazi kwenye demokrasia?
... nashukuru kwa kuliona hilo ndg yangu tatizo sisi wanachama ndo tunafanya viongozi wetu wa vyama kufanya maamuzi ya hovyo bila kuhofia tutawafanya nini kwasababu tunaogopa kuhoji eti tusiitwe wasaliti. Serikali ya ccm imewaengua wagombea wetu na kufanya uchaguzi wao kibabe eti leo mwenyekiti wetu unaenda kujumuika nao na kuchekeana ili iweje sasa! Lisu kafutwa ubunge kibabe akiwa katika maumivu makali ya wasiojulikana leo mwenyekiti unaenda kuchekeana vijana wengi wameumia wengine kufungwa kwa uonevu leo mwenyekiti wetu unaenda kufurahia eti uhuru..bora ungehamasisha siku iyo tukajitolee damu kwa wagonjwa hospitalin ingekua bora sana
 
Kamati kuu ya Chadema kwa kauli moja imeazimia kushiriki katika sherehe za Uhuru zitakazofanyika Mwanza kitaifa.

View attachment 1284723
Mimi naiona hii kama fursa adimu ya mheshimiwa rais wa Tanzania Dr. JSPM kumuita mbowe nakumpa dakika 5 ya kusalimia hadhara itakoyojitokeza kesho.

Inatakiwa nafasi hii itumike kama initiative ya kujenga madaraja ya upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa wa Tanzania.

Vilevile fursa hii itumike kama jukwa la kufunika makaburi yote yaliyofukuliwa na kuruhusu mikutano ya hadhara. Decemba 9, ni siku ya kurudishishia wa Watatanzania Uhuru wao kusema na kutoa mawazo mbadala kwa serikali yao.
 
Ndiyo kwa sababu nyie hamna nia ya kuwa wapinzani wa kweli wa kisiasa. Nyie ni mchanganyiko wa malooser wa kutaka maisha ya mtelemko, watu wenye kisirani na Rais wetu na serikali yake na wazandiki wasio itakia mema nchi yetu.

Nyie sio wapinzani wa kweli. Nyie ni watu ambao ni waroho wakubwa wa madaraka ambao mko tayari kutumia njia zozote zile kinyama ili mradi mfikie malengo yenu. Na ndiyo maana kazi yenu kubwa ni kubuni uongo usio semekana zidi ya Rais wetu na serikali yake.

Kwa hali hiyo hampaswi kuwa katika jehazi moja na wazalendo wa kutaka amani a maendeleo ya nchi yao.
Sio wapinzani wa kweli tukisema mmlipe mkulima pesa yake? Au tukisema ndege yetu ilikamatwa canada?au tukisema raisi anavunja katiba kwa kuzuia mikutano ya kisiasa hasa kwa wapinzani? Au tukiuliza walipo ndugu jamaa marafiki na wachama wetu wakina azor ben na wengine wako wapi? Au tukiuliza ni wakina nani wanateka watu, waliopiga risasi lisu ni wakina nani? Au tukisema watumishi wapewe haki zao vip kuhusu ajira kwa vijana wetu? Utaka upinzani wanaofanyiwa hayo halafu wao wasifu na abudu ndugu hebu fikiri kwa makini kama mtu huru
 
Mkuu kuna kitu hujakiona kitatokea au ndio kitaachwa jumla.
Jiwe kazoea kutoa maneno ya kashfa na matusi kwenye sherehe za kitaifa baada ya kuzibinafsisha kuwa za chama chake.
Sasa kamati kuu ya Chadema imesema itahudhuria maana yake na wapenzi na wanachama nao watahudhuria.
Sasa yeye alete za kuleta eti kumkashifu Mwenyekiti wa Chadema au Chadema yenyewe aone kilichomtoa kanga manyoya au mile cha mtema kuni!
Anaweza jikuta anazomewa na zaidi ya nusu uwanja mbele ya mabalozi na wageni wengine na tabia hiyo ikawa ndio mwisho.
Naamini watu wake watamshtua kuchunga mdomo LA sivyo asimlaumu mtu

Duuu mkuu, kwa hiyo kwenye huo mkutano ndio Magufuli ataelewa cdm ni kina nani? Na asipowakejeli itakuwaje? Kuliko kushiriki hiyo hafla ni bora wangeshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kungekuwa na impact, na sio hiyo hafla ya nusu saa. Kweli kabisa kamati kuu wamekaa wakaona hiyo hafla ndio sehemu ya kutoa fundisho! Nisikufiche kuna tatizo huko kwenye uongozi wa cdm kama maamuzi ni haya. Na ndio maana msimamo wangu uko wazi, nafasi ya mwenyekiti haimtoshi tena Mbowe kwa sasa.

Kushiriki hiyo sherehe ni kwenda kufuta madai yote halali ya cdm kuwa kuna uonevu wa kidemokrasia hapa nchini. Kama wananisikia nawashauri kusitisha mara moja kushiriki hiyo sherehe maana ni kujimaliza wenyewe.
 
Rais atatumia ushiriki wa Mbowe kwenye sherehe za Uhuru kwa kumpiga madongo...wapinzani mbona hawajazira kuja kwenye sherehe za uhuru maendeleo hayana chama ndo maana Mbowe yuko hapa....
 
Mfuatilie vizuri huyu member, huwa anajisifia kasoma Ujerumani na mke wake eti ni mjerumani, anasema hata hilo jina la kwenye id Ni la mkewe! Ana pointless za hatari na hujiona bonge la msomi mzalendo. Sasa pata picha anaandika post ndefu yenye kejeli na kujipendekeza juu, huku akiwa na tatizo kubwa la kuandika kwa ufasaha, kuna post moja nilimpa vitu vyenye ncha kali mpaka akatia akili. Ni mtu aliyechanganyikiwa
Duuh! Wewe jamaa ni cockroach kweli kweli. Hoja gani hii unaileta hapa? Unakusanya majeshi ili kuwa against me? Huniwezi wewe mdudu wa kuvuta hewa ya chooni. Huniwezi kwa principle sio tu ya elimu bali maisha na upeo wa mawazo ya kitalaam.

Wewe huna kitu unacho kijua zaidi ya kuchangia hoja za kikanga kanga na majungu kama haya unayo yatoa hapa?

Niambie una mchango gani wa mawazo au Idea umewahi kuchangia katika jamii ikawa na impact katika maisha ya watanzania?

Off course hujasoma. Huo ni ukweli. Na ukweli utabaki kuwa ni ukweli. Una elimu gani wewe ya kumtambia mtu? Una weza leta mawazo ambayo yanaweza leta manufaa kwa wananchi? Niambie yapi? Wewe mwenyewe hujui utakula nini sembuse kuchangia mawazo ambayo yanaweza tatua matizo ya binadam?

Wewe unafikiri kushinda mitandaoni na kutoa comments za ki local kwa kutumia device ambayo ni visio na innovation ya mtu ambaye alikuwa shoga ndiyo unajiona kuwa una akili? You know nothing brother!

Eti mimi nimechanganyikiwa. Nimechabganyikiwa mimi au wewe? Nikikuuliza nini maana ya "Material science" unaweza nipa jibu sahii? Unajua maana ya Martensitic Transfomation kwenye material science ni nini?

Nimesha kueleza mara nyingi sana kwenye mtandao kama unachangia hoja basi changia hoja na sio kudiscuss personal issues. Na vile vile nimekuambia usipende kuwazarau na kuwatukana watu usio wajua mtandaoni. Huo si ustaarabu wa kuchangia hoja. Lakini wewe inaelekea hunielewi au huwaelewi watu wengine.

Endelea kujidanganya mwenye kuwa wewe ninmwenye akili kwa kutoa comments ambazo ni too shallow na hazina substances.
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Kesho mapema nikiwa ndani ya gwanda langu pa1 skafu ndani ya kirumba
 
Sherehe za uhuru ni za Kitaifa aliyeleta uhuru ni Mwl Nyerere alituachia sherehe hizi na vyama vingi alisema pawepo mfumo wa vyama vya upinzani hili chama tawala kisije kubweteka.Mbowe akiwepo katika sherehe hizo nategemea akijitokeza will be applaused kwa umahili wake wa kutetea demokrasia isibakwe na wanaotetea ubinafsi.wa chama kimoja kinyume na RAI YA MWL NYERERE.

Ni hivi, kuliko kushiriki hiyo hafla ni bora wangeshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwa taarifa yako kushiriki hiyo sherehe ni kuua madai yote halali. Huu utetezi unapitia hapa ndio utetezi tuliopewa wakati Lowassa kapewa nafasi adhimu ya kugombea urais, yaani ni aibu hata kuendelea kufanya utetezi wa huu uamuzi wa kijinga. Ususie uchaguzi kwa madai halali ya rafiki, kisha ukatetee demokrasia isibakwe kwenye hafla ya robo saa? Mungu aniongezee muda niendelee kuona hivi vituko.
 
Tatizo ni dogo,wewe sio mwanasiasa waache wanasiasa wafanye siasa. Hizi ni mbinu za kisiasa kama hawana mikutano ya hadhara,hata ya ndani tu imedhibitiwa hata ya wachaguliwa ni shida unafikiri ili kila mtz ajue cdm bado IPO ni mbinu gani zitumike?!?. Acha aende atambulishwe mbele ya halaiki hiyo hapo ndio utapata jawabu. Kwa sasa usilalamike ndg yangu

Kuzuiwa kwa mikutano ilipaswa kwenda mahakamani kupata tafsiri ya kisheria, hata kama mahakama itatoa uamuzi wa kupindisha lakini hoja za kisheria zitakuwa zimewekwa wazi, kwani hiyo hafla ya uhuru ndio sehemu cdm wataendelea kufahamika kuwa wapo? Ni hivi huyo Mbowe kashakata moto, ni vyema akapisha sura mpya maana hana jipya.
 
Back
Top Bottom