Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

Mbowe "Tunu ya Taifa" 😂😂😂hafungwi Kama Besigye
 
Ni kweli wanaumbuuka, ila wao wana agenda yao na pengine hiyo ndio muhimu zaidi kwao.
Hapana Salary slip, review upya maoni yako. Kesi hii kuanikwa hadharani ni muhimu sana kwa mustakabali ya haki nchini. Acha mvua iendelee kunyesha ili tuone panapovuja. Huko mbele hata walipoweka lami patadondosha maji.
 
Serikali siyo wajinga kumfungulia Mbowe kesi ya ugaidi. Mbowe mwenyewe anajuwa namna alivyolikoroga.

Muulizeni kati ya Desemba 2020 na March 2021 mpaka tunamzika DIKTETA Magufuli alikuwa wapi? Muulizeni ni kitu gani aliomba kwenye ubalozi wa Denmark na alijibiwa nini?

Nendeni na ubalozi wa Canada mkaone status ya papers zake kwa alichokiomba. Mmasingizia alikuwa kwenye biashara zake Dubai, ana biashara gani Dubai?

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?

Mbowe alitaka kuweka nchi kwenye status of instability immediately baada ya uchaguzi kukamilika. Serikali ilipogundua njama ndipo akalazimika kukimbia.

Nani kasikia masekondari ya shule za Kisslami yanachomwa tena baada ya Mbowe kuwa mikono salama pale Ukonga?

Na kwa kiasi kikubwa amshukuru Samia ambaye ameacha Mahakama itende haki kwani ingekuwa hajawahi kukimbia nchi wakati wa Mwendazake, saa hizi Mbowe angekuwa na msaidizi wake Ben Saanane huko kuzimu.

Nashangaa Wana CDM mnamtukana Rais SSH eti DIKTETA mwanamke wakati ameacha uhuru wa habari na utawala wa sheria uendelee.
Haya hukuona Kingai ili umpe ayaseme mahakamani? Mbona alipoulizwa kama Mbowe alikimbia kesi alikanusha mahakamani? Au kati yako na Kingai Nani shahidi muhimu? Kumbe wanaposema kesi hii imetengenezwa na Usalama wa taifa na kukabidhiwa Polisi wamalizie wako sahihi? Maana Polisi tunaowajua wasingeweza kutengeneza upuuzi wa aina hii wakaiiita kesi ya Ugaidi. Tangu 1998 Polisi wa Tanzania wanaujua Ugaidi baada ya kufundishwa na Wamarekeni, TISS ndo wamebaki wabangaizaji na wabambikia kesi wakiongozwa na think tanks za Makonda na Sabaya.
 
Kwahiyo wewe mawazo YAKO ni yapi zaidi ya kutuletea mawazo ya Lema?

Unajua implications za hiyo hatua anayopendekeza Lema?

Unajua kuwa Lissu tangu mwanzoni mwa hii kesi alifikiri hivyo na baadae wakabadili approach?Unajua kwa nini walibadili?

Unajua kuwa upande wa utetezi au jamhuri muda wowote wanaweza kuomba mabadiliko ya jaji kama wanakuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo?
 
Wakijitoa sasa hivi MATAGA watasema mawakili wa mboe wameona wamezidiwa na hivyo kuamua kujitoa,kwa hali ilivyo bora wapambane kupAngua ushaidi mpaka mwisho ili wote tuone vioja vinavyoendelea huko mahakamani
Wiki iliyopita tu walizusha kwamba Kibatala kajitoa kabaki Mtobesya.
 
Sio wazo baya, ila mimi nashauri waombe mwenendo wa kesi toka kwa jaji, kisha hapo wataona nini jaji anaandika, baada ya hapo watajua nini kinaendelea nyuma ya pazia. Wakiona mwenendo wowote uonaoacha shaka, ambao nina uhakika upo wachukue uamuzi wa kujitoa kwani hawana imani na mahakama. Nasisitiza waseme hawana imani na mahakama na sio jaji tu. Kisha wairuhusu mahakama itekeleze inachoagizwa na serikali.
Nadhani kwa hii comment mjadala umesha ufunga
Pale hakuna kesi ni ubabaishaji tu wa mahakama za ccm.
 
Kitu ambacho Mbowe anatakiwa kukaa nacho mbali kwa sasa na akitoka salama ni ushauri wa Lema na Lissu.

Si ajabu ni ushauri wao ndio uliomfikisha huko alipo na wenyewe washasepa.

Ni watu hao hao walimshauri pia CDM isusie viti maalum bila ya ridhaa ya hakina mama, matokeo yake wakavichukua kwa mlango wa nyuma na kupelekea mgawanyiko.

Kuondoka kwa hakina Halima Mdee kumeacha pengo kubwa sana CDM. Mbowe mahakama ndio itaamua mwisho wa siku. Pamoja na hayo Halima Mdee alikuwa mzuri sana kwenye kutoa pressure serikalini na mhamasishaji yaani hii kesi ya Mbowe angeigeuza ya ukandamizaji wa demokrasia kwa namna yake ya kuleta vurugu huko mahakamani.

Mfano polisi kuwapangisha mstari kuingia ndani ya mahakama au treatment zingine CDM wanazopewa wakienda mahakamani angetumia fursa hiyo kutengeneza mazingira ya uonevu wa polisi na ku associate na kesi yenyewe huku kesha kura virungu kadhaa na nundu za kuonyesha.

Mama juzi alikuwa Glasgow zile picha na wababe wa dunia sio photo shop maana yake huko kwa mabeberu awajali kesi ya Mbowe; sasa akiacha kupigana mwenyewe si anakwenda jela kirahisi bila ya kupambania uhuru wake.

Mbowe kwenda jela sio suala zito. Comes with the territory. Huwezi kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ukawa salama Tanzania. Haiwezekani. You have to pay the cost to be the boss. Leo hii tungekuwa na namna ya kupiga hesabu ya gharama zinazoingiwa na serikali katika kuunda na kuendesha machinery ya kupambana na CHADEMA tungetishika.

Huyo Halima Mdee na wenzake wameshakuwa neutralised kwa vijisenti. Wameshapoteza credibility. Huko CCM hakuna anayetilia maanani kauli zake hata akifoka namna gani. Polisi ndio wameshampuuza kabisa as a nonentity.

Angeleta vurugu mahakamani? Polisi wepi wangemruhusu hata afike huko mahakamani? Angetekwa njiani na kufichwa. Na kiwango kilichofikiwa ilibakia kubakwa kabisa wasiwe na sauti tena. Acha Mbowe na CHADEMA waendelee kubeba msalaba wao wa kuwapigania Watanzania wasiokuwa na ujasiri wa kusimama kidete kutetea haki zao.
 
Kwahiyo wewe mawazo YAKO ni yapi zaidi ya kutuletea mawazo ya Lema?

Unajua implications za hiyo hatua anayopendekeza Lema?

Unajua kuwa Lissu tangu mwanzoni mwa hii kesi alifikiri hivyo na baadae wakabadili approach?Unajua kwa nini walibadili?

Unajua kuwa upande wa utetezi au jamhuri muda wowote wanaweza kuomba mabadiliko ya jaji kama wanakuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo?
Wapi alibadili approach? Una ushahidi?
 
Ni kweli wanaumbuuka, ila wao wana agenda yao na pengine hiyo ndio muhimu zaidi kwao.
Salary Slip, ukikaa kimya maana yake ni nini? Si watapata sababu kwamba umedharau mahakama? Dunia itapata wapi ufafanuzi kwamba huna hatia? Kesi iendelee hadi mwisho, ili ijulikane nani muongo na nani mkweli.
 
Wenye nguvu ya maamuzi kesi ya mbowe ni familia na sio chama acheni kujidanganya mitandaoni. Chama kiliisusa kesi,familia wakaingilia kati

Yeye lema katolea mfano uamuzi wa mkewe. Hivyo ujumbe wake ungemlenga mke wa mbowe au mchepuko mkuya(kama ana nguvu za kifamilia)
Saada Mkuya ni mchepuko wa Mbowe!!???
 
Serikali siyo wajinga kumfungulia Mbowe kesi ya ugaidi. Mbowe mwenyewe anajuwa namna alivyolikoroga.

Muulizeni kati ya Desemba 2020 na March 2021 mpaka tunamzika DIKTETA Magufuli alikuwa wapi? Muulizeni ni kitu gani aliomba kwenye ubalozi wa Denmark na alijibiwa nini?

Nendeni na ubalozi wa Canada mkaone status ya papers zake kwa alichokiomba. Mmasingizia alikuwa kwenye biashara zake Dubai, ana biashara gani Dubai?

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?

Mbowe alitaka kuweka nchi kwenye status of instability immediately baada ya uchaguzi kukamilika. Serikali ilipogundua njama ndipo akalazimika kukimbia.

Nani kasikia masekondari ya shule za Kisslami yanachomwa tena baada ya Mbowe kuwa mikono salama pale Ukonga?

Na kwa kiasi kikubwa amshukuru Samia ambaye ameacha Mahakama itende haki kwani ingekuwa hajawahi kukimbia nchi wakati wa Mwendazake, saa hizi Mbowe angekuwa na msaidizi wake Ben Saanane huko kuzimu.

Nashangaa Wana CDM mnamtukana Rais SSH eti DIKTETA mwanamke wakati ameacha uhuru wa habari na utawala wa sheria uendelee.
Kwa kuwa unazo taarifa za alichokiomba na alicho jibiwa katika balozi ulizo zitaja, ni vyema ungeziweka wazi taarifa hizo ili kuimarisha hoja yako.
Gaidi ni mtu hatari sana duniani,Je serikali ilishindwaje kumkamata mtu hatari namna hiyo popote alipokuwa? Mbowe alirudi nchini kwa hiyari yake, Je ilichukuwa muda gani adi kukamatwa kwa mtu hatari aina hiyo? Wakati mbowe anarejea nchini tuhuma za ugaidi kumuhusu zilikuwepo ama zilijitokeza baada ya mbowe kuwepo nchini?
 
Siku chache zilizopita, nilileta mada hapa niki-suggest Mbowe aacha kujitetea mbele ya hizi mahakama zetu kutokana na mwenendo mzima wa hii kesi. Leo hii kupitia You tube, nimemsikia Godbless Lema akimshauri Mbowe aondoe mawakili na akae kimya mahakamani ili wafanye kile wanachokita. Lema pia kaongea na katibu mkuu wa chama na anapanga kuongea na makamu mwenyekiti wa chama kuhusu jambo hili. Isitoshe, Lema kakumbusha uamuzi wa mke wake kutoa mawakili wakati ule wa kesi ya yake alipokuwa ananyimwa dhamana.

Katika kufafanua, Lema kataja mapungufu kadhaa yanayoonekana katika hii kesi na mfano mmojawapo ni Jaji kutumia mawazo yake(opinion) kufanya maamuzi badala ya kutumia vifungu vya sheria katika kuamua mapingamizi. Mbali na kutaja mapungufu yanayojitokeza, Lema anahoji kama katika hatua hizi za mwanzo taratibu zinakikuwa, tunatarajia kweli hukumu itakuwa fair?(swali la msingi sana hili).

Binafsi naungana na Lema kuwa kuna umuhimu wa kuondoa mawakili na Mbowe akae kimya mahakamani tuwaache wafanye wanalotaka kufanya. Hapa tunarudia kosa lilelile la kuwa wagumu kufanya maamuzi kama tulivyofanya kwenye kususia chaguzi zinazoendeshwa na hii tume ya uchaguzi isiokuwa huru. Na hapa niwaambie tu, wakifanikiwa kumfunga Mbowe halafu tukalalamika kuwa taratibu zilikiukwa, majibu yao(MATAGA) yatakuwa mawili: (1) kwanini hamkujitoa (2)Mkakate rufaa kama hamridhiki na maamuzi ya mahakama.

Kuhusu hili la kusubiri kwenda Mahakama ya Rufaa kupinga kitachoamuliwa, naungana pia na Lema kupinga hoja hii kwani hata hao Majaji wa Mahakama ya Rufaa upatikanaji wao ni ule ule wa kuteuliwa na Raisi,hivyo bado lolote linaweza kutokea. Kwahiyo, nashauri viongozi wa CHADEMA na wana familia ya Mbowe watafakari upya kama ni sahihi kuendelea kuweka mawakili mahakamani au Mbowe akae kimya na awaache waamue wanavyoona inafaa.
View attachment 2001948
Mbona yeye aliikimbia nchi Kama rahisi hivyo.
 
Ben Saanane yuko kuzimu?!

Back
Top Bottom