Mvinyo mpya
JF-Expert Member
- Aug 24, 2013
- 3,816
- 9,308
Sio lazima ujibu kwa kashfa. Mimi nimesema ile list ya vyama vilivyopinga case yake itasaidia vipi. Hilo unashindwa kujibu wewe mwerevu?Weee kilaza kwel Kwa iyo huku uvccm unataka waone umesema Actus reus na men's rea waone umefanya kazi ya buku 7? Mbona majaj na mawakili wa serikali wamekaa kmya ww mweny gpa ya 2.3 unaongea nn ?
Una kichwa kizito kwel uliwezaje kusoma Sheria Kwa kichwa hicho? Huon anaweka msingi na alisema kabsa ushahid wake hautaisha Leo ? Hata mwanafunzi wa certificate anaweza kuelewa anaweka faundation ya utetez wakeMmh napata shida kidogo. Hao waliolaani itamsaidia vipi? Na hiyo historia ya kupigania haki itasaidiaje kwenye shtaka lake.
Nilitamani ajikite kwenye elements za uhaini akidili na actus reus na mensrea na kwamba hajafanya chochote kati ya hayo.
Yaani Kuna saa unakaa unaumia serikali kuamua tu kumpa mtu case nzito bila hata aibu.
NotedUna kichwa kizito kwel uliwezaje kusoma Sheria Kwa kichwa hicho? Huon anaweka msingi na alisema kabsa ushahid wake hautaisha Leo ? Hata mwanafunzi wa certificate anaweza kuelewa anaweka faundation ya utetez wake
Kumbe kuna muda unakuwa na akili?!kwa utetezi huu ni wazi atashinda kesi inayomkabili 🐒
Let me rest the case with you ,Sio lazima ujibu kwa kashfa. Mimi nimesema ile list ya vyama vilivyopinga case yake itasaidia vipi. Hilo unashindwa kujibu wewe mwerevu
Mzee subiri aje msingi wa utetezi kwanza kwani hao machawa wenzio wameshapoteza muda kiasi gani mpaka sasa Tulia mwanaume ajenge hoja wewe jizi la ccmWastage of time.
Uko sahihi kabisa, ingawa kwa kiasi kikubwa watesi wake wamejikuta wana rise political status yake na kushusha za kwao huenda pasipo wao wenyewe kujua hiloKuna sababu nyingi zilizomfanya ajitetee mwenyewe;
1. Kuonesha umahiri wake kwenue sheria! Yeye ni mwanasheria na pia ni wakili msomi.
2. Kutuonesha wananchi na dunia kwa ujumla namna bora ya kupigania haki.
3. Kiwaonesha watesi wake namna alivyo jasiri na shupavu kwenye kupigania kile anachokiamini.
4. Kujiongezea umaarufu wa kisiasa kwa maandalizi ya safari yake ya kuufikia uongozi wa juu kabisa nchini (Urais).
Na kwenye hili, hakika amefanikiwa pamoja na mateso yote anayopitia
Huku mtaani kwa sasa habari ni Lissu tu! Lissu ni Shujaa! Lissu ni mpambanaji wa kweli!, Lissu ni mzalendo kwa nchi yake, Lissu ni mwanasiasa wa kweli, nk. Hakuna cha nani wala nani! Habari ya mjini ni Lissu tu.
Kati ya wewe na hao majaji waliotulia wanamsikiliza na wanachukusa notes kabisa, mbumbumbu wa sheria ni nani??okay,
anawataja hata ambao hawamjui na wala hawasaidii chochote kwenye kinachomkabili, dah.
kifo cha nyani ni cha fedheha sana aise, miti yote huteleza 🐒
Aliyenikamata wakati huo alikuwa Senior Superintendent of Police Ramadhani Kingai, leo ndiye...
Majaji: Hebu subiri kidogo.
Mahakama inakaa kimya kidogo, wanaandika.
Mmmh Kwan hii kesi yake Leo ndo umeanza kufuatilia? Hakumbuki alinyimwa haki ya kuonana na mawakili wake ,na akionana nao askari magereza wanakaa pemben ya lissu? Kwa iyo Hajui Kwa nn aliamua kujitetea mwenyew? Na umesema hapo juu upo kwenye tasnia ya Sheria?Hahaha 😂
Ningekua yeye ningejikita kwenye uhaini. Lakini sijui kwanini Lissu kaamua kujitetea mwenyewe. Hiyo case ni nzito na tena ya uonevu. Angekuwa na wakili wake kwa maoni yangu angejitetea vizuri zaidi.
Maanzisha mapambano ya kudai haki, misingi ya demokrasia na utawala wa katiba na sheriaANAENDELEA TUNDU LISSU
SEHEMU YA 3.
Tume iliundwa mwaka 1991, ilikuwa inahoji watu, na mimi nilikuwa mmoja ya watu waliohojiwa.
Nilikuwa mmoja ya watu waliotoa ushuhuda mbele ya Profesa Haroub Othman, ambaye alikuwa mwanazuoni maarufu.
Secretary wa Tume alikuwa baadaye Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, January Msofe.
Kwa hiyo, nimepigania mfumo wa mabadiliko kwa namna hiyo.
Kwa kwenda mbele ya Tume ya Rais kutoa ushuhuda.
Na mwaka 1992 niliacha kusoma chuo nchini Uingereza, nikaja kugombea kwa sababu siku zote nimekuwa concerned na masuala ya ustawi wa nchi hii.
Waheshimiwa Majaji, kwa miaka yote iliyofuata mpaka leo, nimepigania demokrasia, Katiba mpya, mfumo huru wa haki na uchaguzi.
Sijawahi kupumzikaaaaa.
Nje ya kupigania demokrasia, Waheshimiwa Majaji, nimepigania haki za wananchi wa kawaida.
Waheshimiwa Majaji, mwaka 1997 Serikali ya Rais Mkapa iligawa eneo karibu lote la Delta ya Mto Rufiji kwa mwekezaji mmoja wa Ki-Irish.
Ili alime kamba (prawns), wale wadudu wa baharini watamu watamu, enheeeee, kamba.
Kamba ni wadudu wa baharini, lakini wanafugwa.
Waheshimiwa Majaji, najua mmesoma kesi ya Reginald, alikuwa anauzia nchi vifaa vya kijeshi chakavu.
Sasa Mkapa na Serikali yake wakampatia hekta elfu 20 za Delta ya Rufiji ili afuge kamba.
Kama hilo lingefanikiwa, pasingekuwa na msitu wa mikoko katika ile Rufiji tunayoiona leo.
Na kwa tafiti za kitaalamu, ingedhuru maisha ya watu laki moja.
Mimi pamoja na wenzangu, akiwemo Dkt. Nshala...
Hawa ni mashujaa, mnatakiwa muwajue.
Mimi na wenzangu tulisakamwa sana na Serikali ya Mkapa, na Mkapa mwenyewe pamoja na Makamu wake, Dkt. Ali Juma.
Tukaitwa wanaharakati wa kimazingira.
Tukamkimbiza yule M-Irish.
Tukaokoa msitu wa mikoko wa Delta ya Rufiji.
Hiyo ilikuwa 1997 na 1998.
Waheshimiwa Majaji, siyo Rufiji tu. Nimekuwa mstari wa mbele kupigania haki za ardhi za wafugaji na wananchi wanaoishi katika hifadhi za wanyamapori kama Ngorongoro, Loliondo, Tarime, Meatu, Bariadi Mashariki, Maswa Mashariki na ukanda wote wa mashariki ya Serengeti.
Mwaka 2023 nilikamatwa Karatu, nikizuiwa nisiende Ngorongoro kuwaona Wamasai niliokuwa nawapigania tangu mwaka 1996.
Nimepigania haki za wananchi wa maeneo ya ukanda wa mashariki wa Ziwa Tanganyika, kama Nkasi, na ukanda wa Pwani wa Mkoa wa Kigoma.
Maeneo ya wavuvi wa ukanda wote wa Ziwa Victoria, kutoka ukanda wa ziwa magharibi mpaka wa Uganda, pamekuwa na ukiukwaji wa kutisha wa haki za raia.
Watu wanauawa na vyombo vya ulinzi. Inatisha sana.
Mkuu Manyanza Mungu akubariki Sana hili darasa analotoa Lissu ni habari nyingine.TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA
SEHEMU YA 5.
Kama mkishawishika na hoja na ushahidi wa Mawakili wa Serikali, ni kifo.
Msisambwe, ooh sijui kuna nini, bali ni kifo. You don't get more serious than this.
Waheshimiwa Majaji, leo nakabiliwa na kesi kubwa kuliko zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hii ni mwendelezo wa kesi nyingi za jinai ambazo nimewekewa na Serikali hii, Polisi na Mawakili wake.
Waheshimiwa Majaji, sina hakika na watu wengine nje ya chama changu CHADEMA.
Lakini ndani ya CHADEMA, mimi ndiye mwanachama na kiongozi ambaye nimeshitakiwa mara nyingi kuliko kiongozi au mwanachama yeyote.
Waheshimiwa Majaji, na kesi zote ambazo nimefunguliwa zimekuwa ni kesi za kisiasa.
Zimetokana na matendo yangu, kauli zangu na misimamo yangu ya kisiasa.
Waheshimiwa Majaji, tuanze na utawala wa Marehemu Rais Mkapa.
Mwaka jana, Waheshimiwa Majaji, wakati wa Christmas, mwanangu mmoja alinitumia ujumbe kwamba:
“Baba, upo gerezani, unatukumbusha kwamba Christmas yetu ya kwanza duniani ulikuwa gerezani.”
Wakati wa Mkapa, nilikamatwa tarehe 23 Desemba 2002, siku mbili kabla ya Christmas, kwa kosa la uchochezi.
Wanazungumza sana uchochezi watu hawa.
Sababu gani?
Kwa kuongoza kampeni ya kudai mauaji ya wananchi wa Bulyanhulu yachunguzwe, baada ya watu zaidi ya 60 kufa.
Kwa kudai mauaji haya yachunguzwe, nikakamatwa nikapelekwa Makao Makuu ya Polisi, Shimoni.
Pale chini kuna gereza linaitwa Shimoni. Pale wanajaza watu, wengine wanakaa miezi.
Kwa bahati nzuri nilikuwa maarufu, wakanipeleka mahakamani siku ya Christmas.
😂😂😂😂😂
Walimpata wapi Hakimu sijui, ila akanisomea mashitaka, akaniambia ondoka hapa.
Uchunguzi ulikuwa miezi 6.
Walioshitakiwa wenzangu walikuwa Augustine Lyatonga Mrema na Dkt. Lugemeleza Nshala, ambaye leo ni Wakili wangu.
Kosa ni kudai uchunguzi wa mauaji ya wananchi.
Miezi 6 wakaifutilia mbali baada ya kukosekana kwa ushahidi. Wakashindwa kuleta mashahidi.
Mwaka 2005 akaingia Jakaya Kikwete.
Waheshimiwa Majaji, nilizungumzia Tarime, ipo karibu sana moyoni mwangu.
Mwaka 2005, Julai, nikiwa Mbunge, Polisi walifanya mauaji eneo la Nyamongo, wakaua watu 3 (wanakijiji).
Nikiwa Bungeni, wananchi wa Nyamongo wakanipigia simu: “Mheshimiwa, inabidi uje. Polisi wameua na wanataka tuzike, tumegome. Njoo.”
Nikaondoka Bungeni, nikaenda Tarime kudai uchunguzi wa mauaji yale ufanyike.
Nilipofika Tarime, tukapata taarifa kwamba Polisi wana mpango wa kutaka kuvunja milango ya chumba cha kuhifadhia maiti ili waibe maiti.
Tukaenda kuweka kambi chumba cha kuhifadhia maiti ili Polisi wasiibe maiti.
Tukapigwa sana. Kuna picha maarufu Polisi wamenichania combat yangu, ila picha ni ya Tarime.
Nikapigwa vibaya sana. Wakanichania combat yangu, tukakamatwa, tukapelekwa kilomita 40 nje ya Tarime. Kesho yake tukashitakiwa kwa criminal trespass.
Nikapelekwa Gereza la Wilaya ya Tarime siku 4. Pale nilipokuwa natoa wenzangu, safari hii nikawa mimi ndiye mfungwa.
NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI