Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Duuu ! Mpambano ni mkali,,,,busara itumike tu hapo..Wote ni Watanzania....Tupendane tuishi kwa umoja tutoetofauti zetu za kisiasa,kidini, kikanda na n.k Tuijenge Tanzania yetu.............Mungu awasimamie Majaji wa kesi hiyo waweze kutenda haki na watoe maamuzi yaliyosahihi.....Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki viongozi wote ikiwemo na wasimamia...Amani na Haki.
 
Mwamba anawaumbu hat1ei maana anasimuli1 Histori nzima,ili kila mmoja ajue tulikotok1 na wapi anataka tufike,jamaa vizazi vitamkumbuka
 
Chawa,
Mbona umepiga kambi kwenye huu uzi, na unabwabwaja pumba tu kila muda?
tuliza mihemko gentleman,
hakuna haja ya kuweweseke na maoni yangu dhidi ya porojo za huyo mtuhumiwa anae mbwelambwela nonsense kizimbani mahakamani 🐒
 
Amen
 

Kesi/shauri lolote ile linayoletwa mbele ya mahakama; huwa lina "Point of weakness" or holes. Kazi ya upande wa utetezi huwa ni ku challenge ushahidi husika "poking holes".

Kuhusu swali lako; kwenye hii kesi TL ameamua kujitetea mwenyewe kwa sababu moja kubwa. Watesi wake wanaogopa kelele zake, kelele zake zinawakera na ni kelele hizo hizo zinaweza kuwafanya wakaondoa hii kesi.
Pili, hii ni kesi ya kisiasa, na yeye kama "learned brother" kaona namna nzuri ya kudeal na kesi ni kudel nayo kisiasa. Kibatala & Co wasingeweza kusema anavyosema yeye mbele ya mahakama.
Mwisho: Sio kwamba mshitakiwa akijitetea mwenyewe basi hana/hakuna mkono wa mawakili. Mawakili wanaweza wasiende kortini lakini wakachora michoro yote ya kesi na kumfubdisha mshitakiwa namna ya "poke holes". Hivyo TL yupo sahihi kujitetea mwenyewe.
 
Hatoki mtu kwenye Reli hapa
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 15
Ndiyo imetufikisha leo hii hapa na kesi ya uhaini.

Ijumaa nilisahau kuwaambia kuwa mwaka 2020 nilirudi kutoka uhamishoni kuja kumkabili Magufuli.

Nikagombea Urais mwaka 2020, na ni wazi sikuchaguliwa. Ningechaguliwa, leo nisingekuwa hapa.

Sheria ya uchaguzi wakati ule palikuwa na kifungu kwamba matokeo ya uchaguzi yatatangazwa jimbo kwa jimbo na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.

Ninachotaka kusema, zamani Tume ya Uchaguzi ilikuwa inatangaza matokeo ya uchaguzi katika Gazeti la Serikali, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo na ya Urais.

Mwaka 2020 kuna matokeo ya uchaguzi kata kwa kata na jimbo kwa jimbo.

Lakini hakuna matokeo ya Urais ya 2020 yanayoonyesha Magufuli alipata kura ngapi.

Na kamwe hamtokuja kuyaona. Kwa nini? Ni kwa sababu Tume ni ya ki-CCM.

Na sina uhakika kwamba matokeo ya mwaka jana, kama yenyewe yalichapishwa gazetini.

Kuna mambo ya ajabu nchini yanaendelea.

Soma ripoti ya Tume ya Uchaguzi kila mwaka, lazima kuna wadudu.

Uchaguzi wa 2020 ulitia fora kwa wabunge 28 kupita bila kupingwa baada ya wapinzani wao kuondolewa na Tume, wengi wao wakiwa ni CHADEMA.

Tume ambayo Mkurugenzi wake leo ni Mbunge wa CCM.

With Magufuli, ikawa ilikupambana na CHADEMA ni kuwaengua wagombea wa CHADEMA nchi nzima.

Mwaka 2019, wagombea wote wa Serikali za Mitaa wa CHADEMA walienguliwa.

2020 palikuwa na mass disqualification. Walikuwa wagombea 68, wakabaki 34 baada ya kupambana.

Madiwani pia mass disqualification, na mara nyingine mwaka 2020 pakawa na mauaji sana.

Kwa uchaguzi wa 2020, ukisoma taarifa za watazamaji wa uchaguzi wa kimataifa, wakiongozwa na watazamaji wa Umoja wa Afrika, utakubaliana nao kuwa hapakuwa na uchaguzi.

Palikuwa na vurugu, vurugu za Polisi na usalama wa taifa.

Wagombea wetu wanatekwa na Polisi pamoja na Usalama wa Taifa.

Niliposema Polisi wanatembea na vibegi migongoni, huo ni ukweli kutoka moyoni mwetu.

Ripoti ya uchaguzi 2020 ilikabidhiwa Rais Samia Agosti 2021.

Na katika sherehe ya 2021 ya kukabidhiwa ripoti, Samia alisema hivi: “Tuliwapiga fiksi, tukawaengua.”

Watazamaji wa kimataifa wa uchaguzi wakasema bila mabadiliko ya Katiba mpya na sheria ya uchaguzi, 2025 itakuwa maafa.

Ripoti ya watazamaji wa kimataifa kutoka Afrika ilikuwa bora sana.

Walisema Tanzania haina uwezo wa kuendelea kuendesha uchaguzi bila maafa kama hawatakuwa na Katiba mpya, tena ya Warioba, na Tume huru ya uchaguzi.

Hao ni waangalizi wa Afrika.

Magufuli akafa, akaja Samia.

Mwenyekiti wetu akadai Katiba, akafunguliwa kesi ya ugaidi, akakaa Ukonga miezi 8, pale ninapokaa mimi.

Tukapambana na kesi ya uongo.

Siku ya kutakiwa kujitetea hatukumuona, bali akatokea Mahakamani Ikulu.

Na jana nimeambiwa alikuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere wakati Mwenyekiti wake nikiwa Magereza.

MAHAKAMA: Kicheko.

Wakili wa Serikali Mkuu anasimama.

“Samahani, Waheshimiwa Majaji, muda wa mapumziko.”

Lissu: “Hilo naliunga mkono, Waheshimiwa Majaji. Nilisahau kidogo.”

MAJAJI: Wanateta.

Askari Magereza wanasogea katika kizimba cha shahidi.

Lissu amebadilishiwa kizimba kutoka kile cha mshtakiwa; siku hizi 2 anatumia kizimba cha shahidi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Majaji wakimtia hatiani Lissu Kwa uhaini Kwa kesi hii, basi watakuwa wanajiaibisha.

Watanzania mtu akijiamini mnaona ni "Arrogant". Hii kesi imeshusha viwango vyote vya uhaini na kuifanya ionekane kituko.

Jinsi anavyowahoji mshahidi ulitaka awahoji vipi? Nini alikosea kwa mfano?
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

Anasimama tena Wakili Mkuu wa Serikali: “Waheshimiwa Majaji, kama itawapendeza, tunaomba lisamili moja la mapumziko.”

Lissu: “Mheshimiwa Jaji, sasa hivi ni saa 7 na dakika 10. Naomba turudi saa 8 na nusu.”

Jaji Ndunguru: “Naomba tukirudi unalizie ushahidi.”

Lissu: “Sijui, ila tutaenda enda.”

Jaji Ndunguru: “Hutamaliza?”

Lissu: “Tutakuwa tumeenda enda, kama siyo kumaliza.”

Jaji Ndunguru: “Jitahidi ya historia ufupishe, hayo utawaandikia kitabu.”

Lissu: “Ushahidi wangu ndiyo mrefu pekee.”

Jaji Ndunguru: “Tuweke malengo, tumalize leo.”

Lissu: “Tutaenda enda, Waheshimiwa. Siwezi kusema tutamaliza leo. Sijui Mawakili wa Serikali wanawaza nini.”

Jaji Ndunguru anaahirisha kesi.
 
Kwa ule ushahidi wa republic ilitakiwa ruling ya kutokuwa na case ya kujibu. Sidhani kama majaji wapo huru! But I hope Lissu atatoka iwe kwa nolle au kuachiliwa huru na mahakama
 
Nadhani hii hotuba itakaposambaa mitandaoni utapata itapokelewa kipekee.
nadhani uamuzi wa mwisho wa jopo la majaji ndio itakua hotuba nzito, fupi na ya maana zaidi ulimwengu unapaswa kuipa attention kuliko kumbwelambwela kwa huyo kibaraka mropokaji 🐒
 
nadhani uamuzi wa mwisho wa jopo la majaji ndio itakua hotuba nzito, fupi na ya maana zaidi ulimwengu unapaswa kuipa attention kuliko kumbwelambwela kwa huyo kibaraka mropokaji 🐒
Tangu nilipoambiwa hii akaunti ni ya kundi... Huwa napita tu maana hujui unajibishana na mtu mmoja ama kundi Zima😄😀😆
 
hao wanamsikiliza kwa makini huku wanasikitika,

wanatamani walau wapate hata kapointi ka moja
Kumbe akili kisoda wewe,
Hujaona majaji wenyewe wanaomba subira waandike hayo madini ya TAL??
👇
Majaji: Hebu subiri kidogo.

Mahakama inakaa kimya kidogo, wanaandika.

Waheshimiwa Majaji, nimesema nilikamatwa na Senior Superintendent of Police akiwa Deputy ZCO wa Dar es Salaam....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…