Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

gradually, my fellow, the tide is turning for the better.
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Ajuaye: “Ni kweli kwamba video ni kifaa ambacho kinachapisha tu?”

Lissu: “Eheeeeee, hayo siyajui. Wanajua wataalamu.”

Ajuaye: “Unaniuliza mimi swali tena? Subiri nikishitakiwa, na mimi nitakukodi uniwakilishe kama wakili.”

Lissu: “Mimi huwa siwakilishi wateja wa namna yako wanaosingizia watu kesi.”

Ajuaye: “Ulisema kwamba mashahidi ni wahalifu?”

Lissu: “Nyie ndiyo mliwaleta, wakasema wao ni wahalifu.”

Ajuaye: “Ili mtu awe mhalifu atathibitishwaje?”

Lissu: “Na Mahakama.”

Ajuaye: “Mbona unasema wale mashahidi ni wahalifu?”

Lissu: “Nilisikia katika ushahidi wao wenyewe kwamba kesi zao zilifutwa ili waje kuwa mashahidi dhidi yangu.”

Ajuaye: “Nilisikia una challenge committal?”

Lissu: “Ndiyo.”

Ajuaye: “Ulichukua hatua gani?”

Lissu: “Nilileta kwa Majaji hapa mbele ya Mahakama kwamba hakimu amekataa.”

Ajuaye: “Unajua hiyo ni serious allegation?”

Lissu: “Ndiyo.”

Ajuaye: “Tukiangalia proceedings tutaona. Wewe ni mwanasheria?”

Lissu: “Unataka ukute nini, kama hakimu ndiye anayeandika committal?”

Ajuaye: “Ulichukua hatua gani?”

Lissu: “Nilileta kwa Majaji hapa. Au ulitaka nichukue hatua gani?”

Ajuaye: “Unajua kuna tofauti kati ya kuzuia uchaguzi na kupinga matokeo ya uchaguzi?”

Lissu: “Nafahamu, ila sisi tulikuwa tunapinga uchaguzi mpaka mabadiliko ya uchaguzi yafanyike.”

Ajuaye: “Ni kweli ukilenga kuzuia uchaguzi, unalenga kuzuia shughuli za uchaguzi?”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Mkuu kama hujui sheria mahakamani utaacha ndala, lissu ameshahudhuria mahakamani hao wakiwa bado wanafunzi, tena wakifanya mitihani ya multiple choice😄, lisu anasema amefundishwa critical thinking, sasa wew jiulize miaka ya 60s kulikuwa na multiple choice?😂 ukijumlisha na experience, hapo hawawezi fua dafu.
 
Ajuaye: “Unaniuliza mimi swali tena? Subiri nikishitakiwa, na mimi nitakukodi uniwakilishe kama wakili.”

Lissu: “Mimi huwa siwakilishi wateja wa namna yako wanaosingizia watu kesi.”

Hivi hawa mawakili wa serikali huwa wanapatikana vipi ? 🤣🤣🤣
 
Haya maswali ndio ya uhaini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…