Kesi ya Uhaini ya Lissu inaendelea Mahakamani, DCI Kingai kutoa ushahidi wake Septemba 18, 2026

Kesi ya Uhaini ya Lissu inaendelea Mahakamani, DCI Kingai kutoa ushahidi wake Septemba 18, 2026

Naomba nikusahishe. Hakuna mahali mahakama imeelezwa uhaini ulivyopangwa na kutekelezwa. Maana mhaini ni mmoja. Ila mahakama ilisema Kuna kesi ya kujibu kutoka kwa mtuhumiwa, kwa sababu hakuna ubishi kwamba yale maneno yalitamkwa. Sasa wanaangalia kama yake maneno yaliambatana na mpango wa uhaini.
Usiingilie kazi ya majaji ....subiri...kama vipi ungeomba kuwa shahidi wa utetezi ukutane na KATUGA
 
DPP huandaa mashtaka (HATI YA MASHTAKA) Ushahidi hukusanywa na DCI. Hivyo wanaobambika kesi ni mapolisi (DCI),. DPP naye huhusika katika kubambika kesi pale anapomshitaki mtu huku akijua kabisa hakuna ushahidi wa kumtia mshtakiwa hatiani.

katika kesi iliyoko mezani watu hawa wawili wameshirikiana kubambika kwa maelekezo ya yule bibi mwenye Lissuphobia
 
Wamesema na Lissu mwenyewe katuambia walichosema. We hayo ya kwamba eti hawana cha kusema umeyatoa wapi kama sio mzushi?
Kama wangekuwa na la kusema wangekubali kuja mahakamani. Shida ni kwamba hawana la kusema ndio maana wanatoa visababu uchwara.
 
Haya nishatulia. Nambie basi wale Mashahidi Wanaharakati ikoje mana leo Lissu keshafunga ushahidi
Wale hawakuwepo kwenye orodha ya mashahidi wakati mahakama inatoa summons ya mashahidi. Inaonekana hawakuwekwa wakati wa commital kesi ilipokuwa Kisutu. Ndio maana mahakama haikuwiata.
 
Usiingilie kazi ya majaji ....subiri...kama vipi ungeomba kuwa shahidi wa utetezi ukutane na KATUGA
Katuga haniwezi kabisa. Halafu majaji wanaamua kesi kutokana na kinachobishaniwa sio kutoka kwenye akili zao.
 
DPP huandaa mashtaka (HATI YA MASHTAKA) Ushahidi hukusanywa na DCI. Hivyo wanaobambika kesi ni mapolisi (DCI),. DPP naye huhusika katika kubambika kesi pale anapomshitaki mtu huku akijua kabisa hakuna ushahidi wa kutosha kumtia mshtakiwa hatiani.

katika kesi iliyoko mezani watu hawa wawili wameshirikiana kubambika kwa maelekezo ya yule bibi mwenye Lissuphobia
Kweli kabisa mkuu
 
Katuga haniwezi kabisa. Halafu majaji wanaamua kesi kutokana na kinachobishaniwa sio kutoka kwenye akili zao.
Usitake kwalisha mawazo....subiri uamuzi na yapaswa tuuheshimu hata kama ni mchungu
 
Ni kweli, ila Lissu alitaka Sasa hao ndio waseme alitaka kupindua vipi serikali?
Sasa haya angeyasema kama wangeenda kwenye Cross Examination, bt Lissu hajafika huko..

Lissu kwa alipoishia leo, maana yake alitaka Kingai akaseme Lissu hana kosa, ndio maana Kingai yule aliyeamuru Lissu akakamatwe Songea, amekataa kuwa upande wa Lissu.

Mimi bado namshangaa Lissu!
 
Naitafuta logic yake hapa sijaiona zaidi ya kutaka kusherehesha audience kitu ambacho Kingai amemnyima.
Hapa pia ndipo ninapoona weledi wa KATUGA Katika kupanga aina ya mashahidi licha ya kuwa na uwezo wa kuwa na mashahidi wengi....
 
Nikujibu TU Kwa faida ya wajinga wenzako

Lengo la Lisu ni kuonyesha jinsi mifumo ya utoaji haki ilivyo na madhaifu makubwa

Unapoitwa na adui yako ulingoni ukakataa Kwa sababu zozote zisizo na mashiko inaashiria umeshindwa kabla ya pambano na unamuogopa adui yako

Ilikuwa ni wakati wa DCI kuonyesha uhaini wa Lisu sio kukukataa
Siyo lazima shahidi kumtetea mshtakiwa

Besides alikuwa na mashahidi wengi tuh ambao walimtetea baada ya mahakama kumkuta na kesi ya kujibu

Na mwenyewe kakubali kufunga ushahidi wake sasa tatizo liko wapi binti yangu?

Subirini maamuzi ya mahakama sasa.
 
Back
Top Bottom