GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi 18 Agosti 2025

GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi 18 Agosti 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hakimu anasema hakuna upande wowote ambao umeeleza vyombo vinavyorusha live vipo kwa mujibu wa sheria gani wakati media zote zinazorusha live hii case zinachukua maudhui kupitia coverage ya Mahakama yenyewe
 
Mchamungu 😆😆angetishia amani ya taifa
Mchamungu angetetea haki za ushoga
Mchamungu angeleta maneno ya hovyoo
Nyie watu mkoje
Wewe mwehu nini ni lini Bunge la ibilisi wa ccm lilitunga sheria kali za kuzuia Ushoga? Kama wewe na ibilisi wenzako hampendi ushoga mbona hamjawakamata mashoga unaoishi nao hapo ghetto kwako unaposhinda ukivuta Bangi,
 
Huyu hakimu ni kibaraka. Kwanini asitoe amri leo? Atatoaje amri siku ya commital?
 
Kwa hiyo kama itakuja kufahamika hapo baadaye kuwa hakuna sheria ya kuruhusu live streaming ya kesi, basi mvunja sheria wa kwanza ni Mahakama yenyewe.
 
Mbowe toka ashindwe kwa kura kwenye uchaguzi wa chadema amegeuka na kuwa Alishababu, Alikaida gaidi wa ndani ya chadema na Dalali wa Siasa kuuza G55 ya Akina Salam mwalimu huko ccm na wao kuwaisokomeza Chauma ubwabwa chama mchepukaji wa ccm
Ndio uone kua wanasiasa si watu wa kuaminika.kma angeshinda kura za maoni mpk saiv mbowe angekua mwiba kwa ccm
Mfano wa mbowe kma haujakupa funzo bhc chukua wa Dr slaa alivoshindwa kura za maoni
Au chukua wa lowasa
 
Shauri la Jinai Na. 8607/2025 Jamhuri vs Tundu Lissu - Mahakama ya Hakimu Mkazi DSM Kisutu

Kesi ya jinai inayomkabili mwanasiasa na mwanasheria maarufu Tundu Lissu imeendelea leo Agosti 13, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Wanafunzi wa mashtaka na wafuasi wa Lissu wamekusanyika nje ya mahakama huku hali ya ulinzi ikiwa imara.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga, anatarajiwa kutoa uamuzi wa hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili. Upande wa Lissu umeipinga mara kwa mara ombi la Jamhuri la kuahirisha shauri hilo bila kuchukua hatua ya kupeleka kesi Mahakama Kuu, jambo ambalo linaleta wasiwasi miongoni mwa wananchi waliokusanyika kufuatilia kesi hiyo.

Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, Agosti 4, 2025, ilikubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa zingine za mashahidi wa upande wa mashtaka, hatua iliyolenga kulinda usiri wa mashahidi na usalama wa mchakato wa kisheria.


Updates

Asubuhi saa 1:00, Wananchi wamefurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Taifa, Tundu Lissu.


Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Joseph Osmund Mbilinyi akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mmoja kati ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akivutana na askari wa Jeshi la Polisi katika Mahakama ya Kisutu ambako kesi inayomkabili mwenyekiti wao, Tundu Lissu, inaendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 13, 2025 ambapo Mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.

Nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wananachi wakisubiri uamuzi wa shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.


Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu haijaanza hadi sasa Saa Nne Asubuhi

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, iliyokuwa imepangwa kuanza kusikilizwa saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mpaka sasa saa nne bado haijaanza.

Wakati huu, Lissu pamoja na jaji hawajaingia ndani ya ukumbi wa mahakama, huku wananchi na wanahabari wakiendelea kusubiri.

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga

"Upande wa Jamhuri umeshapeleka taarifa Mahakama Kuu, kwa maana ya kufaili taarifa, kwa mujibu wa kifungu cha 262(6), na taarifa hiyo imepokelewa na kusajiliwa kwa namba Criminal Session 19605/2025 ambayo ni shauri la Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu."

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Antiphas Tundu Lissu.

"Mheshimiwa naomba maelekezo ya Mahakama yako, taarifa iliyopelekwa Mahakama Kuu kama imeshaletwa kwenye Mahakama hii, maana yake ikishapelekwa Mahakama Kuu inatakiwa iletwe kwenye mahakama hii ni Msajili wa Mahakama Kuu....Mahakama yako mheshimiwa itupe maelekezo kama 'file' limekuja kutoka mahakama kuu tuendelee mimi niko tayari."

"Sasa ile hofu yangu ya Star Chamber Court, inatima sasa, tunaingizwa katika utaratibu ambao kesi zitafanyika gizani kesi ya uhaini ambayo adhabu yake ni kifo kwa maombi yao inatakiwa ifanyike gizani."

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, ametaka kesi ya Tundu Lissu isiendelee kuonyeshwa moja kwa moja kupitia Vyombo vya Habari.

"Mahakama Kuu, kwa busara zake na kutaka kuona kwamba hawa mashahidi raia hawapati vitisho vyovyote kabla na baada ya kutoa ushahidi, ikasema wakati wa usikilizaji wa kesi mahakamani hatakuwa na chapisho la nyaraka yoyote au ushahidi mwingine wowote utakaopelekea utambuzi wa mashahidi ambao ni raia, vinginevyo kuwe na ruhusa ya Mahakama Kuu."

"Mhe. Msingi wa kuyasema haya ni kwamba shauri hili linaendeshwa na kurushwa moja kwa moja dunia nzima, kwa maana tayari tukiyasoma kwa njia hii ya kurusha moja kwa moja itakuwa tumekinzana na maamuzi ya Mahakama Kuu ya kwamba tusi-publish nyaraka au ushahidi mwingine wowote ambao unapelekea utambuzi wa shahidi huyu."

"Ombi letu sisi pamoja na nia njema ya Mahakama ya kuonyesha moja kwa moja mwendo wa Shauri hili tunaiomba Mahakama yako tukufu iweze kufuata maagizo kwenye rulling hii na Mahakama Kuu kwa kuzuia publication ya ushahidi wa namna hii"


Kwa Mwenendo huu wa Uendeshaji wa Kesi katika Mahakama za hapa nchini, naona umefika wakati Sasa wa kila mTanzania mwenye nia njema na nchi hii, Mpenda HAKI na Demokrasia ya kweli, basi anawajibika individually kutoa mchango wake wa Hali na Mali, kufa au kupona ili kuitetea HAKI katika Nchi hii. Now, it becomes an individual duty to bring Justice Environment within this country.
Kwa Hali mbaya Sana ilipofikia, kwa Sasa, haivumiliki tena kuendelea kukaa kimya katika Nchi hii. Ni lazima Sasa wajitokeze Watu ambao watakuwa sadaka ili kurekebisha Hali ya Mambo.
Actions speak louder than words. Muda utaongea!
 
Kwa hiyo kama itakuja kufahamika hapo baadaye kuwa hakuna sheria ya kuruhusu live streaming ya kesi, basi mvunja sheria wa kwanza ni Mahakama yenyewe.
Mahakamaccm haifanyi kazi kwa mjibu wa sheria bali inafanya kazi kwa mjibu wa Amri haramu za kishetani toka kwa ibilisi wa ccm
 
Mahakamaccm haifanyi kazi kwa mjibu wa sheria bali inafanya kazi kwa mjibu wa Amri haramu za kishetani toka kwa ibilisi wa ccm
Nimekutana na hii comment kwenye live session ya Mahakama

1755078056838.png
 
Tunaomba mahakama imtendee Lissu haki kwa namna alivyokua anaongea asipohukumiwa kunyongwa itakua hawajamtendea haki, kitendo cha kutishia kukinukisha kilisababisha nipate hofu na niwe na mashaka na maisha yangu, mtu huyu akirudi uraiani itasababisha wananchi tusio na hatia tuishi bila amani
Hii watu wanaichukulia poa.
 
Lissu anaomba tarehe ya karibuni yupo tayari kwa committal.
 
Wee ni kilaza, weka hapa huyo ushahidi lissu akitetea ushoga/mashoga, na mie nikuwekee official statement za viongoz wakuu wa nchi juu ya masuala ya utetezi wa ushoga/Mashoga
Mtu akikukuta kule kwenye Uzi wa watu hawaandaliwi kabla ya tendo... anaweza sema huyu nae ni kama zimemruka😂

Kumbe n smart bhana!! Ila huku unashusha nondo haswaaa
Hongera kwa kutuchanganya watizamaji
 
Kwanini hakimu ameshindwa kutoa hizo orders leo? Maana amedai ni nyepesi.
 
Kuanzia utawala wa kikwete hili jambo walipinga vikali na tukatishiwa kutopewa misaada
Kikwete alizuia meli iliyokua na wanaharakat za upinde ikarudi huko huko kwao.
Msimamo wa serikali mpk leo umepinga huo upuuuzi 😆😆
Sikandikiii😁
Huna akili kabisaa, unakumbuka, wakati wa magu, sakata la makonda kuhusu ushoga/mashoga, wizara ya mambo ya nje, ilikuja na statement gani? Waziri akiwa balozi Mahiga?

Vipi Madame president aliyetangaza wazi kuwa wafanyane wakubwa kwa wakubwa, ila wasiwafate watoto? Au hukuwa umezaliwa?
 
Kwa Mwenendo huu wa Uendeshaji wa Kesi katika Mahakama za hapa nchini, naona umefika wakati Sasa wa kila mTanzania mwenye nia njema na nchi hii, Mpenda HAKI na Demokrasia ya kweli, basi anawajibika individually kutoa mchango wake wa Hali na Mali, kufa au kupona ili kuitetea HAKI katika Nchi hii. Now, it becomes an individual duty to bring Justice Environment within this country.
Kwa Hali mbaya Sana ilipofikia, kwa Sasa, haivumiliki tena kuendelea kukaa kimya katika Nchi hii. Ni lazima Sasa wajitokeze Watu ambao watakuwa sadaka ili kurekebisha Hali ya Mambo.
Actions speak louder than words. Muda utaongea!
Tiba sahihi ni kuwafungulia kesi mahakimu majaji wote waonevu wanyanyasaji kwenye mahakama ya uhalifu kule The Hague ili wapate fundisho, na pia njia ya pili ni kuwasomea visomo vikali zikiwemo Alibadiri nyingi, Dua kibao kali laana nyingi toka kwa wapenda haki
 
Back
Top Bottom