Shauri la Jinai Na. 8607/2025 Jamhuri vs Tundu Lissu - Mahakama ya Hakimu Mkazi DSM Kisutu
Kesi ya jinai inayomkabili mwanasiasa na mwanasheria maarufu Tundu Lissu imeendelea leo Agosti 13, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Wanafunzi wa mashtaka na wafuasi wa Lissu wamekusanyika nje ya mahakama huku hali ya ulinzi ikiwa imara.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga, anatarajiwa kutoa uamuzi wa hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili. Upande wa Lissu umeipinga mara kwa mara ombi la Jamhuri la kuahirisha shauri hilo bila kuchukua hatua ya kupeleka kesi Mahakama Kuu, jambo ambalo linaleta wasiwasi miongoni mwa wananchi waliokusanyika kufuatilia kesi hiyo.
Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, Agosti 4, 2025, ilikubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa zingine za mashahidi wa upande wa mashtaka, hatua iliyolenga kulinda usiri wa mashahidi na usalama wa mchakato wa kisheria.
Updates
Asubuhi saa 1:00, Wananchi wamefurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Taifa, Tundu Lissu.
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Joseph Osmund Mbilinyi akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mmoja kati ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akivutana na askari wa Jeshi la Polisi katika Mahakama ya Kisutu ambako kesi inayomkabili mwenyekiti wao, Tundu Lissu, inaendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 13, 2025 ambapo Mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.
Nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wananachi wakisubiri uamuzi wa shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.
Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu haijaanza hadi sasa Saa Nne Asubuhi
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, iliyokuwa imepangwa kuanza kusikilizwa saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mpaka sasa saa nne bado haijaanza.
Wakati huu, Lissu pamoja na jaji hawajaingia ndani ya ukumbi wa mahakama, huku wananchi na wanahabari wakiendelea kusubiri.
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga
"Upande wa Jamhuri umeshapeleka taarifa Mahakama Kuu, kwa maana ya kufaili taarifa, kwa mujibu wa kifungu cha 262(6), na taarifa hiyo imepokelewa na kusajiliwa kwa namba Criminal Session 19605/2025 ambayo ni shauri la Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu."
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Antiphas Tundu Lissu.
"Mheshimiwa naomba maelekezo ya Mahakama yako, taarifa iliyopelekwa Mahakama Kuu kama imeshaletwa kwenye Mahakama hii, maana yake ikishapelekwa Mahakama Kuu inatakiwa iletwe kwenye mahakama hii ni Msajili wa Mahakama Kuu....Mahakama yako mheshimiwa itupe maelekezo kama 'file' limekuja kutoka mahakama kuu tuendelee mimi niko tayari."
"Sasa ile hofu yangu ya Star Chamber Court, inatima sasa, tunaingizwa katika utaratibu ambao kesi zitafanyika gizani kesi ya uhaini ambayo adhabu yake ni kifo kwa maombi yao inatakiwa ifanyike gizani."
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, ametaka kesi ya Tundu Lissu isiendelee kuonyeshwa moja kwa moja kupitia Vyombo vya Habari.
"Mahakama Kuu, kwa busara zake na kutaka kuona kwamba hawa mashahidi raia hawapati vitisho vyovyote kabla na baada ya kutoa ushahidi, ikasema wakati wa usikilizaji wa kesi mahakamani hatakuwa na chapisho la nyaraka yoyote au ushahidi mwingine wowote utakaopelekea utambuzi wa mashahidi ambao ni raia, vinginevyo kuwe na ruhusa ya Mahakama Kuu."
"Mhe. Msingi wa kuyasema haya ni kwamba shauri hili linaendeshwa na kurushwa moja kwa moja dunia nzima, kwa maana tayari tukiyasoma kwa njia hii ya kurusha moja kwa moja itakuwa tumekinzana na maamuzi ya Mahakama Kuu ya kwamba tusi-publish nyaraka au ushahidi mwingine wowote ambao unapelekea utambuzi wa shahidi huyu."
"Ombi letu sisi pamoja na nia njema ya Mahakama ya kuonyesha moja kwa moja mwendo wa Shauri hili tunaiomba Mahakama yako tukufu iweze kufuata maagizo kwenye rulling hii na Mahakama Kuu kwa kuzuia publication ya ushahidi wa namna hii"