Najazia, mimi ni mkristo, ninayoshuhudia makanisani siyo yale tuliyofundishwa kwenye maandiko, ninachokiona sasa ni bora mtu ujifungie kwenye chumba chenye utulivu na kumuomba Mungu wako, kisha ukawasaidie masikini, wajane, wagonjwa na yatima, Mungu wa mbinguni atakupa thawabu kuliko kwenda kushiriki biashara haramu ya kupora fedha za watu kwa kisingizio cha sadaka
- Kuna vitu viwili vinaitwa ubatizo na kipaimara, mawili haya yamekuwa biashara hivi sasa huko makanisani, Yesu kristo alibatiza bureeee!!! Lakini hivi sasa unajazishwa form kwaajili ya ubatizo au kipaimara, hizo fomu zinawekewa viwango vya pesa ya kulipa bila kujali ni mtu wa kipato cha chini au cha juu, usipoweza kulipa basi mtoto habatizwi na kijana hapewi kipaimara.
- Kwenye mazishi, kunatangazwa sadaka, mwisho wa siku sadaka ile inatajwa kuwa nauli ya kiongozi wa ibada ya mazishi, ni wizi mtupu.
Ukristo umekuwa biashara hivi sasa, wenye pesa ndiyo wanahudumiwa haraka zaidi kiroho kuliko masikini