Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama "Mkristo" maana yake ni kumfata Yesu Kristo basi hakuna shaka kuwa Muislam ndiye Mkristo wa kweli. Kama hujawa Muislam basi humfati Yesu Kristo.
Kiaje?
Uislam umenyooka sana mkuuUnauwakika ayo mambo huko kwa waislam hayapo?
Ila upo sahihi pia
SawaUislam umenyooka sana mkuu
Ulawiti,ushoga ni tabia ya mtu,hakuna maandiko yoyote kwenye vitabu vitakatifu vinafundishwa hayo mamboZinafuata watu na si maagizo ya Allah,mfano wasabato wamekuwa brainwashed na Ellen G White,waluteri na martin luther king,waanglikana na ushoga ni damdam,wakatoliki na ulawiti na kuhukumu wasio wanajumuia,Uislam umenyooka hawana konakona
Kutokuamini kwako hakumaanishi hayupo.Mungu hayupo achana na maandiko ya kitapeli ya quran ama biblia. Yale maandishi hayawezi kua yaliandikwa na anaeitwa mungu, labda kama aliandika akiwa amelewa.
Lakini still aijazuia hizo fitinaMoja ya vitu ambavyo uislamu unataka vifanyike kwa haraka wakati ukifika ni ndoa na kuzika. Sababu kubwa ni kuepusha fitna ya dunia na maaswi
Tungehamia uislam Kama tungegundua kwamba viongozi wa kidini wanayafanya haya mambo haya kwa miongozo wa bible direct, lakini kwakuwa tukisoma bible tunaona kabisa wanakosea wao na siyo bible. Bible is a perfect book Ila wanaotutafsiria wanatupotosha tu.Mkuu hamia unapoona nafuu. Am proudly Christian yaani kila tunachokifanya naona fahari mno mno mnooooo.
Nimecheka sana aiseh!!!mkuu umeua AISEH!!Mungu hayupo achana na maandiko ya kitapeli ya quran ama biblia. Yale maandishi hayawezi kua yaliandikwa na anaeitwa mungu, labda kama aliandika akiwa amelewa.
Wewe pia kuamini kwako hakufanyi awepo. Hilo la kwanza.Kutokuamini kwako hakumaanishi hayupo.
Hapo ni SAwa na kutaka ushahidi wa uwepo wa mawimbi ya sauti.kwani uoni radio,tv,simu.Wewe pia kuamini kwako hakufanyi awepo. Hilo la kwanza.
Jambo la pili, hakuna ushahidi kwamba Mungu ama shetani wapo, huo ni uongo wa wazi.
Achana na hizo hadithi za kitaahira. Mungu hayupo.Hapo ni SAwa na kutaka ushahidi wa uwepo wa mawimbi ya sauti.kwani uoni radio,tv,simu.
Ushahidi wa Mungu na Shetani.
Nyumba za ibada uzioni? Mpangilio wa uumbaji wa duniani ujauona?
Biblia na Quran ujaviona?
Kwenye ishu za ndoa, uislamu uko vizuri sana, hongera sana uislamu.Nikiri wazi Mimi ni mkristo kidanki ndaki , ni mafungu machache ya kwenye biblia yanaweza nipiga chenga ...
Dini zote mbili za kikristo na kiislamu zilitokea eneo moja , mashariki ya Kati , kile ambacho Biblia inasema na kile ambacho Qur'an inasema ni copyright for more than 80% , waislamu wamekuwa waaminifu kuendana na dini Yao angalau Kwa 75% Ila Kwa wakristo kumekuwa na kata funua nyingi , hasa Kwa viongozi wa dini , utitiri wa madhehebu , na taasisi za kiupigaji japo Biblia haihalalishi kile wanachokifanya...ni madhehebu machache yanayoweza kuifuata biblia hata Kwa 50%
Kuna mambo mawili kwenye dini ya kikristo ni wrong copy, au yamechepushwa kimakusudi na genge la watu fulani , na karbia madhehebu yote ya kikristo yanaona huo ndo mfumo sahihi , hata hvyo kiukweli hata Biblia yenyewe haikubaliani nayo...!!!
Jambo la Kwanza ni mfumo wa Sherehe za harusi na Jambo la pili ni mfumo au taratibu za kuwahifadhi wapendwa wetu wanaopumzika (wafu) ....!!
Sina uzoefu na dini ya kiisilamu , hata hvyo kuishi kwangu Tanga Kwa mda fulan kulinipa uzoefu fulani, hvyo kama nitakosea au kwenda kinyume basi nakubali kusahihishwa ....!!
Ndoa za kiislamu Swala la Harusi sio first priority, wapo wachache wanaoweza kulipigia chapuo, hata hvyo waislamu wamekuwa waaminifu Kwa hili , michango ya Harusi isiyo na uhalisia na yenye kuumizana na kutupiana lawama Kwa waislamu hii ni asilimia kidog Sana ,ndoa za mikeka Kwa ubani wa 300 nimezishuhudia several times na familia zao zimekuwa zikienda viral 😊
Cha msingi kuwe na kipunga na ngoma mbili tatu basi lyfe linaenda.
Kwa wakristo ndoa imegeuzwa kuwa mtaji , Kwa asilimia kubwa ndoa bila Harusi kubwa na vinono hyo ni kama haitambuliki , kumekuwa na masharti kibao kwenye kuchumbia , mlolongo mrefu usiokuwa na maana , tozo nyingi Kwa ajili ya mchungaji anayefungisha ndoa , na Gharama zikiongezeka mara dufu , michango ya Harusi , unywaji wa pombe uliokithiri na anasa za kila namna ukumbini ndo fashion now days , sherehe zikiisha usku wa manane na kutengeneza kichaka cha uzinzi na uasherati ....Nina uhakika Mungu hakubaliani na huu ujinga, thus why ndoa nyingi za kikristo zimekuwa zikiishia kwenye maumivu yasiyoelezeka....!!!
Vijana wengi wa kikristo wameishia kuoa kinyemela ili kuepukana na hii adha , wengi wanaishi gheto na mabinti na maisha yanaenda hata hvyo viongozi wa dini huwachukulia kama waliolaaniwa .
jambo la pili ni swala la kuwahifadhi ndugu wanaofariki, hapa pia ni vurugu tupu , Kwa waislamu msiba ni swala zito , na maiti inatakiwa ihifadhiwe kaburini haraka iwezekanavyo , nilishuhudia kwenye msiba wa mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Nyerere kama sikosei , alifariki sa 12 jioni , kesho akazikwa mapema iwezekanavyo, Baba mzazi wa GSM alifariki usiku na Kesho yake akazikwa ..na watu wengine maarufu imekuwa ndo utaratibu...!!
Biblia pia inakubaliana na utaratibu huo , mara nyingi wafalme wa Isarel walipokuwa wanafariki Biblia ilisema sentensi moja tuu , akafariki akazikwa kwenye makaburi ya kifalme full stop , badae yanafanyika maombolezo mara nyingi ilikuwa sku 40...
Kifo cha kuhani mkuu Haruni na nabii Mussa kule jangwani pamoja naa mazishi yao kinaonyesha namna Mungu asivyokubaliana na kuchelewesha mazishi , Kifo cha Miriamu aliyekuwa mtu mkubwa Sana Kando ya Musa na Haruni biblia inatoa sentesi moja tuu , Miriamu akafa huko akazikwa huko , kuchelewesha mazishi kunaongeza machungu Kwa wanandugu na pia kushawishi Ibada za kishetani na matambiko , thus why Musa na Haruni walizikwa haraka iwezekanavyo tena chini ya Mwenyezi Mungu mwenyewe , na makaburi Yao yalifichwa ili kuepusha akili mbovu za binadamu kufanya yasiyompendeza Mungu....
Kwa wakristo wa sa hv Misiba ni mzigo mzito , maiti itazungushwa weee, kuanzia hospitali , kanisani , mara ukumbini , atasubiriwa sijui ndugu gani yupo ulaya , maiti atasafrishwa , kule akifikishwa na penyewe inaanzishwa Ibada fupi sjui , mpak anazikwa , basi ashasababisha taabu kuu , watu wamelia mpak machozi yamekauka , utapeli wa madaftari ya michango rambi rambi ushafanyika vya kutosha huku familia ikiachiwa mzigo mzito wa madeni ya Gharama za mazishi ..!!!
Watu bilioni 6 duniani sio wote wajinga waamini kisichokuwepoAchana na hizo hadithi za kitaahira. Mungu hayupo.