bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Uamuzi wake ni sahihi Bora uvunje uchumba na sio ndoa.
Asili ina nguvu,we kurupuka tu
Asili ina nguvu,we kurupuka tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona nyie mnatuacha kisa tumefulia kwani kukosa pesa ni jambo la kudumuHuna mapenzi ya dhati wewe.
Huwezi kumuacha mtu kisa ulemavu kwani yeye anapenda,.?
Wabongo inabidi tubadirike na fikra mgando za sampuli hii.
Haya mambo hutokea ghafla sana bila kupangaBado ana utoto huyo
Anajua anapoenda kuoa sasa
Au yeye anaijua kesho yake
Hajafanya jambo sahihi, siku zote ulemavu unaweza kusababishwa na changamoto zingine za kiafya hasa wakati wa kujifunguaBinafsi mimi naona kijana kakosea, hakuwa sahihi, mkasa huu hapa nawapeni.
Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22, wote ni wasomi binti kamaliza degree mwaka jana.
Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.
Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi
Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.
Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.
kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.
Kijana akamkimbia mwenzake na kumuweka wazi kwamba anampenda lakini anachukua tahadhari hawezi kurisk kumuoa sababu ndoa bila watoto ni ngumu na anahofia alichokigundua kwenye familia anayotokea huyo binti, aloimwambia kwamba mtu yeyote anaweza kupata mtoto mlemavu lakini anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi wakipata mtoto kwa kuhofia binti kabeba genes / genetics zinazoweza kuleta mtoto mwenye ulemavu (alimficha sababu ya ziada kwamba anahofia kuna mambo ya mila / ushirikina yanayoweza kurithika kwa watoto),
Alimwambia binti wanaweza kuwa na mahusiano mengine ila si kwenye kupata watoto, Binti hakumwelewa kabisa ikawa ndio mwisho hapo.
Je, ni sawa ?
Hakika. Na inapokua haipatikan hali huwa hailezek vile una feel.Pole sana mkuu,
Hapa changamoto kubwa huwa ni pesa, Yaani pesa isipokuwepo mzazi anaweza fanya maamuzi magumu sana pesa ipatikane
KabisaHaya mambo hutokea ghafla sana bila kupanga
Asije jikuta yeye katika familia yao ndio anakuwa wa kwanza kupata ulemavu.
Kumcheka au kumdharau mlemavu ni jambo baya sana na malipo yake huwa ni ya haraka sana.
Ukiwa mzima shukuru.
Ila kuna familia nyingine jamani sikieni tu. Niliwahi kuwa karibu na familia moja ya mke na mumuwe ambao ni wasomi wazuri tu na wana kazi nzuri. Shida ilikuwa kwenye watoto. Walikuwa na watoto wanne na wote walikuwa na maumbo kama mazombi hivi. Yaani wakati wa kuzaliwa, wanazaliwa vizuri kabisa, wakiwa watoto wazuri mno. Na wanakua vizuri kabisa kuanzia kuzaliwa mpaka miaka minne. Wakifikisha miaka minne wanaanza kupata mabadiliko. Maumbo yanaanza kubadilika, miguu inajipinda na maumbo yao yanageuka wanakuwa kama ndondocha au mazombi. Pia akili nazo zinabadilika wanakuwa kama mazuzu. Yaani walikuwa wanatia huruma kweli kweli watoto wazuri wanne wote wakageuka kuwa mazombi. Hakuna maombi ambayo hakupitia na hospital pia. Hospital alimbiwa wana kasoro kwenye gene zao na jambo walilorithi. Nikajakusikia baadae walijafariki wote.Pole mkuu, mama yake anaongea na kusikia vizuri?
Hivi inatokeaje mtu akatae mtoto wake? Ninavyopenda watoto mimi... da.Kabisa
Niliwahi simuliwa story
Jamaa alimkataa mtoto albino
Matokeo yake yeye akaanza kupata ule ugonjwa vitiligo ukubwani ukasambaa mwili mzima
🤣🤣Jamaa yangu aliwahi ku-date na demu mmoja ana mguu mmoja mfupi na hakujua kwa kipindi kirefu tu. Alikuwa anajua kuuficha kweli kweli, ila baadae akamgundua.Huna mapenzi ya dhati wewe.
Huwezi kumuacha mtu kisa ulemavu kwani yeye anapenda,.?
Wabongo inabidi tubadirike na fikra mgando za sampuli hii.
Umenikumbusha baba yangu alikua anasisitiza ukipata mchumba umwambie mapema achunguze ukoo wake maana kuna magonjwa ya kurithi, tabia za kuhama vizazi, laana za ukoo na mambo muhimu kuchunguza kabla ya ndoa.Kosa alilolifanya Ni kumwambia( kuropoka) kwa Nini anaachana naye, angetafuta tu njia ya kuachana naye tu kiaina kwa ustaarabu bila binti kujua, Hata wazee wa zamani walikuwa wanafuatilia familia ya mtu mnaetaka Kuoana nae, Kama familia Ina changamoto walibadili maamuzi na ilisaidia Sana kuepusha changamoto mbalimbali.
Jamani, hadi huruma.Ila kuna familia nyingine jamani sikieni tu. Niliwahi kuwa karibu na familia moja ya mke na mumuwe ambao ni wasomi wazuri tu na wana kazi nzuri. Shida ilikuwa kwenye watoto. Walikuwa na watoto wanne na wote walikuwa na maumbo kama mazombi hivi. Yaani wakati wa kuzaliwa, wanazaliwa vizuri kabisa, wakiwa watoto wazuri mno. Na wanakua vizuri kabisa kuanzia kuzaliwa mpaka miaka minne. Wakifikisha miaka minne wanaanza kupata mabadiliko. Maumbo yanaanza kubadilika, miguu inajipinda na maumbo yao yanageuka wanakuwa kama ndondocha au mazombi. Pia akili nazo zinabadilika wanakuwa kama mazuzu. Yaani walikuwa wanatia huruma kweli kweli watoto wazuri wanne wote wakageuka kuwa mazombi. Hakuna maombi ambayo hakupitia na hospital pia. Hospital alimbiwa wana kasoro kwenye gene zao na jambo walilorithi. Nikajakusikia baadae walijafariki wote.
Mmmmh jitahidi uwe na akiba ya manenoUamuzi wake ni sahihi Bora uvunje uchumba na sio ndoa.
Asili ina nguvu,we kurupuka tu
Kuna watu Wana laana mnoHivi inatokeaje mtu akatae mtoto wake? Ninavyopenda watoto mimi... da.
Mkuu ww unaonekana unaelewa sana haya mambo ya magonjwa ya kurithi..Nami naomba niulize hapa. Hivi ukoma(leprosy) nao pia huwa ni ugonjwa wa kurithi, genetically?Hajafanya jambo sahihi, siku zote ulemavu unaweza kusababishwa na changamoto zingine za kiafya hasa wakati wa kujifungua
Kuna baadhi ya huduma ukichelewa kuzipata kipindi cha ujauzito au wakati mzazi anajifungua inaweza kupelekea mtoto kupata athari katika afya yake au hata kupoteza maisha
Hivyo hii sio kigezo sana, ila kwenye imani ya kishirikina unapaswa uwe na imani na uamini, hupaswi kufunga ndoa na mtu asieamini na mshirikishe Mungu naye atavunja hizo imani za kishirikina
Mwisho, nimeshuhudia baadhi ya walemavu wa kuzaliwa wakipata watoto wazima wa afya na nimeona pia watu ambao hata familia zao hata ukoo hamna mlemavu hata mmoja pande zote mbili, lakini isivyo bahati wakazaa mlemavu na kuishia kukisia na kupiga ramli inawezekana kwa mababu na mababu walikuwepo walemavu kitu ambacho ni senseless
lolote linaweza kutokea na Mungu ndio muweza wa yote, mtangulize daima katika kila kitu.
Shukran mkuu ndio kazi ya MuumbaPoleee