عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لأَرْبَعٍ: لِمَالِهَا وَلِحَسَبِهَا وَجَمَالِهَا وَلِدِينِهَا. فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاكَ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mwanamke huolewa kwa sababu nne; Kwa mali yake, nasaba yake [ukoo], uzuri wake na Dini yake. Tafuta mwenye Dini ubakie salama)).[Al-Bukhaariy na Muslim] (yaani usiharibikiwe katika maisha yako).
Chagua Mwenye Dini kisha mengine utayatazama. Ukipata mwenye Dini kisha ana uzuri unaoupenda sawa na ni muhimu, ana dini kisha ana nasaba nzuri sawa, ana dini kisha ni mkwasi sawa. Ana vyote vinne ni kheri juu ya kheri. Lakini Dini ndio kwanza kisha mengine. Chagua/tafuta mwenye Dini. Tuwe makini kwa hili ndugu yangu. Allah atusaidie.