Kila nikiwaza haya majanga nakosa hamu ya kupata mtoto

Ndugu wee umeongea cha maana kidogo, kwamba Kuna familia ni vizazi mpaka vizazi kwao ni umasikini tu au ni maradhi tuu, hii maana yake ni hivi alivyoishi Babu ndio kaishi baba na ndio ninavyoishi mimi na hata na kizazi changu pia,. Sasa kwa kuliona hili ndio maana nawazaga bora mimi niwe wa mwisho kwenye hiki kizazi, yaani kisiendelee tena ndio njia nzuri,. Au unasemaje mkuu
 
Eeee yaani Sio HAKI, machozi ya mtoto juu ya janga nitakalo muachia yatanitesa na kunisakama mpaka mwisho wa maisha tangy,.
Nakuelewa sana mkuu, sisi tunawaleta duniani kwa vile Mungu atatoa riziki zake Ila hatuna maandalizi yoyote kwa hao viumbe wanaokuja.

Sio sawa kuleta watoto duniani wapate shida, waishi dhiki na umasikini, magonjwa nk Ila ndio hivyo tena sisi tunafyatua tu.
 
Kufyatua watoto kisa mungu anatoa rizki ni ujinga Kama miujinga mingine mkuu, kwenye hii mada wewe ni mtu wa tatu tu tokea nimelianzisha ambaye kajibu point ila Kuna msomi mmoja nilimsikia akisema "wajinga huwa wengi kuliko waelevu"
 
Wakuu Kuna vingi vya kuviangalia kwenye vizazi vyenu ukiachana na riziki ambayo anaitoa
 

hizo sababu ulizotoa ni ndogo. mimi nahofia kupata watoto sababu matibabu bei juu elimu shida utamsomesha mtoto miaka 14 mwishowe anaambiwa akajiajiri mbali ni hiyo nahofia watoto kukosa maadili wataingia kwenye ubongo fleva au kushabikia mipira asubuhi mpaka jioni maisha yanapanda hapana bora ningekuwa nchi nyingine ningekuwa na tamaa ya kupata mtoto
 
Ukifika muda utapata tu bila hayo mawazo kuwa kikwazo
 
Sasa hapo ndg,tafuta chanzo kwa babu hadi mshua utagundua jambo.mmi niliongea kwakuwa niliona familia moja ilifungwa babu yao alioa wanawake wawili sasa familia hizi mbili zikawa na mvutano bibi MKUBWA akafunga watto wa bibi MDOGO wasitoboe maisha ila wa bibi MKUBWA ndo wawe na maish kwa hiyo hiyo kitu imetembea mda mrefu sna baada ya kufatilia wakapata taarifa kama hizo.hapo sasa ni wajukuu ndo wanafatilia sasa ila walipo jua wakawa wazito kuchukuwa hatua,sasa mmoja ndo akajitoa ufahamu akachukuwa hatua akaombewa ndo sasa wanaona mwanga kwahiyo ktk maisha kuna mambo mengi.
 
Nafikiri ni maamuzi biinafsi, lazima tuyaheshimu
 
kwa kutumia neno mungu basi hatupaswi kujadili chochote, mpaka tunajadili hi inamaana kwamba tunahitaji kutumia akili na mawazo yetu sio MUNGU Tena, maana ukuanza kuingiza mungu kwenye maada yangu utaonekana haupo timamu,.
Mungu lazima umuhusishe kwasababu akili ya binadamu ina ukomo wa kufikiri na binadamu ana ukomo wa kufanikisha atakalo
 
kweli mkuu haya yako ni makubwa pia,.
hapo pa matibabu bei juu nishida na tatizo maradhi mengi,.
 
Ukifika muda utapata tu bila hayo mawazo kuwa kikwazo
kitu kama hiko kwangu hakipo, siwezi zaa bila ya kujua kizazi changu kitakuja kuishi vipi? na pia mi naamini hakuna kuzaa kwa bahati mbaya,.
 
Ni ushauri mzuri kiroho,. sawa!
 
Nafikiri ni maamuzi biinafsi, lazima tuyaheshimu
Sana,. lazima maamuzi yangu ya maisha yangu na kizazi changu yaheshimiwe,.
watoto wangu watabikia hukohuko mbinguni ntaenda kuonana nao siku nikifa,.
 
Mungu lazima umuhusishe kwasababu akili ya binadamu ina ukomo wa kufikiri na binadamu ana ukomo wa kufanikisha atakalo
Sawa!. sikupingi kupitia imani yako ya mungu yu muheza wa kila jambo,.
 
Sawa Mimi nimezaliwa kwa zali la mentali Sasa na Mimi ndio nizae ki zali la mentali kweli nitakuwa nipo sahihi? Sawa Mimi nimekuwa kimapenzi ya mungu kwahiyo na Mimi ndio nizae nikisubiria mapenzi ya mungu kweli ntakuwa timamu?
One man down!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…