Kila nikiwaza haya majanga nakosa hamu ya kupata mtoto

Mttupplli:nakuelewa na hii uwatokea watu ambao wametoka familia ngumu kwa maana ya hali duni Ki uchumi na maradhi hadi chakula.unaweza ukamkuta kijana yuko 35-40+ yrs amepambana kuokoa familia yake angalau wavuke ktk daraja hilo la ufukara lakini hadi anajikuta umri huo anaanza kuwaza mambo yanayo umiza akili kama usemavyo.Alafu jamii inayomzunguka haijui unapambana kwa kiwango gani ili nawewe uwe au muwe kama familia zingine zenye *3 kutwa.sasa jamii inaanza kukuhukumu haujao hadi sasa umri unakwenda,hapo unaingiwa na hofu unaanza kujiuliza hivi nilikuwa na ndoto watto wangu wasisome mazingira kama uliyopitia,sasa utaishi vipi?na watto ktk malezi yapi na huku hauna pesa.sasa ndg nikusaidie kitu kimoja nahiki kitu huwa tunajisahau au Maarifa ndo huwa hatuna.ktk familia zetu Mara kwa mara kulikuwa na matambiko sasa ukifatilia utakuja kugundua mmefungana kizazi kwa kizazi hadi unasikia ukoo flani huwa ni masikini mambo yaliyotendeka huko nyuma hauyajui na ukifatilia utasikia hivi Mara vile.tafuta sehemu moja ambayo utaamini kuwa yule ni mtumishi wa MUNGU kweli nenda kakae naye msimulie kisha tubu na kuwaombea na ndg zako wengine wafunguliwe ktk vitanzi hivyo hakika ipo siku utakuja kushukur JF.MUNGU akutangilie chukuwa hatua sasa hakika ata kama unamaradhi yanayo shindikana kwa wataaram kwa MUNGU nijambo dogo sna.na mwisho wasiku utakuwa na familia yako na maisha yakuwa historia.
Ndugu wee umeongea cha maana kidogo, kwamba Kuna familia ni vizazi mpaka vizazi kwao ni umasikini tu au ni maradhi tuu, hii maana yake ni hivi alivyoishi Babu ndio kaishi baba na ndio ninavyoishi mimi na hata na kizazi changu pia,. Sasa kwa kuliona hili ndio maana nawazaga bora mimi niwe wa mwisho kwenye hiki kizazi, yaani kisiendelee tena ndio njia nzuri,. Au unasemaje mkuu
 
Eeee yaani Sio HAKI, machozi ya mtoto juu ya janga nitakalo muachia yatanitesa na kunisakama mpaka mwisho wa maisha tangy,.
Nakuelewa sana mkuu, sisi tunawaleta duniani kwa vile Mungu atatoa riziki zake Ila hatuna maandalizi yoyote kwa hao viumbe wanaokuja.

Sio sawa kuleta watoto duniani wapate shida, waishi dhiki na umasikini, magonjwa nk Ila ndio hivyo tena sisi tunafyatua tu.
 
Kufyatua watoto kisa mungu anatoa rizki ni ujinga Kama miujinga mingine mkuu, kwenye hii mada wewe ni mtu wa tatu tu tokea nimelianzisha ambaye kajibu point ila Kuna msomi mmoja nilimsikia akisema "wajinga huwa wengi kuliko waelevu"
 
Wakuu Kuna vingi vya kuviangalia kwenye vizazi vyenu ukiachana na riziki ambayo anaitoa
 
Natamani sana kuwa na watoto, ila nina mambo yanayonikosesa furaha kila nikiwaza juu ya kuwa na watoto,.
Miongoni mwa mambo hayo nina makubwa mawili nayo ni;-

1. Umasikini, Umasikini ni janga kubwa kwa upande wangu, huwa nakosa amani pale ninapoiona kesho ya watoto wangu kwenye swala umaskini, sina njia mbadala ya kuwa kwamua watoto wangu kwenye hili janga.

2. MARADHI, Hili ni kubwa pia japo halilingani na la kwanza, mfano kwenye hili gonjwa la UKIMWI kila nikiiwaza kesho ya wanangu katika hili janga linanikatisha tamaa na kujiona mwenye hatia endapo ntawaacha watoto waje duniani na niwaingize kwenye hili janga.

3. Upofu, Maradhi ya akili kama uchizi, utahaira nk. Pia kuna maradhi ya moyo. Na hata kifafa. Huwa nakosa furaha kila nikiifikilia kesho ya kizazi changu na naona ni bora niishi mwenyewe na hata nikifa basi nife bila ya kuacha KIZAZI kisicho na furaha.

Nimeikopy facebook

hizo sababu ulizotoa ni ndogo. mimi nahofia kupata watoto sababu matibabu bei juu elimu shida utamsomesha mtoto miaka 14 mwishowe anaambiwa akajiajiri mbali ni hiyo nahofia watoto kukosa maadili wataingia kwenye ubongo fleva au kushabikia mipira asubuhi mpaka jioni maisha yanapanda hapana bora ningekuwa nchi nyingine ningekuwa na tamaa ya kupata mtoto
 
Ukifika muda utapata tu bila hayo mawazo kuwa kikwazo
 
Ndugu wee umeongea cha maana kidogo, kwamba Kuna familia ni vizazi mpaka vizazi kwao ni umasikini tu au ni maradhi tuu, hii maana yake ni hivi alivyoishi Babu ndio kaishi baba na ndio ninavyoishi mimi na hata na kizazi changu pia,. Sasa kwa kuliona hili ndio maana nawazaga bora mimi niwe wa mwisho kwenye hiki kizazi, yaani kisiendelee tena ndio njia nzuri,. Au unasemaje mkuu
Sasa hapo ndg,tafuta chanzo kwa babu hadi mshua utagundua jambo.mmi niliongea kwakuwa niliona familia moja ilifungwa babu yao alioa wanawake wawili sasa familia hizi mbili zikawa na mvutano bibi MKUBWA akafunga watto wa bibi MDOGO wasitoboe maisha ila wa bibi MKUBWA ndo wawe na maish kwa hiyo hiyo kitu imetembea mda mrefu sna baada ya kufatilia wakapata taarifa kama hizo.hapo sasa ni wajukuu ndo wanafatilia sasa ila walipo jua wakawa wazito kuchukuwa hatua,sasa mmoja ndo akajitoa ufahamu akachukuwa hatua akaombewa ndo sasa wanaona mwanga kwahiyo ktk maisha kuna mambo mengi.
 
Natamani sana kuwa na watoto, ila nina mambo yanayonikosesa furaha kila nikiwaza juu ya kuwa na watoto,.
Miongoni mwa mambo hayo nina makubwa mawili nayo ni;-

1. Umasikini, Umasikini ni janga kubwa kwa upande wangu, huwa nakosa amani pale ninapoiona kesho ya watoto wangu kwenye swala umaskini, sina njia mbadala ya kuwa kwamua watoto wangu kwenye hili janga.

2. MARADHI, Hili ni kubwa pia japo halilingani na la kwanza, mfano kwenye hili gonjwa la UKIMWI kila nikiiwaza kesho ya wanangu katika hili janga linanikatisha tamaa na kujiona mwenye hatia endapo ntawaacha watoto waje duniani na niwaingize kwenye hili janga.

3. Upofu, Maradhi ya akili kama uchizi, utahaira nk. Pia kuna maradhi ya moyo. Na hata kifafa. Huwa nakosa furaha kila nikiifikilia kesho ya kizazi changu na naona ni bora niishi mwenyewe na hata nikifa basi nife bila ya kuacha KIZAZI kisicho na furaha.

Nimeikopy facebook

Nafikiri ni maamuzi biinafsi, lazima tuyaheshimu
 
kwa kutumia neno mungu basi hatupaswi kujadili chochote, mpaka tunajadili hi inamaana kwamba tunahitaji kutumia akili na mawazo yetu sio MUNGU Tena, maana ukuanza kuingiza mungu kwenye maada yangu utaonekana haupo timamu,.
Mungu lazima umuhusishe kwasababu akili ya binadamu ina ukomo wa kufikiri na binadamu ana ukomo wa kufanikisha atakalo
 
hizo sababu ulizotoa ni ndogo. mimi nahofia kupata watoto sababu matibabu bei juu elimu shida utamsomesha mtoto miaka 14 mwishowe anaambiwa akajiajiri mbali ni hiyo nahofia watoto kukosa maadili wataingia kwenye ubongo fleva au kushabikia mipira asubuhi mpaka jioni maisha yanapanda hapana bora ningekuwa nchi nyingine ningekuwa na tamaa ya kupata mtoto
kweli mkuu haya yako ni makubwa pia,.
hapo pa matibabu bei juu nishida na tatizo maradhi mengi,.
 
Ukifika muda utapata tu bila hayo mawazo kuwa kikwazo
kitu kama hiko kwangu hakipo, siwezi zaa bila ya kujua kizazi changu kitakuja kuishi vipi? na pia mi naamini hakuna kuzaa kwa bahati mbaya,.
 
Sasa hapo ndg,tafuta chanzo kwa babu hadi mshua utagundua jambo.mmi niliongea kwakuwa niliona familia moja ilifungwa babu yao alioa wanawake wawili sasa familia hizi mbili zikawa na mvutano bibi MKUBWA akafunga watto wa bibi MDOGO wasitoboe maisha ila wa bibi MKUBWA ndo wawe na maish kwa hiyo hiyo kitu imetembea mda mrefu sna baada ya kufatilia wakapata taarifa kama hizo.hapo sasa ni wajukuu ndo wanafatilia sasa ila walipo jua wakawa wazito kuchukuwa hatua,sasa mmoja ndo akajitoa ufahamu akachukuwa hatua akaombewa ndo sasa wanaona mwanga kwahiyo ktk maisha kuna mambo mengi.
Ni ushauri mzuri kiroho,. sawa!
 
Nafikiri ni maamuzi biinafsi, lazima tuyaheshimu
Sana,. lazima maamuzi yangu ya maisha yangu na kizazi changu yaheshimiwe,.
watoto wangu watabikia hukohuko mbinguni ntaenda kuonana nao siku nikifa,.
 
Sawa Mimi nimezaliwa kwa zali la mentali Sasa na Mimi ndio nizae ki zali la mentali kweli nitakuwa nipo sahihi? Sawa Mimi nimekuwa kimapenzi ya mungu kwahiyo na Mimi ndio nizae nikisubiria mapenzi ya mungu kweli ntakuwa timamu?
One man down!!
 
Back
Top Bottom