Ya ni kweli kwa namna fulani, ila kwa namna nyingine ni unafiki mkubwa unaofanywa na baadhi ya hayo hayo mataifa makubwa kwa kuipatia Israel silaha nzito ambazo mataifa hayo yanajua fika kuwa ndio zinazotumika kuua hao raia.
Ilitakiwa wasitishe kuipa silaha Israel kama wanavyopinga Hamas kuwa nazo, hii ingesaidia kwa kiwango kikubwa kuokoa uhai wa hao raia, maana Israel isingekuwa na uwezo wa kuendelea na vita miezi mingine miwili mbele. Ingeondoa majeshi yake, ingepinga vitendo vya uvamizi katika ardhi za wapalestina huko west bank, ingepinga kukamata raia kuwatesa, kuwaua na wengine kuwafungulia kesi kila siku zisizokwisha. Ingeacha kuwakandamiza na kuruhusu haki zao za msingi kama shughuli za uvuvi, kufanya kazi kwa uhuru, kuwa na maji safi, umeme nk.
Raia wowote duniani huanzisha mashambulizi pale tu haki zao za msingi zinaponyang'anywa na kupewa watu wengine. Hivyo watu kama Hamas wamejikuta wanaingia mapambanoni baada ya haki zao za msingi kunyang'anywa na waisrael. Wanaona ni bora waingie mapambanoni na kama kufa wafe kuliko kuendelea kuvumilia ukandamizaji wa miaka na miaka.