Kinachoendelea huko Mashariki ya kati kinadhihirisha kuwa uongo wa wazungu unaelekea kufika mwisho

Kinachoendelea huko Mashariki ya kati kinadhihirisha kuwa uongo wa wazungu unaelekea kufika mwisho

Israhell nchi ya hovyo sana halaf wanatumia nguvu kuubwa sana kuhalalisha failure yao

Yaani wanakosa hoja kabisa wamechanganyikiwa kiasi kwamba wanaua mpaka watu wao na washirika wao

Israhell hata wakiona sehem kuna panya kakatiza watampigia simu rubani adondoshe ghorofa zima zima yaaani

Intelijensia na jeshi la israhell zakawaida sana sio kama tulivyokua tunahubiriwa na MSM

Kama wameshindwa kuwakomboa mateka wao siku 💯 kasoro kidogo sasa hapo jirani yao

Wakat walienda mpaka Entebe eti kuokoa watu wao maelf ya kilometers tena
Ni nani alikuwepo wakati wanaokoa watu wao Entebe?
Kama yupo atuwekee ushahidi jinsi walivyookoa watu wao, na sio kutuwekea movie iliyoigizwa na wazungu wenzao.
 
Ni nani alikuwepo wakati wanaokoa watu wao Entebe?
Kama yupo atuwekee ushahidi jinsi walivyookoa watu wao, na sio kutuwekea movie iliyoigizwa na wazungu wenzao.
Watakuja tu kutupa documentary hawana mpya

Wazungu walitufanya kua mazombi muda mwingi sana kwakweli

Ila uzuri ujinga wao umejulikanika kweupee eeee
 
YAn hata operation Entebe, kama wale mateka wangekua bongo under JWTZ, israel asingeokoa hata mmoja na tungewalamba vyuma mpaka wasijue pa kutokea 😂😂.
Ni vile tu jeshi la Idd Amin lilikua la kijinga jinga
 
Yaa ni kweli maelfu wanauwawa wakiwemo watoto wadogo ambao hawajui hata kuongea wala kutembea.

Fikiria nchi ambayo umedanganywa kuwa ina intelejensia kubwa, weledi na uwezo mkubwa wa kijeshi inaweza kutumia ndege zisizokuwa na rubani, vifaru na silaha zake nzito kuuwa watoto wachanga wasiojua hata kurusha jiwe?

Hii ni sawa na wewe uingie ulingoni kupigana na katoto ka miaka miwili, ukarushie ngumi, mateke na nguvu zako zote alafu uje ujitape kuwa wewe ni bingwa kwa kukapiga katoto hako. Wenye akili na nguvu za kweli nafikiri watakucheka sana.
IDF piga hadi ile midoli yao takbirr ziendelee kupotea hapo GAZA ikiwezekana hata huko ulaya muwatimue.
 
Ikiwa unamaanisha mtume Muhammad basi ukae ukijua ya kwamba,,,
Alikuwa na wake wanne,,
Watoto saba,,,
Kaongoza vita Zaidi ya moja,,
Alikuwa pia mfanyabiashara, yani kifupi alikuwa mwanaume wa shoka haswa tofauti na nyie Ambao kiongozi wenu kule Italy katoa dongo mgongwe pumbavu kabisa,,, sasa wewe sijui ushaenda kubariki kanisani ili ufilwhe vizuri,,
Kwa hiyo mudy alikuwa mfanyabiashara?huyu mo wa bongo kamzidi huyo mbakaji
 
Vifuasi vya magaidi vina hasira hivyo,ile oktoba 7 vilitarajia makubwa sana sheitwani bhana!
 
Au wewe ndio unajifariji. Kama ingekuwa ina huruma kama unavyofikiri, basi isingeuwa maelfu ya watoto wadogo wasiokuwa na hatia, pamoja na wanawake including raia ambao hawana hata visu vya kupambana na vifaru vya Israel.
Hao watoto wanatumiwa kama ngao na wahuni wa Makamasi!! Wanarusha makombora wanakimbilia kujificha kwa watoto na raia kwa ujumla, damu yao ipo juu ya magaidi, mlitaka IDF wasijibu!! Infact silaha zote za magaidi zipo maeneo ya raia!
 
Niaje waungwana?

Wazungu baada ya kuona wamefanikiwa kutawala sehemu kubwa ya dunia haswa haswa katika bara zima la Afrika, wakaona kuwa hata uongo wao pia watakaoleta kwa watawaliwa utaweza kuishi milele, bila kujua kwamba zama zinabadilika na akili za watawaliwa nazo pia zinabadilika.

1. Kwanza wazungu walitudanganya kuwa wanakuja kutukomboa kiuchumi na kiroho, kumbe nyuma ya pazia lengo lilikuwa ni kututawala, kumiliki ardhi yetu na kila kilichopo katika nchi zetu.

2. Pili walitudanganya kuwa binadamu wa kwanza au wa kale walikuwa ni manyani, lakini hapo hapo kupitia vitabu vitakatifu vya dini wakatuambia kuwa binadamu wa kwanza alikuwa ni binadam wa kawaida ambae jina lake ni Adam.

cha kushangaza katika vitabu vinavyoonesha kuwa binadamu wa kwanza walikuwa nyani, utakuta waliochorwa ni watu weusi, na vile vinavyoonesha kuwa binadam wa kwanza alikuwa Adam utakuta amechorwa mzungu, hivyo ni wazi kuwa binadam wote tulikuwa ni binadam wa kawaida kutoka kwa baba yetu Adam, hao nyani tulioambiwa ilikuwa ni uongo mahususi uliotengenezwa kwa malengo yao watawala (wazungu)

3. Tatu wanadanganya kuwa pale Mashariki ya kati nchi yenye nguvu zaidi za kijeshi ni Israel, lakini wengi tumeshuhudia kwamba Israel haina tofauti na Ukraine, kwamba kila inapotaka kupigana na adui yake, au hata kikundi cha vijana wasiozidi hata 20,000 kama vile Hamas lazima waombe msaada wa silaha kutoka Marekani, huku UK na EU nao wakiipa kwa njia ya kimya kimya ili kupambana na kakundi hako.

Bora hata Ukraine inapambana na taifa ambali ni la kwanza kwa ukubwa duniani, taifa ambalo Ukraine inaingia zaidi ya mara 10, lakini pia ni la pili kwa nguvu za kijeshi duniani, hivyo kutokana na udogo wake na pia utoauti wa nguvu za kijeshi, ina haki ya kuomba msaada kutoka katika nchi nyingine. Lakini Israel inaomba msaada wa kifedha na silaha hata pale inapopambana na kikundi cha watu wachache wasiofika hata elfu 50 ambacho sio nchi, sasa inawezaje kuwa taifa lenye nguvu kuliko nchi zote za eneo hilo?

Mbona tukifuata uhalisia wa kweli bila kutanguliza mihemko ya kipropaganda za magharibi ni kama vile Israel haiwezi kufua dafu hata mbele ya mziki wa Iran kijeshi, japo nchi hiyo ina vikwazo lukuki vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 70. Kama vikundi vidogo vidogo vinavyodhaminiwa na Iran iliyowekewa vikwazo kwa takribani miaka 70 Hezbollah, Hamas na vinaitoa kamasi Israel inayodhaminiwa kijeshi na kifedha na Marekani kwa zaidi ya miaka 80 tena bila kikwazo hata kimoja, je hiyo ndio ya kuuita yenye nguvu hapo Mashariki ya kati zaidi ya nchi zingine? Kuna kikundi kidogo tu cha vijana kadhaa kilichopewa silaha mbili tatu na Iran hapo Yemen, kimesababisha nchi kubwa duniani zaidi ya 10 kuingia baharini kwenda kupambana nacho. Hivyo kudai kuwa Israeli ni taifa lenye nguvu kwa sasa, kwakweli ni uongo wa dhahiri ambao kwa dunia ya leo watu wanaanza kuushtukia kutokana na kile kinachoendelea katika eneo hilo.

Fikiria hiyo miaka zaidi ya 70 ambayo muisrael anapewa misaada ya kijeshi na kifedha na Marekani pamoja na vibaraka wa magharibi, kama pia ingetumika kutoiwekea vikwazo Iran hali ingekuaje, bado wangeendelea kudanganya hivi hivi au wangeongea ukweli kwa sababu ingekuwa ngumu kuuficha ukweli huo?

4. Walidanganya kuwa Russia ni nchi hatari kwa usalama na amani ya dunia, japo Russia ni wazungu wenzao, lakini ukweli ni kwamba wazungu wa nchi za West ndio wanaoongoza kwa kuhatarisha usalama na amani katika nchi za wenzao. Wengi tuliona jinsi wafaransa walivyopachika wavaa kobaz huko Mali, Niger, na kwengineko ili aweze kutumia mwanya huo kuiba rasilimali za nchi hizo kupitia maeneo yale ambayo serikali haiwezi kuyadhibiti tena. Hata miaka kadhaa iliyopita Msumbiji iligundua kuwa katika eneo la kusini mwa nchi yake kuna utajiri mkubwa wa gesi, hivyo waliingia mkataba na kampuni fulan ya kifaransa kwa lengo la kuja kuchimba gesi hiyo kwa makubaliano maalum, bila kujua kwamba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inakaribisha nyoka katika ardhi yake.

Miezi michache tu baada ya wafaransa kuingia eneo la kazi na kuisoma vizuri ramani, wakaunda kikundi cha wavaa kobaz kama ilivyozoea kufanya katika nchi Mali, Niger, Gabon nk. Lengo la kuunda kikundi kile ni kutaka lile eneo lisitawalike na kampuni yao ijifanye inakimbia kutokana na sababu za kiusalama, kumbe nyuma ya pazia wawe bado wapo wanachota gesi hiyo watakavyo huku wakiwapa silaha na hela ya kula viongozi wa wavaa kobazi ambao wanajua kile kinachoendelea katika eneo hilo. Hivyo kusema kuwa Russia ni nchi hatari kwa usalama na amani ya dunia ni uongo mtupu wanaojaribu kutudanganya sisi watawaliwa ambao wanahisi hatuwezi kujua lolote.

Uongo wao ni mwingi, siwezi kuuorodhesha wote, ila wajue kwamba watawaliwa tumeshaamka, sio kila tango pori watakaloturushia sisi tutalimeza bila kulimung'unya ili kujiridhisha kuwa ni lenyewe kweli au tango la miba.
Jidanganye kamanda mwenzio katangulizwa Kwa bikira 72
 
Ila waarabu siyo waongo wala si wabaguzi!! Mzungu na mwarabu wote ni wakoloni waliotutawala mbaya zaidi Mwarabu alihasi (castrate) watumwa wa kiafrika na mateso yasiyo na mfano na hadi leo mahouse maid wa kiafrika wanateswa na kuuwawa uarabuni, ila cha ajabu waarabu na vibaraka wao wanataka waafrika wawachukie adui zao wazungu na wayahudi, Mkoloni ni mkoloni tu waafrika tusidanganyike na vibaraka wa waarabu.
 
Vifuasi vya magaidi vina hasira hivyo,ile oktoba 7 vilitarajia makubwa sana sheitwani bhana!
 
Watakuja tu kutupa documentary hawana mpya

Wazungu walitufanya kua mazombi muda mwingi sana kwakweli

Ila uzuri ujinga wao umejulikanika kweupee eeee
Na bado tutayajua mengi tu kuhusu uongo wao.
 
YAn hata operation Entebe, kama wale mateka wangekua bongo under JWTZ, israel asingeokoa hata mmoja na tungewalamba vyuma mpaka wasijue pa kutokea 😂😂.
Ni vile tu jeshi la Idd Amin lilikua la kijinga jinga
Ni kweli kwa hapa bongo wasingeokoa mateka hata mmoja. Labda kama wangetupa hela ili tujifanye tumeshindwa, kwa lengo la kutimiza uongo wao wa kuonekana kuwa wana jeshi bora 😄😄😄
 
Ila waarabu siyo waongo wala si wabaguzi!! Mzungu na mwarabu wote ni wakoloni waliotutawala mbaya zaidi Mwarabu alihasi (castrate) watumwa wa kiafrika na mateso yasiyo na mfano na hadi leo mahouse maid wa kiafrika wanateswa na kuuwawa uarabuni, ila cha ajabu waarabu na vibaraka wao wanataka waafrika wawachukie adui zao wazungu na wayahudi, Mkoloni ni mkoloni tu waafrika tusidanganyike na vibaraka wa waarabu.
Umeandika ujinga mwingi ambao hauna kichwa wala miguu. Kwa mbali unaonekana kama ni mtu unaejielewa, lakini baadae unarudi tena katika ujinga ule ule uliotengenezewa na waliokutawala.

Hii ni sawa na mtu unaeja-m-ba mwenyewe, alafu unajifanya haujui harufu inatoka wapi.

Mada imezungumzia mambo manne yanayohusu uongo wa wazungu, lakini mabrain wash mmejikita katika jambo moja tu la Israel kwa lengo la kila mmoja aonekane yeye ndio myahudi wa kweli, hata kama anaishi bonyokwa na midabwada yake, vizaka utafikiri kakatwa na nyembe miguuni huku hata hao wayahudi wenyewe anaopanua mdomo wake kuwatetea huku jasho la meno likimtoa wakiwa hawamjui yeye wala imani yake.

Waethiopia waliodanganywa kuwa na wao ni sehemu ya wayahudi kilichowakuta wewe mwenyewe kama ni mfuatiliaji wa mambo yanayotokea duniani utakuwa unakijua, mpaka wengine Kagame aliamua kuwahifadhi katika nchi yake.

Kinachoshangaza mtu ukiandika mada ambayo haioneshi kuwaunga mkono waisrael, basi hata wewe kama sio mfuasi wa dini zilizoletwa na meli, utalazimishwa kuitwa muislam au muarab na wachovu waliofilisika kiakili, ambao wao ukiwa kinyume na wale waliowaletea dini zao za kutunga wataanza kukupa majina na imani za dini ambazo hata mleta mada mwenyewe hazifahamu.

Mwl Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu mpumbavu utamjua upumbavu wake kupitia kauli zake. Yani mtu unaweza mfano kujadili ulilokutana nalo kwa mtu fulani bila kuhusisha imani yake, ila ghafla utashangaa anakuja mpumbavu aliefilisika kiakili na kulihusisha jambo hilo na dini yako au ya yule unaemjadili.

Ndiomaana hata raisi wa China aliwahi kutushangaa sana waafrika kwa kujifanya sisi ndio wenye kuzifahamu dini na kuumizwa zaidi na imani za dini hizo kuliko hata walioleta dini hizo.

Waafrika haswa watanzania mnatakiwa muamke na mbadilike. Achaneni na mawazo ya kipumbavu kwamba mtu akizungumzia Israel au Saudi Arabia anakuwa ameizungumzia dini ya mtu. Mbona juzi raisi Biden watu walianza kumkimbia kanisani alipokuwa anatoa hotuba yake! Wengi ambao wanaonekana wamekataa kuwa brain washed wa wazungu kanisani mle walionekana kukerwa na unyama unaofanywa na Israel huko Gaza, na hivyo kumtaka aamrishe vita visitishwe mara moja, maana inaonekana jeshi lenye silaha zinazosemekana ni za kisasa, intelejensia kubwa, na jeshi lenye weledi linashambulia waandishi habari, wanawake, watoto tena wengi wao ni wachanga wasiokuwa na uwezo hata wa kushika jiwe, kama hiyo haitoshi wanafikia hadi hatua ya kuuwa waandishi ambao ni raia wao wenyewe kisa wanaandika ukweli wa kile kinachotokea kwenye ground na kuuonesha umma kuwa kile tulichokuwa tunadanganywa na wazungu, waisrael na vibaraka wao ni uongo mtupu.

Hata sen. Benie Sander wa Marekani ni mzungu pyuu na haujui hata uislam kama mimi lakini kaamua kuwa sehem ya wapigania haki bila kujali dini ya wale anaowapigania. Pia anapingana na uongo wa wazungu wenzake kui over-rated Israel kwa zaidi ya miaka 70, lakini bado ni midebwedo yani hata kupigana na vijana wasiozidi elfu 20 ambao hawana ndege hata moja ya kijeshi, wanaomba tena msaada wa kijeshi wa Marekani 😄😄😄
 

Attachments

  • 13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    67.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom