Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Kuna kipindi alikuwaga manyaunyau, watu wamegombana Sana, mpaka Leo Kuna watu hawaongei,
 
Huyo muweka uzi ni muongo. Mtu halazimishwi kutoa fedha. Fedha zinachangwa kwa hiari. Na fedha hizo ni kwaajili ya wanaowasaidia hao wataalamu kufanya shughuli yao. Hao wataalamu hawachukui hata mia mbovu.
Kwamba hao wataalamu hawana familia au mahitaji yao binafsi?
Hizo pesa hua wanachukua hao waganga uchwara na wasaidizi wao Ila wao wanakula pakubwa.

Ni utapeli tu kama ulivyo utapeli mwingine hakuna zaidi na hakuna mchawi wanaweza kumtoa kwa usanii wao zaidi ni kudhalilishana tu.
 
Lengo la hiyo operation ni kuondoa huo uchawi,amini nakwambia uchawi umetajwa hadi kwenye vitabu vitakatifu,kwa hiyo upo.Ambaye familia yake ni wachawi ndoo wanalalamika na hii operation.
Sasa kama umetajwa mpka kwenye vitabu viatakatifu Leo hii nyinyi mtaweza kuuundoa kwa hizo operation zenu za maigizo?
 
Narudia tena ni Udhalilishaji, Upuuzi, Ushenzi, Uchonganishi na Utapeli.

Nimefika mkoa wa Kigoma Tokea Majuzi nilicho Kikuta huku Sielewi Huku ninchi Nyingine au ni Tanzania hii hii !

Kuna kitu kinaitwa  KAMCHAPE, hawa wapuuzi nani kawaleta, Hili kweli nani kalipa Baraka kufanyika karibu mkoa mzima wa Kigoma?

Kinachofanyika Ni Udhalilishaji na Uchonganishi kwa jamii.

Kwanza Wanachangisha Tsh 5,000 kila kaya kwa lazima sio ombi.

Kisha Wanapita kila nyumba Eti wanatoa Uchawi na wachawi! Tena utake usitake lazima.

Wakifika kwako wanasema hapa kuna uchawi Lazima uchapwe kisha unanyolewa Nywele Mbele ya umati wa watu kisha kunyweshwa Kile wanachoKiita Dawa hautakuwa mchawi tena!

Nimefuatilia kinachofanyika pale ni Mazinga Ombwe na Kujipatia Pesa kwa Utapeli!

Wakati Yakifanyika hayo Kijiji Jirani, Nyie mnaanza jiandaa na kama mwenyekiti hata Wakaribisha hao watu au kuchangisha hizo pesha kila kaya naye Anajumuishwa kwenye Kundi moja la Wachawi !

Kuna vitu vya Ajabu sana Vinafanyika mpaka nimeshikwa na Butwaa. Nimeuliza nikaambiwa Serikali Ndio Imeruhusu hili Lifanyike Mkoa mzima kweli?

Mbona Sioni Dodoma na Mbeya Kwanini Kigoma?

Kwasasa zoezi limepamba Moto Vijiji vya Nyarubanda, Kalinzi, Mukigo, Muhinda, Nyaruboza, Rukoma, Igalula, Mgambo, Katumbi, Kalya Nk.

Huko kumechafukwa hali ni mbaya na lisipofanyiwa kazi na kuacha litaleta shida kwa watu


Pia soma
- Mfahamu 'Kamchape' mkamata wachawi na shughuli zake kwa ujumla kutokea hapa Mkoani Kigoma
Huyo kamchape ni mchawi ila wachawi wenzie wanamuogopa
 
Haya yanafanyika hata huko songwe na chunya.Ni nani huwa anawaruhusu hawa wapuuzi? Hivi wakuu wa mikoa na wilaya ambao ndo wakuu wa ulinzi na usalama kazi yao ni nini dhidi ya kuwalinda wananchi hasa kwenye upuuzi kama huu?


Tanzania nchi ya hovyo sana
Hao unao waita wakuu wa wilaya ni watiifu kwa kamchape
 
Nyie mnaopinga hiyo Operation mnajua mateso wanaopitia watu huko inakofanyika hiyo Operation?

AFRIKA HAIENDELEI SABABU MACHAWI YANANENEPEANA TU KILA SIKU CHA KUSHANGAZA KUNA WATU WANAWATETEA HUMU!
Sasa hizo operation tngu lini zimewahi ondoa dhana ya uchawi kwenye jamii? Au unafikiri hiyo ndio ya kwanza? Zipo tangu enzi za mababu zetu na hazijawahi kuondoa kitu zaidi ya kudhalilishana tu.

Tena saizi zimevamiwa na matapeli wanachagua nyumba za watu wenye kauwezo wanakuja wanachimba wanafukia vitu hata mwezi kabla, siku ya operation wanafukua halafu wanasema ni mchawi unapigwa faini.

Hizo operation uchwara hakuna kitu ni utapeli tu na udhalilishaji na hazijawahi kusaidia popote pale zaidi ya kuwasaidia maisha hao kamchape.
 
Zoezi limeingia pia huku Katavi, wilaya ya Tanganyika katika makazi ya Mishamo. Yaani ni mwendo wa mchakamchaka kitaa Kwa kitaa.
 
Mtoto wa kaka yangu aliponeshwa na hawa watu amini usiamini

Unajua ilikuwaje..........

Mtoto wa bro. alikuwa mwenye afya njema hadi alipotimiza miaka 2 ndipo akaanza kuugua na kukonda huku akijisaidia kinyesi cheusi

Alikonda na kubakia mifupa hospitali alitumia dawa lakini hakupata unafuu,

Siku hao jamaa walivamia kijiji na walipofika kwenye kaya ya bro. alibainika mama mdogo alihusika na kumchezea huyo mtoto....

Uji ukatengwa kwenye jikoni na huyo mama mdogo aliukoroga huo uji kwa mkono wake hadi ulipoiva bila kuungua mikono yake.....

Baadae aliamriwa kumnywesha mtoto ule uji , tokea hapo mtoto alipata unafuu na kupona kabisa hadi leo hii ana familia yake.


Sasa nyie kama mnahisi kwamba serikali yenu hii fisadi itawasaidia kwenye mambo haya ya kiroho......nawashangaaa


Ya kaisari mwachie kaizari
 
Hii yote ni sababu watu hawaendi makanisani Kwenye ibada bali wanakubali udanganyifu na shoti kati
 
Back
Top Bottom