Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Ma ccm yakiona hivyo yanafurahi, jinsi wananchi walivyowajinga na mazuzu!
 
Hayo mapembe,watu wao wanayachombia usiku. I'll
 
Hii yote ni sababu watu hawaendi makanisani Kwenye ibada bali wanakubali udanganyifu na shoti kati
Makanisani kwenye,kuna baadhi ya madhehebu,ya kitapeli tu.
 
Jambo usilolielewa ni vyema ukasalia kimya kuliko kulizungumzia!
 
💔So kitabu Cha dini kikisema magonjwa yote ni mapepo nenda kaombewe we unaacha kwenda hospital...dunia imeendelea saa hivi unabidi uache Mila za kitoto na za kijinga
Mila za kitoto na za Kijinga...! Sema watu wengine wana Amini vitu usivyoamini....!

Kuna Nchi kama South Africa, unakuta wanaamini uwepo wa Mungu, wanasali na kuomba kwa namna yao, lakini hawaamini kuhusu Yesu, na wana sababu zao wakikupa unabaki kusema kila mtu wacha aamini anachoamini.

Mfano huwa wanaomba kwa Mungu kupitia Mizimu yao, ukiwauliza kwa nini wanachanganya mizimu na Mungu, wanakwambia Yesu mwenyewe ni Mzimu, aliishi na kufa zamani, kwa nini nimtumie Yesu kumfikia Mungu, wakati nina Ndugu zangu walishatangulia...!?
 
Naandika haya, nikiwa nimeshikwa na butwaa kubwa kwa Taifa langu Tanzania. Hapa Kigoma, limeibuka kundi la watu wanaojiita Kamchape. Watu hawa wanajitambulisha kuwa wanatoa watu uchawi. Hivyo wanazunguka vijiji kwa vijiji, kuwatoa uchawi hao wanaowaita ni wachawi. Ajabu ni kwamba, wanalazimisha watu kuwapa hela, la sivyo unapigwa na kuitwa Mchawi. Mpaka sasa nimeona watu kadhaa, ambao wamepata majanga hayo kwa kupigwa, kunyang’anywa mali zao na fedha wakiwemo viongozi wa dini. Kuna wakati nililazimika kumpeleka mtu Hospitali baada ya kupigwa vibaya kwa kuwa alikataa kutoa hela. Habari za Kamchape zimesambaa karibu Kigoma nzima, lakini hakuna jitihada zozote za kuwazuia watu hawa.

Mambo yanayofikirisha kuhusu Kamchape

  • Watu hawa wanajisifu kuwa wanatambulika serikalini, je Wametumwa na nani?
  • Kwa nini Serikali mkoa wa Kigoma haichukui hatua za dhati za kuzuia watu hawa, je wamewashindwa au na wao ni waamini wa mambo hayo?
  • Ikiwa hali hii ikiachwa iendelee tutakuwa na taifa la namna gani? Yaani mtu anapewa shutma za uchawi, na kupigwa au kunyang’wanywa mali. Maafa yatakuwa mengi sana na chuki itatawala Taifa
  • Nahuzunika kwa Taifa langu, nchi niipendayo kwa kuendekeza imani hizi za kishirikina na kutengeneza chuki na maafa kwa jamii.
 
Hao jamaa inatakiwa wapate mtu mmoja mwenye akili timamu akawashitaki watalipishwa hela hawatakaa wasahau!.. hiyo ni Moja kati ya fursa sema wanafanyiwa hivyo wamelala tu.. ingalikuwa Mimi sahivi tayari navibunda kadhaa mfukoni mwangu..😋
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…