Wewe ni mgonjwa wa akili. Ungetenga muda angalao ushughulikie tatizo lako la afya ya akili yako kuliko kuleta upuuzi humu JF.
Ungekuwa na uzima wa akili japo kidogo, ungeorodhesha wakati wa utawala wa Mkapa au Magufuli ni rasilimali gani ziliporwa na kuwagawia wageni kupitia mkataba wa kishenzi kama ule wa DP World. Ungeeleza pia wakati wa hizo tawala ni nani waliwahi kuhamishwa maeneo yao ya asili na kupelekwa mbali kabisa, ili kutimiza matakwa ya waarabu ambao hawataki kuwaona wamasai Ngorongoro. Fikiria mtu anahamishwa toka Manyara, anavuka Arusha, Kilimanjaro, na kupelekwa Tanga, kwenye mazingira mageni kabisa.
Halafu ulivyo na akili na kumbukumbu ndogo umeshindwa kukumbuka kuwa kiongozi mkubwa aliyetajwa kuwa ni fisadi wakati wa utawala wa Kikwete alikuwa ni Hayati Lowasa RIP. Hivi Hayati Lowasa alikuwa muislam?
Mtu kama Lucas Mwashamvwa ifahamike ni mgonjwa wa kichwani apuuzwe kwa maandiko yake takataka.