Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Binafsi huyu mzee kinana simuelewi haya majibu yake, ni anarukaruka tu kwenye majibu.

Mfano kwenye issue ya usawa wa wabunge wa znz na Tanganyika, nyingine ni amekubali kuwa ziliungana nchi mbili na akahitaja moja kuwa ni Zanzibar ila amekimbia na hakuitaja Tanganyika.

Pia ametoa mifano mingi kuhusu wingi wa wabunge na wingi wa wananchi kutoka nchi kadhaa, katoa mf. kutoka Switzerland ambayo ina idadi ya watu 8,842,736 na ikiwa na cabinet ya watu 8 tu.

Huo mfano umetokana na yeye mwenyewe kusema ni kihoja basi ni kihoja kweli.

Na kagusia TICTS ambayo ilikuwa mgodi wake ambao anajua fika alikuwa anaihujumu nchi ila kwa kuwa yupo upande wa kula mema basi anadhihaki.

Mengi anayoongea mzee Kinana siyo kweli vile hapa ukumbini wengi tuliopo ni kondoo tu.
 
Hivi kwa akili tu ya kawaida unaweza kuamini hilo. Wote tunajua basics za katiba mpya. Uzuri tulishaona mchakato wake before.

Kinana ni spin master wa CCM aliyebakia kwa sasa. Anachokifanya ni propaganda tu.

Hivi kajibu na maswali ya Muungano...!?
Tuwakumbushe kuwa Ifakara hakupo salama hizo posho wanazopeana Dodoma wapeleke kwenye mafuriko
 
Chadema ni washindi. Yaani kama mtu mmoja tu (Tundu Lisu) kaongea halafu ccm nzima inakusanyika kuanza kujibu.

Na pamoja na kukusanyika wote wameshindwa kupangua hoja hata moja. Kinana pamoja na kutumia muda mwingi sana kutoa maelezo lkn bado kashindwa kujibu hoja za Lisu.

Lisu hoyeee!!
 
Hayo magarasa wewe ndiyo unayaamini! CCM hivi sasa haina watu imebaki na manyangarakasha tatizo walitegemea dola kuwa ndiyo inayojibu kupitia kesi za mchongo, vijitu vijanja kama Lucas Mwashambwa ndivyo vimekuwa vinanajibu tofauti na hoja kisha vinakimbilia eti wametukana!
Anayemwamini Lissu ni chizi kama chizi mwenzie
 
Jimbo la Mbeya mjini lina wapiga kura laki200 inawezakanje kuwa sawa na Jimbo la micheweni znz Jimbo la watu elfu tano

hakuna usawa hata kinana akihutubia uchi

Zanzibar Ina wabunge takribani 80 kwenye bunge la jamuhuti kinyume na uwiano wa uwakilishi kwa idadi ya watu siyo sawa ni unyonyaji na ubagizi

Kwa uhalisia zenji inabidi iwe na wabunge 5 tu kwenye binge la jamuhuri
 
Kinana ajibu haya maswali:
1. Kwa nini leseni ya Tanzania haitumiki Zanzibar
2. Kwa nini Mtanganyika hawezi kununua ardhi Zanzibar
3. Kwa nini Mtanganyika hawezi kuwa DC Zanzibar
4. Kwa nini Wazanzibar wengi wameajiriwa Wizara ya Afya huku Tanganyika wakati afya siyo suala la Muungano
5. Kwa nini Mtanganyika hawezi kupiga kura Zanzibar
6. Kwa nini Wazanzibar wanakuwa viongozi kwenye masuala yasiyo ya Muungano Tanzania


NB: Wazanzibar wanabinya nafasi za Waislam wa bara kuwa Rais Tanzania maana mara nyingi Rais akitakiwa kuwa Muislam anatokea Zanzibar na akiwa Mkristu anatokea Bara. Hii siyo sawa maana Waislam wa Bara wanakuwa wanabaniwa nafasi ya kuwa Rais. Kati ya Marais watatu Waislam wa Tanzania wawili wametoka Zanzibar. Na JK alikuwa rais kwa sababu Zanzibar ilinyimwa zamu yake la sivyo hatungeweza kuwa na Muislam wa bara RAIS hadi leo
Akijibu mnitee
 
Back
Top Bottom