GODZILLA,
Siku zote mwamba ngozi huvutia kwake ili amfurahishe bwana wake aliyemtuma.
Hivi kweli huu ni unyama gani mmeuanzisha kipindi hiki cha miaka minne nyie Askari,tuliwaamini sana na tukawa tunaishi vizuri tu mtaani, tukawa tunapanga pamoja kwenye nyumba ya baba mwenye nyumba.Lakini kwa haya yanayoendelea sasa tumeogopa, unyama huu anaweza akafanyiwa yeyote kwenye nyumba ya baba mwenye nyumba.
Miaka minne iliyopita hatukuwahi kusikia wala kuona vitu vinavyofanyika na watu wachunga mali na watu wa Taifa.Ni aibu kwa Nchi, nchi inatoa harufu mbaya kwa majirani na mataifa mengine mpaka wanatushangaa.
Aibu hii tutajificha wapi sisi.Habari hizi zimeenea kila pande za dunia.Juzi tulikuwa na siku ya Wanawake yaliyozungumzwa huko tuliyasikia.Inasikitisha kwani hata aliyemvunja mkono sana sana bila shaka atakuwa mwanaume tena askari.Jamani hii wapi na wapi.
Nyie mnaofanya hivi vitendo viovu vya kuumiza Watanzania wenzetu, hakika mna watoto.Watoto wenu hii laana itaambatana nao kila watakapopita.Kumbuka maandiko yanasema kuwa, na matendo yao yataambatana nao.
Siamini kama haya yaliyozungumzwa na yanayoendelea kuzungumzwa na hawa wafungwa waliotoka huko ni ya uongo.Kwa sababu wote kwa nyakati tofauti wanazungumza mambo hayohayo yanayofanana.Iweje mtu mmoja aende kukanusha tena akiwa Dodoma wakati tukio limetokea Dar.Nilidhani kuwa angechukua muda kuchunguza ili ukweli upatikane na sio kukimbilia kukanusha kabla hajachunguza.
Magereza sio utumwani, wala sio porini, ni mahali panapoishi binaadamu na wala sio wanyama,panaishi pia wenye hatia,walioonewa, waliosingiziwa,na hata waliowekewa kesi za kufikirika.Tochi imeisha betri tutaonana kesho.