Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu


(Thought Experiment):

Fikiria hivi.

Imagine Leo binadamu wote duniani wanapatwa na aina fulani ya amnesia kali. Kila kumbukumbu inapotea. Hakuna anayekumbuka historia, sayansi, dini, falsafa — hakuna kitu. Vitabu vyote vinapotea. Data zote zinafutika. Tunaamka kesho tukiwa kama watupu kabisa kichwani hivyo tunaanza upya kabisa.

Sasa Imagine miaka 50 mbele.

Nini kitatokea?

Watu wataanza kuchunguza mazingira yao. Wataanza kuuliza kwa nini. Taratibu wataigundua tena kanuni ya mvuto (gravity), kwa sababu vitu bado vitaanguka kama zamani. Wataona mzunguko wa jua na mwezi, wataanza kuhesabu, wataunda hesabu (mathematics) kwa sababu idadi na mahusiano bado yapo. Watafanya majaribio, wataona matokeo yanajirudia. Hapo ndipo sayansi itaanza kujijenga tena.

Inawezekana majina ya formula, theories, SI Unit kuwa tofauti, lakini ukweli wa kimsingi utakuwa ule ule.

Kwa nini?

Kwa sababu sayansi haitegemei kumbukumbu za watu. Inategemea uhalisia wa dunia. Asili (nature) haibadiliki kwa sababu tumepoteza kumbukumbu.

Sasa fikiria upande wa dini.

Baada ya ile amnesia ya dunia nzima, je, Ukristo utarudi tena kwa muundo ule ule? Je, Uislamu utajitokeza tena na maandiko na manabii wale wale? Je, Uhindu utajijenga tena kwa cosmology ile ile?

Uwezekano ni mdogo sana.

Binadamu wataunda imani mpya — kwa sababu kutafuta maana ni sehemu ya asili ya mwanadamu. Lakini imani hizo zitakuwa tofauti kati ya jamii na jamii. Zitatofautiana na zile zilizokuwepo kabla ya amnesia. Hazitakuwa kama za zamani.

Kwa nini?

Kwa sababu dini zinategemea simulizi za kihistoria, mapokeo, na urithishaji wa kizazi hadi kizazi. Ukivunja mlolongo wa urithishaji, mfumo nao unavunjika.

“If all scientific knowledge were wiped out, it would eventually be rediscovered. If all religious knowledge were wiped out, it would not return in the same form.”
 
Kama tunasambaza uongo na ujinga shida iko wapi?

Nani alikwambia sio vizuri kusambaza uongo?
Nani alikwambia ni vizuri kusambaza uongo?
Kama mnasambaza uongo na ujinga, kwanini wenye kujua ukweli wasiseme kwamba mnasambaza uongo na ujinga?
 
Science inaelezea repeatable facts.

Dini inaelezea historia!

Apples and Oranges.

Huwezi kusema wataunda dini mpya, unasimama kwenye msingi / dhana potofu tayari: kuwa Dini zote ni uongo.

YOU'RE WRONG. Dini ya kweli IPO.

Maarifa ya kisayansi yatagunduliwa tena kwa sababu yanaelezea mifumo inayojirudia katika asili.

Vipi mambo yaliyotokea kabla ya kumbukumbu kufutwa? Je ni ya uongo au hayakuwepo kwasababu tu umeyasahau? ?

UKWELI utasimama milele.

Dini ya kweli ipo.

YESU ndiye KWELI.

Fanya kama kumbukumbu yako ilifurwa na sasa unatafuta ukweli upya. Ukitaka kusave muda, anza kwa YESU.
 
Nani alikwambia ni vizuri kusambaza uongo?
Kama mnasambaza uongo na ujinga, kwanini wenye kujua ukweli wasiseme kwamba mnasambaza uongo na ujinga?
Hilo swali ni la muhusika. Mradi amelikimbia, liache lisimame kama lilivyo.
 
From the mountain of information I posted ukaona hizo credentials ndo kitu cha maana kutolea maoni! ! !

Kwenda zako shetani! Usinitoe kwenye line.
 
Hakukuwahi kuwa na mtu aliyeitwa Yesu kwenye historia ya ulimwengu huu. Huyo anaeitwa Yesu ni "Character wa kutungwa alliyewekwa kwenye script inayoitwa agano jipya"
Hata wasiomwamini Yesu na wasomi ya historia wapagani wanajua Yesu aliishi hapa duniani.
Kusema kwamba hakukuwahi kuwa na Yesu kwenye historia ya ulimwengu huu ni kujidhalilisha uonekane mjinga.
Unaweza kataa kuhusu uungu wa Yesu, kufa na kufufuka kwake lakini kubishana kuhusu historical Jesus hata msomi mpagani asiyemwamini Yesu hawezi kukuunga mkono.

NB: Wazazi mkiwa mnapeleka watoto shule wasisitizeni wawapo masomoni wawe serious
 
Wala haukuhitaji maelezo mengi ku justify imani yako kwa Mungu.

Ukiwa una amini Mungu hutakiwi kuwa na mambo mengi ya kujifanya una mix na facts.

Facts ni adui wa imani, better stay on your lane.
 
Wala haukuhitaji maelezo mengi ku justify imani yako kwa Mungu.

Ukiwa una amini Mungu hutakiwi kuwa na mambo mengi ya kujifanya una mix na facts.

Facts ni adui wa imani, better stay on your lane.
Hayo ni maelezo sio maelezo mengi. Nani anayeamua kama ni mengi ama si mengi?

Mnapodai kuwa imani ni kinyume na sayansi au haina mantiki, ni jambo la akili kuonyesha kwamba sivyo, na siwezi kuelezea kwa sentensi moja!

Sio najifanya kumix imani na facts: nakuonyesha, nakuthibitishia kuwa imani na sayansi sio maadui.

Hakuna hoja hata moja uliyopinga zaidi ya kusema najifanya, stay in your lane. Hakuna ulichopinga kwa hoja hata kimoja! ! !

Mwenye facts anaonekana ni nani hapa.

Na anayejifanya naye anaonekana.

Kwenda zako shetani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…