Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Sisi wauza urembo unakuta mdada anataka wanja anachagua mmoja anautest halafu anarudisha anachukua mpya ambao haujaguswa ndio ananunua ule aliotest anakuachia .Hii tabia wanafanya hata kwa bidhaa nyingine pia .
Hivi hakuna tester kama perfumes ambapo unakuwa na za kujaribu tu
 
Wewe ni mnoma sana hadi bando la simu yako unatumia njia za panya.
 
Feedback toka kwa wateja wengine ni muhimu..maana hata aliexpress na nk huko unakuta watu wameweka reviews zao kibao...
 
Me nko mbeya na huu ni mwaka wa 7 nanunua bidhaa online...nikisha kuamini,hata mzgo uwe wa mil 5 nakutumia
Hununui kwa wabongo bila shaka....
Wabongo online uaminifu zero.
Tena wale wanaojifanya kuagiza sijui China ndio wametapeli sana pesa za watu aisee.
 
Yaani chief watu wanakuuliza maswali ambayo yana majibu kwenye description tena umeyapanga very clear.
Tatizo wafanyabiashara wa online bongo hamuaminiki kwahiyo muendelee kuvumilia tu watu wanapohoji kujiridhisha
 
Basi mfunge biashara maana kutulalamikia wateja kumekuwa kwingi mnoo. We unataka watu wote wafanane who are you? Alowaumba mwenyewe kawaumba tofauti tofauti. Umba wateja wako wanaofanana ebo!!

🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mteja nikitoa povu.
 
Elimu ya customer care mkuu unamaanisha nini kuweza kuvumilia ujinga wa wengine..

Ili kupunguza maswali unaweka maelezo yote yaliyoshiba tena kwa msisitizo ili mtu akija inbox basi aje kama mnunuzi. kama sio mnunuzi ni alipite tu tangazo.
Msumbufu wa leo ni mteja wa kesho au ni balozi bila malipo. Kuna jamaa mmoja alinieleza kilichomtokea, alifika mteja dukani kidogo amwambie ondoka ila uvimilivu na huduma yake ilimpa biashara nzuri sana.
 
Yaani chief watu wanakuuliza maswali ambayo yana majibu kwenye description tena umeyapanga very clear.
Wateja wengine ni wasumbufu sababu ya kulizwa.

Hujawahi sikia dalali kapost vitu online ila kacopy and paste na hajui in details alichopost? Unamuuliza swali ambalo jibu lipo kwenye post na anakata ili asome jibu ndo akurudie.
 
Wauzaji pia sio waaminifu.. ndo maana wateja tunakua na maswali mengi ili kujiridhisha na huduma mkuu..
Imagine kuna mzgo nmeagiza kutoka dar tangu J3 ya wiki iliyopita, ila cha ajabu mpaka leo muuzaji hajautuma.

Uaminifu wenu ni ZERO
Kwa kuongezea.

Mteja anachagua bidhaa na kulipia. Baada ya kupokea mzigo unakuwa tofauti na alichochagiza.

Wengi sana wanashindwa kuzinagtia mahitaji ya mteja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…