Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Unawaongeleaji Wauzaji ambao huwa wanaweka picha ambazo si halisi??

Mtu anauza gari anatumia picha za gari hilo lilipokuwa kwenye hali nzuri miaka kadhaa nyuma.
 
Hii km ni kweli basi labda useme ni uko mambeleni. bongo tunajuana vizuri hakuna mtu wa kukufanyia uaminifu uo na hasahasa iwe DSM!
Bongo hii hii mkuu nimeshanunua vitu kibao tu instagram na sijawahi kupigwa.
 
Mi naekaga hadi bei kwenye picha ya bidhaa.bado unaulizwa bei gani hii na picha ile ile..
 
Inaonekana bado biashara sio talanta yako. Unajua Kuna pesa laini. Kumbuka mitandao bado Ni migeni hapa afrika labda baada ya 50yr or 100 itakuwa kitu Cha kawaida kabisa.
 
Ni kweli lazima mteja aulize maswali ili akinunua bidhaa anunue bidhaa ambayo anaiitaji au kuna rafiki yake anayo
 
Mkuu lazima wakuulize ili wajilizishe je kilicho andikwa ni wewe umekiandika au umekopi sehemu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Biashara ya mtandaoni inahitaji vitu vitatu tu... Professionalism, Excellence na Integrity ukikosa kujifunza mambo haya mara kwa mara nakuhakikishia 100% biashara itakushinda..., Biashara bila mteja ni hasara, Mheshimu sana mteja maana yeye ndio nguzo ya biashara yako.
 
Wauzaji pia sio waaminifu.. ndo maana wateja tunakua na maswali mengi ili kujiridhisha na huduma mkuu..
Imagine kuna mzgo nmeagiza kutoka dar tangu J3 ya wiki iliyopita, ila cha ajabu mpaka leo muuzaji hajautuma.

Uaminifu wenu ni ZERO

Sio wote wachache ndio wanafanya ayo mambo
 
Elimu ya customer care mkuu unamaanisha nini kuweza kuvumilia ujinga wa wengine..

Ili kupunguza maswali unaweka maelezo yote yaliyoshiba tena kwa msisitizo ili mtu akija inbox basi aje kama mnunuzi. kama sio mnunuzi ni alipite tu tangazo.

Yes nikweli aise wateja wengi awapo seriously kama FB Mungu wangu FB kuna ujinga mno unalipia tangazo lako alafu watu wanakuja kukuuliza maswali ulio yatolea majibu kwenye post
 

Kabisa wasumbufu wameguswa
 
Huu uzi ni mzuri sana kwa Wafanyabiashara wanaouza bidhaa mtandaoni na wateja wao maana una maoni mchanganyiko ambayo ni mazuri,kila mtu ayatumie kujifunza.Biashara ya mtandaoni haikwepeki miaka michache ijayo itashika kasi sana na ndiyo itakayotawala soko.Cha muhimu wateja wavumiliwe mtu anayetoa fedha yake kununua bidhaa yako hata kama ni tsh. 200 mshukuru sana na mpe thamani kubwa maana akiridhika na huduma yako siku nyingine atakuja kununua bidhaa za 10,000 kisha za 1,000,000 kwahiyo muache aulize hata maswali milioni.Mteja ni bosi na kumbuka bosi hanuniwi na vilevile mteja ni Mfalme na Mfalme anatoa amri na zinatekelezwa na pia ananyenyekewa.
 
Uzoefu wangu kwa uchache.
nina miezi mitatu, nimeuza bidhaa 300+ kupitia online.

NILIYO KUTANA NAYO
Wateja wengi wanahofu ya kupigwa hivyo wateja zaid ya 150 niliwaruhusu wanilipe baada ya kupokea mzigo Kati yao 4 wakanipiga(hawajanilipa kabisa), 2 wakajipa punguzo wakalipa pungufu ya kiasi tulicho kubaliana japo kidogo. kifupi zaid ya 96% ya waliosema watalipa baada ya kupokea walilipa.

Wateja wasumbufu wapo, mfano anakuambia umtumie mzigo ukifika anakuambia mzigo urudi kaenda kijijini au anamatatizo hela imepungua n.k.

kama mlikuwa mnachat online hakikisha anakupa namba ya simu inayopatikana, unaweza fanya delivery ukafika sehemu husika mteja yuko offline.

WATEJA
Akiwa Mzungu, hindi, mtanzania aliyeishi nje, au raia wa taifa tofauti basi 100% niliuza bila kutaka maelezo sana.

Pia wapo watanzania ambao wako very straight mnafanya biashara ndani ya muda mfupi.

Hao wengine nisiwazungumzie, nimewauzia zaidi ya watu 300 online ila waliofika inbox kuhusu bidhaa ni zaidi ya 1000.

kuulizwa kitu umesha eleza kupo.

wanunuaji wengi huwa hawa comment, wanapiga simu au inbox.

kwenye post yako atakuja mtu ata comment "UTAPELI".
sikatai utapeli upo, mwenyewe nilitaka kutapeliwa Zanzibar uzuri nilienda mwenyewe baada ya kufika location akani block nikarudi, ila sio kila muuzaji online ni TAPELI.

MAPUNGUFU YANGU.
Nafanya kama part time, muda mwingi nabanwa na shughuli nyingine hivyo natumia wastani wa masaa 2 kwa siku hasa jioni. hii hupelekea

kidogo kuchelewa kujibu meseji mara nyingine. ila huwa najitahidi kushika simu kila nipatapo nafasi.

huwa nakosa muda wa kuijaribu bidhaa hivyo nyingi nimezituma zikiwa hazijafunguliwa, imetokea mara 2 bidhaa zikawa na mapungufu baada ya mteja kupokea mkoani ila wote niliwatumia nyingine. Tatizo moja ilisafirishwa vibaya na nyingine ilikuwa haiwaki tu (Nikawabadirishia 🤝).

Namba ngeni huwa napokea nyingi sana katika shughuli zote ninazo fanya hivyo kumuuliza mteja ni nani akinipigia haliyakuwa tumechati ni kawaida.


Baada ya mwenzi wateja niliowauzia mwanzo wakaanza niletea wateja.

na huu ndio uzoefu wangu kwa uchache ndani ya hiki kipindi kifupi, japo nafanya kama part time tu, kwani muda ninaotumia kwa siku kufanya hii biashara, wastani ni masaa 2.
 

Safi. Unauza nn naweza kukuunga
 
Sahihi 💯 mkuu hata mimi ni ishu ya ziada maana kwa aina ya shughulinzangu wakati mwingine najikuta ndani ya siku 2-3 za week niko free.

Wanaocomment sana asilimia kubwa ni mba mba mba tu si wanunuaji yaani kwa muda mfupi nimexprience. Wanaoniiungisha ni wale wanaopiga simu moja kwa moja.
wanunuaji wengi huwa hawa comment, wanapiga simu au inbox.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…