Uzoefu wangu kwa uchache.
nina miezi mitatu, nimeuza bidhaa 300+ kupitia online.
NILIYO KUTANA NAYO
Wateja wengi wanahofu ya kupigwa hivyo wateja zaid ya 150 niliwaruhusu wanilipe baada ya kupokea mzigo Kati yao 4 wakanipiga(hawajanilipa kabisa), 2 wakajipa punguzo wakalipa pungufu ya kiasi tulicho kubaliana japo kidogo. kifupi zaid ya 96% ya waliosema watalipa baada ya kupokea walilipa.
Wateja wasumbufu wapo, mfano anakuambia umtumie mzigo ukifika anakuambia mzigo urudi kaenda kijijini au anamatatizo hela imepungua n.k.
kama mlikuwa mnachat online hakikisha anakupa namba ya simu inayopatikana, unaweza fanya delivery ukafika sehemu husika mteja yuko offline.
WATEJA
Akiwa Mzungu, hindi, mtanzania aliyeishi nje, au raia wa taifa tofauti basi 100% niliuza bila kutaka maelezo sana.
Pia wapo watanzania ambao wako very straight mnafanya biashara ndani ya muda mfupi.
Hao wengine nisiwazungumzie, nimewauzia zaidi ya watu 300 online ila waliofika inbox kuhusu bidhaa ni zaidi ya 1000.
kuulizwa kitu umesha eleza kupo.
wanunuaji wengi huwa hawa comment, wanapiga simu au inbox.
kwenye post yako atakuja mtu ata comment "UTAPELI".
sikatai utapeli upo, mwenyewe nilitaka kutapeliwa Zanzibar uzuri nilienda mwenyewe baada ya kufika location akani block nikarudi, ila sio kila muuzaji online ni TAPELI.
MAPUNGUFU YANGU.
Nafanya kama part time, muda mwingi nabanwa na shughuli nyingine hivyo natumia wastani wa masaa 2 kwa siku hasa jioni. hii hupelekea
kidogo kuchelewa kujibu meseji mara nyingine. ila huwa najitahidi kushika simu kila nipatapo nafasi.
huwa nakosa muda wa kuijaribu bidhaa hivyo nyingi nimezituma zikiwa hazijafunguliwa, imetokea mara 2 bidhaa zikawa na mapungufu baada ya mteja kupokea mkoani ila wote niliwatumia nyingine. Tatizo moja ilisafirishwa vibaya na nyingine ilikuwa haiwaki tu (Nikawabadirishia [emoji1666]).
Namba ngeni huwa napokea nyingi sana katika shughuli zote ninazo fanya hivyo kumuuliza mteja ni nani akinipigia haliyakuwa tumechati ni kawaida.
Baada ya mwenzi wateja niliowauzia mwanzo wakaanza niletea wateja.
na huu ndio uzoefu wangu kwa uchache ndani ya hiki kipindi kifupi, japo nafanya kama part time tu, kwani muda ninaotumia kwa siku kufanya hii biashara, wastani ni masaa 2.