Uchaguzi 2020 Kufungiwa Lissu kwa siku 7 ni ‘advantage’ kubwa sana kwake

You nailed it!!!!Kwa kweli umeongea kama nilivyokuwa nawaza na nilivyoandika sehemu mbalimbali.Atulie,atafakari
Unajua kwa sasa CCM imejawa hofu ya kushindwa uchaguzi imefura imekwama inatafuta kila sababu ili na Lissu akwame.
 
Unajua kwa sasa CCM imejawa hofu ya kushindwa uchaguzi imefura imekwama inatafuta kila sababu ili na Lissu akwame.
Kushindwa CCM sio kama ni jambo feasible kwa sasa lakini wakati mwingine "Wasiwasi ndio akili"
 
Namba saba ni namba ya ukamilifu katika ulimwengu wa roho, yeye atulie apange mikakati, hizo siku saba wazitumie kiroho zaidi hasa maombi ya siku saba, chama kijigawe makundi Saba ya kuomba kura kwa njia watazaona wao, wazee wao, wabunge, madiwani, wamama, vijana, wababa, na viongozi katika hizo siku saba na Mungu atawashindia.
 
Ushauri mzuri sana aupokee na kuufanyia kazi aachane na heroics hazimsaidii yeye binafsi wala wananchi wengi wenye matumaini nae. Hizo siku 7 za adhabu akizitumia vizuri na kikamilifu litakuwa pigo kubwa kwa adui zake ambao wanasubiri kwa hamu afanye kosa dogo wammalize kabisa lakini pia kumaliza adhabu kunaweza kumwongezea wapiga kura mara dufu. Halmashauri/Kamati Kuu ya Chama chake imshauri aachane na nia yake ya kuendelea na kampeni mpaka baada ya adhabu wakati huohuo wakiangalia namna ya kutumia muda wa adhabu kwa manufaa ya Mgombea wao. Wapiga kura wanasubiri kwa hamu kuona hatua atakayochukua na kitakachoendelea ili wafanye uamuzi wao wa mwisho maana bado wana imani nae na wanafuatilia na kulaani yaliyompata na yanayompata. To sup with the Devil you need a long spoon!
 
Wakati mwingine mtu hujitathmini akiwa kwenye utulivu na kubadili msimamo wake aidha kwa kubaini uhalisia wa jambo au kwa kusikiliza hoja za washauri wake wa karibu. Hiyo siyo dhambi, ni kuonyesha ukomavu wa kifikra. Daima mwanadamu tangu kuumbwa hajawahi kukamilika bali hukamilishwa na wanaomzunguka na kumtakia mema.
 
Kama ni ushauri kwa kweli tumempa,KAZI KWAKE!!
 
Tatizo ccm hamuamini kinachotokea kwa kuinasibu kufanya mambo mengi Kama kununua ndege na kujenga flyover mlidhani kua lisu hatapata support yeyote kwa wananchi , sasa mambo yaanenda tofauti mmeamua kutumia njia nyingine ya kumnyongonyeza bila ya kujua kumbe ndio mnampa kiki zaidi , mm nilikua sina mpango Wa kupiga kura mwaka huu ,lakini kwa haya yanayoendelea , inabidi tu niende nikampigie kura lisu aisee , maana wengine hua hatupendi uonevu ,
Inabidi tu nimpe faraja lisu kwa kumpigia kura tuu.
 
Wengine wameanza kujinyonga kwa kujua imekula kwao
 
Kweli sio kila biashara inahitaji matangazo, brand bora inajiuza yenyewe..
 
mwaka huu mtaaanzisha thread za kutosha mbna, na isisahaulike kwamba kesi zake znaskilizwa baada ya uchaguzi tu MFULULIZO: hili si la kusahau
 
Kwa hyo Bora nini tuingie kwenye Vita au tulinde amaani yetu?.
Unadhani Vita ikitokea hayo unayosema yatafanyika Tena?.
Nani atalima mazao wakati wa Vita?
Nani atanunua mazao wakati wa Vita?
Hawajui madhara ya vita hao
 
Kwa hyo lisu ndo amekwambia atakusaidia kwenye hayo matatizo?
 
Ccm kwa sasa kuondoka madarakani ni ndoto yasaa saba mchana.
Ila isiwe sababu ya kupotea kwa amani ya nchi yetu.
Wakati mwenyekiti wa tume anachaguliwa na rais aliyepo madarakani na ni mwenyekiti wa ccm NYIE MMEKAA KIMYA.
wakati mkurugenzi wa uchaguzi anachaguliwa na rais aliyepo madarakani na mwenyekiti wa ccm NYIE MMEKAA KIMYA.
wakati IGP, CDF,DG n.k wanachaguliwa na rais aliyepo madarakani na mwenyekiti wa ccm NYIE MMEKAA KIMYA.
alafu mnataka mje mshinde Hilo msahau.
Lakini pia isiwe sababu ya kutuvunjia AMANI YETU.
nendeni mahakamani mkadai tume Huru,MAJESHI HURU
 
Wananchi wameichoka ccm wanataka waangalie upande wa pili wa shilingi.

Hali zao ngumu za maisha hawana wa kumlaumu zaidi ya ccm waliong'ang'ania kukaa madarakani miaka yote hiyo.

Inaweza isiwe mwaka huu ila mwisho wa ccm unaonekana
 
Akili kubwa, madini aina ya vito, big up man
 
Excellent
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…