Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko
Mama ashaanza kuonja utamu wa Ikulu, kuteua na kutengua si mchezo.

Meko alikuwa anadanfanya eti hii kazi ngumu-ujanja tu!

Eti katiba huko mbeleni ahahaha hamna mtu hapo! Na akiruhusu katiba mpya atakuwa Rais mwenye historian zote ikiwemo ya kuwa Rais wa mwisho wa CCM
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha rais Samia kuwa, hoja ya katiba mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo

1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi
Rais anaposema eti tumpe muda ajenge uchumi kwanza ndo afikirie katiba mpya, tungependa kumueleza rais kuwa kuwa na katiba mpya hakumzuii yeye au serikali yake kukjenga uchumi, Labda Rais atueleze, je katiba bora iliyo nzuri inazuiaje yeye kuvutia wawekezaji, inazuiaje kuboresha utalii, inazuiaje kujenga miundo mbinu?. Hapa kimsingi rais hana hoja yenye mashiko kabisa juu ya kukataa kuwapa wananchi aina ya katiba wanayoitaka.

2. Mchakato wa katiba mpya si hisani ya rais bali ni hitajio la kisheria
Ipo sheria ya mwaka 2012 inayogovern mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya, Sisi wananchi tunamtaka rais atekeleze sheria hiyo, asifanye hili suala kama hisani yake binafsi, hili ni hitajio la wananchi wengi.

3. Hofu ya rais ni ya kisiasa na si kimaslahi ya kitaifa
Kauli ya rais ya kukataa kuipa katiba kipaumbele ilianza kwenye awamu ya tano ambayo yeye alikuwa makamu wa rais, rais wa wakati huo na yeye alisema hoja hizohizo za kujenga uchumi kwanza kabla ya kuleta katiba mpya, leo hii tuna miaka mitano bado tunapigwa kalenda hizohizo za ngoja tujenge uchumi. Huhitaji kuwa genius kuona kwamba hofu ya viongozi hawa ni hofu za kisiasa tu, za kuhofia hatma zao na vyama vyao kisiasa iwapo Taifa litapata katiba mpya, ni dhahiri wahafidhina ndani ya CCM hawataki. katiba mpya, lakini kama alivyowahi kusema katibu mkuu mstaafu wa CCM, Hoja ya katiba mpya haitakufa mpaka ipatikane.

4. Kujenga uchumi bila kuwa na katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa rais mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila katiba nzuri huwezi kuulinda uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la katiba mpya ni muhimu sana

5. Watanzania hatuko tayari kurudi katika utawala wa kidikteta aina ya awamu ya tano
Ktk utawala wa awamu ya tano tuliona matendo ya kinyama na kiuonevu yaliyofanyika, sababu mojawapo ya matendo hayo ni kuwa na katiba inayotoa mwanya mtawala kuvunja sheria bila consequences ikiwemo kushtakiwa, Katiba hii imetoa mamlaka makubwa kwa rais, na kiukweli ni katiba ya kidikteta, Hatuwezi kuruhusu scenario ya kupata aina ya uongozi wa awamu iliyopita, na guarantee bora ya kutofika huko ni katiba mpya na si maneno matamu tu ya rais Samia
Mimi ni muumini wa katiba mpya lakini hoja ya kuinua uchumi inamashiko uchumi ulivurundwa kutokana na sera ambazo hazina muelekoe, 'policy uncertainty and herding behaviour', herding behaviour is an occurrence of thoughtful people suspending their individual reasoning because of panic or fear of their leaders(unyumbu) awamu ya 5 biashara zimekufa siyo kwakukosa mitaji ama elimu ya ujasiriliamali
 
Watu wananjaa na bado wanapiga kelele ile mbaya wakishiba sijui itakuajee!?
 
Hii katiba ipo toka mwaka 1977 ingekuwa nzuri basi CCM wasingeiweka kwenye ilani ya uchaguzi mwaka 2015 ibadilishwe. Ofcourse tunajua kuwa Serikali ya Magufuli na Samia akiwa makamu wake ilifanya uhuni na kukataa kutekeleza suala hilo!

Haiwezekani mtu aliyeomba kazi ya kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la kubadili katiba aone eti katiba mpya siyo kipaumbele chake. Kwa hii flipflop ambayo rais anaifanya anaonyesha kuwa naye kanogewa na katiba hii ya kidikteta
Anavutia wawekezaji akishirikiana na Mulamula. Wanataka waache legacy fulani. Kwenye 2023 au 2024 mchakato wa katiba unaweza kuanza tena.
 
Hatutaki Tanganyika kuendelea kuvaa koti la Muungano
 
Jiwe alijua kutetea hoja zake hata kama ni upuuzi. Sikumpenda jiwe kabisa lakini ilikuwa ukisoma speech zake unaelewa anaongelea nini
Jiwe alisema tutamkumbuka ndio kama hivi sasa, jumong sijawahi kuona mantiki kwenye speech zake karibu zote
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
Kujenga uchumi ni kazi ya kila siku ya serikali yoyote, haiwezi kuwa excuse ya kuwanyima wananchi katiba bora ambayo ni msingi wa siasa safi na uongozi bora vitu ambavyo ni misingi ya maendeleo!
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Anahisi kila muda kwamba yeye sio "mkuu" anakaa kutukumbusha kila siku nafasi yake, akimaliza hapo anaongelea jinsia tu. Hayo ndio mambo anayoweza.
In short hana consistency, jiwe alikuwa akisema leo hakuna corona kesho na kesho kutwa atasema hivo hivo, ila jumong juzi alisema tujikinge kwani nchi jirani zina wimbi la tatu, jana akasema mengine, leo amesema kuna wagonjwa zaidi ya 100, sasa je hao wamepatikana kwa siku moja ? Na kwanini hataji idadi kamili
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.

Sisi ni wananchi na tunataka katiba mpya, hao wananchi wanaotaka wapate mkate wao, katiba mpya haizuu mkate wao, bali itawapa mkate wa siagi.
 
Siku Chama cha Mapinduzi kikikubali suala la Katiba ndo itakuwa mwisho wa uhai wake.Amini usiamini
 
Back
Top Bottom