Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko
Kilichoshuka ni kasi ya ukuaji wa uchumi, lakini uchumi wetu bado unakua.

Usisahu kuwa tuko uchumi wa kati!
sio Tanzania tu iliyo pigika kiuchumi bali Dunia nzima ipo ktk kipindi kigumu sana kiuchumi, ni ajabu kwa wanasiasa kudai mchakato wa katiba mpya ktk kipindi hiki kigumu cha kiuchumi bila hata kuwaonea huruma wananchi.

Wanacho waza wanasiasa wao ni kutwaa dola tu hawana mpango na umasikini unao tukabili. Hata hivyo katiba mpya ni jambo jema ila ni vyema tukawa na subira kwani subira yavuta heri.

Tusiwe ving'ang'anizi kama ruba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama ni mwepesi sana..upinzani waki fail i term wasahau kabsa
Hujui nguvu ya kile kiti yaani.

Tafsiri ya hiyo nguvu ni jenga picha watoto wadogo wenye kaka yao wa miaka 10 wameachiwa makampuni kama urithi na baba mwenye watoto wengine wengi na mama tofauti tofauti ambao ni watu wazima, wale watoto wakapewa na msimamizi ambaye ni mmoja ya mtoto wa marahemu, Sasa ile nguvu ya maamuzi ya msimamizi kwenye makampuni ipoje?

Sasa upinzani ni mtoto mkubwa wa miaka 10 na raisi ndo msimamizi wa urithi.
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo...

Kuna kitu umesahau
Katiba mpya inaitaji pesa tena pesa nyingi

Serikali haina hiyo pesa kwa sasa, unless useme ww na familia yako mtatoa hizo pesa,

Chadema mnadhan katiba mpya itawasaidia kwa lolote but nothing will change
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.

Sema kukuamulia usitujumlishe na sisi
 
sio Tanzania tu iliyo pigika kiuchumi bali Dunia nzima ipo ktk kipindi kigumu sana kiuchumi, ni ajabu kwa wanasiasa kudai mchakato wa katiba mpya ktk kipindi hiki kigumu cha kiuchumi bila hata kuwaonea huruma wananchi.
wanacho waza wanasiasa wao ni kutwaa dola tu hawana mpango na umasikini unao tukabili.
hata hivyo katiba mpya ni jambo jema ila ni vyema tukawa na subira kwani subira yavuta heri.
tusiwe ving'ang'anizi kama ruba.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kitu ambacho chadema hawajui ni kuwa hata kukiwa na katiba mpya still wanainchi ndio watachagua viongozi
 
Kwa taarifa yako mimi si mwanasiasa lakini nataka kuona Tanzania yenye Utawala bora utawala wa sheria. Tanzania yenye chaguzi zilizo huru na haki na Watanzania tukawa na uhuru wa kuchagua madiwani. wabunge na Rais tuwatakao bila ya kura zetu kuibiwa kupitia mtutu wa bunduki na ile Tume FAKE ya uchaguzi. Tumechoka na chama kung’ang’ania madarakani kwa miaka 60 kwa mtutu wa bunduki huku wakiwa hawana jipya.
Uchaguzi huru ni chadema kushinda?
Utawala bora ni kuruhusu chadema kuandamana mitaani?
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo...

Ni kweli kabisa...

Tatizo moja kubwa na la hatari kwa watawala hawa na chama chao - CCM ni kudhani kuwa;

1. Watakuwa watawala milele. Hawajui kuwa siku moja (na ipo tayari) watakuwa hawana uongozi tena wa kiserikali. Hebu fikiri, CCM hii bila dola na chini ya katiba hii mbovu itakuwa CCM ya namna gani..?

2. Katiba iletayo usawa kwa Makundi yote ya kijamii haiwahusu wao. Wanaamini kuwa, wao ndiyo wenye hisani ya kutuamulia mfumo wetu wa kikatiba na kiutawala wa nchi yetu ambao unalinda maslahi yao..

USHAURI KWA SAMIA SULUHU HASSAN NA CCM YAKE:

Mnakosea sana. Mnachimba kaburi lenu mwenyewe. Mnao muda na mamlaka ya kutengeneza mambo haya sasa kwa manufaa yenu ya baadaye...

Ni bora mkatengeneza mazingira ya kikatiba sasa kukiwa na giza hili bado ili kesho mkiangaziwa na jua, mpate pa kuficha uchi wenu...

Nyakati na majira yamekwisha wadia wa kutokuwa na control ya dola na serikali. Hili liko crystal clear. Maandishi yako ukutani lakini hamuwezi kuyasoma na kuyaelewa kwa sababu mmelewa mvinyo wa madaraka uliochanganyikana na damu za watu, mkapumbazika na kujiona nyie ni miungu mnaoweza kuamua hatima ya mtu yeyote kwamba huyu aishi na huyu afe...

Uzoefu huu wanaopitia ndugu zenu walio nje ya dola na serikali chini ya katiba hii, kwenu utakuwa mchungu sana na pengine ndiyo itakuwa mwisho wa CCM hapa duniani kama hamtajiandalia mazingira mazuri ya kustaafu kwenu.!!
 
Ni kweli kabisa...

Tatizo moja kubwa na la hatari kwa watawala hawa na chama chao - CCM ni kudhani kuwa;

1. Watakuwa watawala milele. Hawajui kuwa siku moja (na ipo tayari) watakuwa hawana uongozi tena wa kiserikali. Hebu fikiri, CCM hii bila dola na chini ya katiba hii mbovu itakuwa CCM ya namna gani...

Hata katiba mpya ikiwepo.

Chadema haiwez kuongoza Tanzania never
 
Hata katiba mpya ikiwepo
Chadema haiwez kuongoza Tanzania never
Siyo lazima iwe CHADEMA lakini inaweza kuwa CDM au MADECHA party...

Lililo na uhakika ni hili;

CCM imekwishakufa kifo cha kawaida siku nyingi. Kilichobaki ni dola kukipa kisogo tu chama hiki na kifo chake kuthibitika rasmi na ndiyo mwisho wake wa milele...
 
Wanasiasa, mjuwe sisi wananchi, hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa, kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani, tukishapata mahitaki muhimu, hatuna zaidi ya hapo.
Huko ni kutokuelewa kwamba katiba bora inakuwezesha kupata vyote hivyo kwa ubora zaidi. Katiba mbovu ndiyo iliyompa mtu mmoja madaraka ya kuamua kujenga uwanja wa ndege kwao badala ya kununua dawa, kuanza mradi wa kujenga bwawa la Nyerere badala ya kuendeleza miradi ya gesi ambayo tulishaianza, kuingia mikataba ya kununua ndege bila kilishirikisha bunge na madhara mengine ambayo yangeepukika kama tungekuwa na katiba yenye kudhibiti mamlaka yake.
 
Siyo lazima iwe CHADEMA lakini inaweza kuwa CDM au MADECHA party...

Lililo na uhakika ni hili;

CCM imekwishakufa kifo cha kawaida siku nyingi. Kilichobaki ni dola kukipa kisogo tu chama hiki na kifo chake kuthibitika rasmi na ndiyo mwisho wake wa milele...

Kwa hoja hizi ndio hata katiba mpya ikija hakuna kitu kitatokea
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi? Wananchi wengi, tunataka uchumi, tupate mkate wetu wa leo na kesho, mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa, sisi wananchi bora mkono uwende kinywani. Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi, hata kwa kupiga kura, kwenye maeneo yenu.
Hata mama akikidhi haja zako zoote!; Yeye Ataondoka Katiba Itabakia!
Jee Akija mwingine uongozi wake haushahabiani na huyu mama! Yeye akavuruga uchumi na mkate wako Wa kila siku ndipp utakapo ona Umuhimu wa Katiba
 
Sio Tanzania tu iliyo pigika kiuchumi bali Dunia nzima ipo ktk kipindi kigumu sana kiuchumi, ni ajabu kwa wanasiasa kudai mchakato wa katiba mpya ktk kipindi hiki kigumu cha kiuchumi bila hata kuwaonea huruma wananchi.

Wanacho waza wanasiasa wao ni kutwaa dola tu hawana mpango na umasikini unao tukabili. Hata hivyo katiba mpya ni jambo jema ila ni vyema tukawa na subira kwani subira yavuta heri.

Tusiwe ving'ang'anizi kama ruba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo...
Katiba ya nchi gani na muungano ni Batili? Hata yeye kuwepo hapo hastahiki kwani hakuna Muungano. Ni kiini macho cha Laanatullahi Nyerere.

La muhimu ni warudishe nchi ya Zanzibar kule UN baadaye ikatafutwe ile nchi iliyokuwa ikiitwa Tanganyika ndio baada ya kuulizwa wananchi kama wanataka kuungana au la ndio waje na mashauri ya kuandika hiyo katiba.

Vinginevyo ni kuzidi kunya juu ya vinyesi.
 
sio Tanzania tu iliyo pigika kiuchumi bali Dunia nzima ipo ktk kipindi kigumu sana kiuchumi, ni ajabu kwa wanasiasa kudai mchakato wa katiba mpya ktk kipindi hiki kigumu cha kiuchumi bila hata kuwaonea huruma wananchi...
Tupo uchumi wa kati, tutembee kifua mbere!
 
Rais Samia alisema kuwa mambo hayo yasubiri sasa anashughulikia uchumi wa nchi.
Hebu tutafakari katika mambo yatakayozuwiya uchumi. pia tuangalie yale mambo amabayo ya tagharimu fedha za serikali.

Mikutano ya hadhara ya kisiasa
Jamabo hili kweli linaweza kuingilia kwa uchumi wa nchi?
kwa wale wajuzi watujulishe vipi .
Wanao gharimika katika hili ni vyama vya siasa. Serikali haitowi hata senti moja.
Kubwa ni Serikali kuhakikisha usalama wa raia zake kwa kutumia polisi, na hapo ndipo serikali itagahrimika. lakini ndio kazi ya Polisi.
Hata kama vyama vifidie hiyo gharama basi vitakuwa Tayari. Hapo hana point Mama

Kutangaza Tume huru, Mahakama huru na mengine
Hili lahitaji kauli tu.
Viongozi wa dola kama Takakuru, Usalam wataifa, Mahakama, Jeshi ,Polisi na vyombo vyote vya dola wasiwe wana CCM.
Jambo jingine ni kuwapa vyeo wanajeshi na wakuu wa polisi bila ya kustaafu vyeo vyawo . hili kwangu naona sisawa.

Katiba mpya
Hili litahitaji fedha kutoka serikalini ipo haja ya kusubiri kidogo lakini watu wapewe nafasi ya kulizungumza. Vyama vyasiasa kama wanataka kuelimisha watu juu ya hili wasizuwie wapate ruksa ya kwenda nchi nzima.
 
Tukiwaacha hawa wapiga dili wa dubai watuamulie namna ya kuendesha nchi tutarudi nyuma sana.

Issue ya katiba mpya sio issue ya wananchi wanyonge na wengi bali ni maslahi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa.

Mama muuza dagaa ambaye amekopeshwa kwenye kikoba au bodaboda anayetakiwa kupeleka 17000 kwa siku hawahitaji katiba mpya.
Zaidi katiba mpya kule kenya haijawaletea tija wakazi wa Kibera(hili ni somo)

Wapinzani hasa CDM wasituamulie mambo yasiyo na tija kwa maskini.

Tuletewe na tujadili hoja za kuujenga uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Tusiwe kasuku wa nchi za magharibi bali tufanye yetu kwa style yetu kukuza hali ya kiuchumi ya wananchi
 
Back
Top Bottom