Kukatika umeme Uwanja wa Mkapa: Serikali yawasimamisha watendaji kadhaa; yaomba radhi
Duh!
Nasikia kama nimepata mshtuko wa moyo wadau.

Yani mpaka hili la kukatika umeme viwanjani linahitaji uchunguzi??

Watu waunde kamati, walipwe posho, wale tozo za watu kisa kuchunguza viwanja???

Kwa kuficha mlengo wenu, mmeshindwa kusema uwanja wa taifa na badala yake mnataja viwanja vyote.


NCHI HII HAINA DIRA, NCHI HII IMEPOTEA KABISA


Chanzo cha habari: Star TV Tuongee asubuhi
 
Nitoe rai kwa serikali, timu ya uchunguzi ilipwe posho nzuri ili iweze kuleta ripoti yenye tija kwa maendeleo ya soka nchini😁
 
Wakina Karia ndio wanakaa kwenye Vikao vya kutoa gharama za Uwanja harafu mnakuja kuwalaumu watu wadogo wasio na maamuzi hii dhambi inaendelea kuwatafuna ,meneja wa Uwanja gani anaeweza kununua generator mpya au kukodisha hiyo kitu bila ya ruhusu ya hao wapiga hela kwa kutumia vikao...
Yanga akili hamna!

Karia na uwanja anahusikaje?Au unadhani uwanja ni wa TFF?

Hivi nyie utopolo akili zilienda wapi?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Screenshot_20230501-083929_Twitter.jpg

Waliosimamishwa ni Kaimu meneja wa uwanja ndg.Manyoni Juma Kapesa, muhandisi wa umeme ndg.TuswegeNikupala, Afisa uwanja ndg. Gordon Nsajigwa, na Gabriek Mwaswele.
 
wasiishie tu kuwasimamisha kazi ili watu wafuraho warekebishe matatizo hayo ya kujirudia rudia ili wengine watakapoingia wasibebeshwe mzigo wa lawama.

Ila bora wamekula mshahara wa mwezi April
 
huu uzembe upo kila mahali kipi hasa kinatustua kama sio unafiki …mara ngapi umeme unakatika ghafla maeneo nyeti kama Hospital na watu kupoteza maisha au kupata madhara wakiwa kwny vyumba vya upasuaji....
Ndio tulipofikia watz, mgonjwa akifariki kwa umeme kukatika wakati akifanyiwa upasuaji sio swala la msingi. Na wala hutasikia habari hiyo.

Ila kwa swala la mpira watu wanasimamishwa kazi.

Asante Tanzania.
 
Upo sahihi Mkuu sema umasikini upo kwenye Damu ndio maana hata tupate vip vitu vidogo vidogo vitaendelea kutusumbua miaka nenda rudi hapa tunajadili umeme wa Taa tuu sio wa kiwandani...
 
Wewe acha ujuaji,Uwanja wa serikali Karia anahususikaje?
Karia anatumia ule Uwanja anatakiwa ashauri na kujua wapi pana matatizo kama kweli mnadhani hatakiwi kujua kitu kuhusu uwanja ambao yeye kwenye Chama chake wanakitumia basi mna tatizo sana...
 
Back
Top Bottom