Kuna dogo kashinda Millioni 58 kwa kubeti. Mnashauri nini?

Kuna dogo kashinda Millioni 58 kwa kubeti. Mnashauri nini?

Kuna dogo huku mtaani kampiga meridian bet milion 58 halafu dogo tu miaka 29

Nimejionea kwa macho yangu betting inalipa.

Hapa anatuomba ushauri ma broo wake asijui tumpe ushauri gani

Wanajukwaa najua vichwa vyenu vina IQ huyu dogo awekeze kwenye nini hii pesa kabla hajaanza starehe maana imekuja ghafla sana?
Unaposema betting inalipa, niambie katika maisha yako, umewahi kuona watu wangapi wameshinda betting millioni 10? Kama hujawahi unawezaje kusema inalipa? unajua wangapi wanaliwa? Haya tufanye inalipa, cheza na wewe ndani ya miaka mitatu uone kama utawahi kushinda millioni tano kwa mara moja.
 
Hizo hela aziweke kwenye chumvi ya mawe siku 3. Siku ya 4 aweke UTT milioni 50. Hizo nyingine atambe nazo sasa afanye anachojiskia.

Kila mwezi kule UTT atakua anavuta laki4+
Si bora akanunue nyumba ya 50mils Kila mwezi anakula 500k Kwa kupangisha
 
Unapoambiwa elewa hela ya Kamari sio hela haikai fanya kitu cha maana ijishikize hapo, ukiweza msukumie mtu kiasi halafu kwa kipindi hiki bakia na kiasi kwenye 28 mpe mtu 25 akushikie chapu wewe baki na 3 tu hizo 25 usizichukue tena kisha pima upepo hizo 3 zinavyopukutika ndio utaelewa. Na zikikatika usizikimbilie 25 haraka ukazitaka unaenda kumrudishia Muhindi unakua km umerogwa uzirudishe zote. Ogopa sana.

Kwenye 58 mpe mtu 55 azizuie kwanza wewe baki na 3 kwanza. Hizo 55 fanya kitu cha maana kisichohamishika au kinachobeba thamani ya pesa mfano kiwanja, shamba, nyumba, nk

Mfano mimi nitakueleza sikuwahi kula hela nyingi ila nilikula hela kwa mkupuo wiki nzima, cha kwanza hela ya Kamari huoni dhambi kuitumie kuifanyia kitu chochote yaani ni hela ambayo inapukutika vibaya sana, unaweza ukaondoka asubuhi na million ukarudi na 50k yaan 950k zote umezitumia na haushangai hio ni siku 1.

Ukipiga mshindo mkubwa ku-stake high kwako inakua sio jambo la ajabu yaan ulikua unaweka labda 1000 tu ukipiga million za kutosha wewe kuweka million hata 20 kwa mchezo mmoja hauoni hatari sasa hio ni hatari sababu hizo 20 zikienda zimeesha hazirudi.
Last week nilipiga million 2.8.. bet pawa,leo nadaiwa elfu 30 kwa Mangi,nimebadilisha na njia.
 
Kuna dogo huku mtaani kampiga meridian bet milion 58 halafu dogo tu miaka 29

Nimejionea kwa macho yangu betting inalipa.

Hapa anatuomba ushauri ma broo wake asijui tumpe ushauri gani

Wanajukwaa najua vichwa vyenu vina IQ huyu dogo awekeze kwenye nini hii pesa kabla hajaanza starehe maana imekuja ghafla sana?
Kwani yeye alibet apate pesa afanyie Nini?
 
Atenge milioni moja kwanza atoe wenge la kushika pesa nyingi kwa kwenda kufanya starehe alizokuwa anafkiria. Narudia aende akafanye starehe atoe wenge.

Ule muda mfupi wa jinsi 1 milion itakavyopita kama upepo shwaaa itakuwa ni degree tosha ya financial management.
Baada ya hapo astafu kwa hiari maswala ya betting maana zile hela kwa uzoefu huwa zinakawaida ya kurudi njia ileile zilikotoka, unaweza kupata meidianbet kisha ukarudisha pmbet.

Ajitahidi kwa hatua za awali asinunue vitu vya gharama vya luxury ambavyo ukitaka kuuza unaweza kubeba na kumpelekea mtu ukarudii na pesa kama TV kubwa, ndugai, iPhone nk.

Naongea kama afisa ubashiri niliyebobea kwenye maswala ya betting and odds management upande wa financial match analysis (utani)
 
Kuna dogo huku mtaani kampiga meridian bet milion 58 halafu dogo tu miaka 29

Nimejionea kwa macho yangu betting inalipa.

Hapa anatuomba ushauri ma broo wake asijui tumpe ushauri gani

Wanajukwaa najua vichwa vyenu vina IQ huyu dogo awekeze kwenye nini hii pesa kabla hajaanza starehe maana imekuja ghafla sana?
Yeye mwenyewe kaomba ushauri au ww umejipendekeza kuomba ushauri wakati hela si yako?
 
Unaposema betting inalipa, niambie katika maisha yako, umewahi kuona watu wangapi wameshinda betting millioni 10? Kama hujawahi unawezaje kusema inalipa? unajua wangapi wanaliwa? Haya tufanye inalipa, cheza na wewe ndani ya miaka mitatu uone kama utawahi kushinda millioni tano kwa mara moja.
Kama haijakulipa ni wewe wenzio imewalipa biashara yeyote hamuwezi kufaidika wote
 
Mtoa mada linda marinda yako kwa wivu mkubwa sana,huyo jamaa aliyeshinda asije akaanza na wewe!
Maana inaonekana una tabia za kimbea sana.
 
Ajenge, kama wazo la biashara hana basi akalime
 
Back
Top Bottom