Kuna dogo kashinda Millioni 58 kwa kubeti. Mnashauri nini?

Unaposema betting inalipa, niambie katika maisha yako, umewahi kuona watu wangapi wameshinda betting millioni 10? Kama hujawahi unawezaje kusema inalipa? unajua wangapi wanaliwa? Haya tufanye inalipa, cheza na wewe ndani ya miaka mitatu uone kama utawahi kushinda millioni tano kwa mara moja.
 
Hizo hela aziweke kwenye chumvi ya mawe siku 3. Siku ya 4 aweke UTT milioni 50. Hizo nyingine atambe nazo sasa afanye anachojiskia.

Kila mwezi kule UTT atakua anavuta laki4+
Si bora akanunue nyumba ya 50mils Kila mwezi anakula 500k Kwa kupangisha
 
Last week nilipiga million 2.8.. bet pawa,leo nadaiwa elfu 30 kwa Mangi,nimebadilisha na njia.
 
Kwani yeye alibet apate pesa afanyie Nini?
 
Atenge milioni moja kwanza atoe wenge la kushika pesa nyingi kwa kwenda kufanya starehe alizokuwa anafkiria. Narudia aende akafanye starehe atoe wenge.

Ule muda mfupi wa jinsi 1 milion itakavyopita kama upepo shwaaa itakuwa ni degree tosha ya financial management.
Baada ya hapo astafu kwa hiari maswala ya betting maana zile hela kwa uzoefu huwa zinakawaida ya kurudi njia ileile zilikotoka, unaweza kupata meidianbet kisha ukarudisha pmbet.

Ajitahidi kwa hatua za awali asinunue vitu vya gharama vya luxury ambavyo ukitaka kuuza unaweza kubeba na kumpelekea mtu ukarudii na pesa kama TV kubwa, ndugai, iPhone nk.

Naongea kama afisa ubashiri niliyebobea kwenye maswala ya betting and odds management upande wa financial match analysis (utani)
 
Yeye mwenyewe kaomba ushauri au ww umejipendekeza kuomba ushauri wakati hela si yako?
 
Kama haijakulipa ni wewe wenzio imewalipa biashara yeyote hamuwezi kufaidika wote
 
Mtoa mada linda marinda yako kwa wivu mkubwa sana,huyo jamaa aliyeshinda asije akaanza na wewe!
Maana inaonekana una tabia za kimbea sana.
 
Ajenge, kama wazo la biashara hana basi akalime
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…