Kuna njia nyingine ya kupunguza uzito?

Umenizungumzia mimi kabisa😊
 
Unaonekana umridhika Sana na maisha, huumizi kichwa Wala kuwaza unapolala usiku
 
Ukitaka kufanikiwa zaidi acha vitu vifuatavyo
Ugari mweupe na kaka ni dona kula ukubwa wa ngumu wako na isiwe usiku.
Wali mweupe.
Ngano nyeupe, hapo Maandazi, chapati, tambi, keki nk.
Sukari na chumvi
Mafuta kwa vitu vya mikaango na yenye viungo vingi ili kupata radha.
Acha unywaji wa soda, pombe
Chipsi, hovyo hovyo ambazo hujaziandaa wewe kiafya.
Nyama zenye mafuta mengi punguza.
Mayai na kuku wa kisasa.
Badala yake
Usile chakula chochote wakati inapofikia saa kumi na mbili kamili hapo ndio mwisho wa kula.
Jitahid kula vyakula vya kuchemsha zaidi ukizingatia mboga za majani yenye mchanganyiko wa bamia, figiri, mchicha, sukuma wiki, hoho, karot hrf Tia limao na uhakikishe mchemsho huo usiive Sana.
Tumia juice yenye mchanganyiko wa pasioni, mchicha/sukuma wiki, tangawizi, parachichi, Unga wa mlonge kisha Tia asali mbichi.
Pendelea kula mchemsho wa Samaki, dagaa na mayai kienyeji 3 kwa siku.
Inapofaa kula mlo mmoja kwa siku mlo ulio kamilika na maji mengi.
Ukibahatika kupata muda wa mazoezi
Tafuta begi zuri Tia mchanga mgumu kg 30 unavaa begi Anza kutembea km 1/2 kila siku jion au asubuh au mara 2 kwa siku, ukifululiza wiki 2 wewe mwenyewe utaona mabadiriko kwenye wepesi wa mwili utashawishika kukimbia na begi. Ukiona umefika hatua hiyo ongeza kilo kwenye begi endelea kutembea ukipiga mwez mmoja, Anza kukimbia na kutembea taratibu haina haja kuingia jimu boss wangu.
Muda wa kupumzika tafuta kazi ya kufanya hata kufyeka au kulima majani,
Pendelea kutumia pia alovera chungu, kokwa ya parachichi, tangawizi, swaumu, asali mbichi, Unga mlonge saga juice piga japo kwa wiki mara 2.
NB. KIPIMO CHA ULAJI MBOVU NI PALE AMBAPO MTU ANAENDA HAJA KUBWA MARA ZAIDI YA MARA MOJA KWA SIKU. YAAN UKIONA KAMA MTU ANAPATA HAJA KUBWA MARA MOJA KWA SIKU HUYO YUPO VZR, ISIWE TU TATIZO LA KIAFYA.
 
umemaliza mzee...akifanya haya in 6 months anakuwa na kilo 70
 
Kila siku hakikisha unatembea dakika 20 had nusu saa
Punguza wanga kabisa achana na ma supu na chapati mi soda fanya diet au Anza na kula mlo mmoja Kwa siku
 
Kachukue mkopo bank au oya
 
Unakula chapati na juice za maparachichi sahau kuhusu kupungua. Uzito umejificha kwenye vitu vitamu
 
Ulitumia njia gani hapo awali?
 
Akiendeleza ubishi+uvivu unene utabaki pale pale
Halafu wewe sio mvivu kwani? Ndio maana nikasema nachukia sana mimi mtu kuniona fala, mimi sio mvivu kwa taarifa yako elewa hivyo kua bonge sio ishara ya uvivu
 
Bonge kama bonge. Lol.

Kuna baba mmoja niliwahi kumuona amekaa kwenye kiti ile kutaka kuamka alijivuta zaidi ya mara kumi baadae ndo akainuka kuanzia pale nikajikuta tu nikiwaona vibonge huwa nawaonea huruma mbaya.

Poleni jamani mana mnateseka hasaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…