Kuna staff mwenzangu kaenda kunisemea kwa Boss kuwa ninatumia sana kilevi na kutoa maneno machafu kitu ambacho sio kweli

Kuna staff mwenzangu kaenda kunisemea kwa Boss kuwa ninatumia sana kilevi na kutoa maneno machafu kitu ambacho sio kweli

Wakuu habari…

Niende moja kwa moja kwenye mada mimi ni mfanyakazi Halmashauri fulani ila sina muda sana kazini ni kama miezi sita kwa sasa tangu nianze kazi.

Sasa ikohivi kuna staff mwenzangu kaenda kunisemea kwa Boss kuwa ninatumia sana kilevi na kutoa maneno machafu kitu ambacho sio kweli nilikuwa nikinywa au kulewa ni story nyingi na utani kwa sana ila mtu huyo kaenda kusema ndivyo sivyo

Kuhusiana na hilo nimejaribu kudadisi kidogo nakugundua ni dada mmoja mnafki mnafki pale kazini kwanamna moja ama nyingine ndie aliyehusika na kutoa maneno hayo kwa Boss

Hivyo leo niliitwa nakuulizwa lakini niliona nisiwe mbishi ili nisikuze jambo mana tulizungumza kirafiki kabisa na pia sikutaka kujua kuwa ninani aliepeleka maneno ya hivyo kwa Boss huku akidai nikilewa natukana hovyo na kujisifu kuwa hakuna wakunifanya lolote (Yote hayo ni chuki na hakukuwa na ukweli wowote)

Hivyo tulikubaliana nitabadilika na sitorudia tena makosa niliyoyafanya na kumuahidi sitorudia tena kunywa pombe.

Wakuu naombeni ushauri maana tayari naishi kwa wasiwasi sana sina amani na sijui ninamna gani nitaweza kuishi na watu wanamna hii kazini

Ahsanteni nimeandika huku nimepaniki mno mnisamehe ndugu zangu nahitaji ushauri wenu.
we mwenyewe ni jinsia gani?
kama ni Ke basi angalia iwapo kuna namna imeingilia makoloni ya watu hapo kazini kwako.​
Kama ni Me basi angalia vizuri interest zako kwa wadada wa hapo kazini kwako...huenda huyo dada anakutaka na wewe unajifanya mbukina faso, au umetongoza rafiki yake (Huyo dada) while anaye kutaka ni mwingine.​
 
Nenda kamroge awe mlevi na yeye halafu muanze kulewa na kutukana wote, hapo kutakuwa hakuna wa kumsemea mwenzie 😀 😀
 
Ulanzi tunao na tunatamba nao, karibu Nyumbi bombiii, huku uko wa kushato, afu nagema mwenyewe ule ulio koli koli, kunoga Lyo lyo lyo.
😂😂😂😂😂
Like serious dada ? Ikiwa uko serious kweli jua nimekupenda bure na sasa wewe ni rafiki yangu wa hiyari ,nikija Dar wewe ndiye utanipa machimbo ya ulanzi .
Ila usiwe ule unaochanganywa na maji alafu ukaleta tafrani tumboni
 
Ulanzi tunao na tunatamba nao, karibu Nyumbi bombiii, huku uko wa kushato, afu nagema mwenyewe ule ulio koli koli, kunoga Lyo lyo lyo.
😂😂😂😂😂
Palepale pa Mfaranyaki bimbii,nyumbii!
 
Haya mambo ni hatari sana .
Mwanzake niliwahi andikishwa barua ambayo boss alisema niitetee pombe ikiwa mimi ndiye mkorofi au pombe ndiyo chanzo .

Nilipata tabu sana kuiandika ile barua kusema mimi ndiye mkorofi sio kweli mimi ni mpole sana ,kusema pombe ndiyo chanzo nikaogopa hawakawii kuwatisha watu wa bar zote around kazini kuwa ukikutwa unaniuzia bia basi utakuwa umeitafuta hasara yaani kaka haya mambo yaone kama yalivyo ila kikubwa hakuna magumu yasiyopita na hili lilipita na sasa ni mshindi miongoni mwa washindi
Aisee napitia wakati mgumu sana ndugu yangu
 
Like serious dada ? Ikiwa uko serious kweli jua nimekupenda bure na sasa wewe ni rafiki yangu wa hiyari ,nikija Dar wewe ndiye utanipa machimbo ya ulanzi .
Ila usiwe ule unaochanganywa na maji alafu ukaleta tafrani tumboni
Ulanzi unachanganywa na maji ule mkangafuu, maana unakua unachuchuta kdg, but unaweka na sukari kdg.

Ila mie huu ni wenyewe OG, nautoa halisi ukiwa kwenye Mbeta yake, yaan ni kujileweaa tyuuh.
Usijari karibu Ulanzii mkuu.
 
we mwenyewe ni jinsia gani?
kama ni Ke basi angalia iwapo kuna namna imeingilia makoloni ya watu hapo kazini kwako.​
Kama ni Me basi angalia vizuri interest zako kwa wadada wa hapo kazini kwako...huenda huyo dada anakutaka na wewe unajifanya mbukina faso, au umetongoza rafiki yake (Huyo dada) while anaye kutaka ni mwingine.​
Mwanzo alitaka kuleta mazoea ya kimahusiano nikamtolea nje sa sikujua wenda ndio chanzo au laa
 
Back
Top Bottom