DOKEZO Kuna wakimbizi wengi toka Malawi maeneo ya Mwananyamala

DOKEZO Kuna wakimbizi wengi toka Malawi maeneo ya Mwananyamala

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Uswazi kote wamalawi wapo.

Ukipiga nao stori wanasema Tz tuna vitu vingi bei rahisi ila kwao ni bei ya juu mno. Mfano kwa mtaa wa Mwananyamala wana kama kampuni yao inasafirisha vitu kutoka Tz kwenda Malawi utakuta wanapeleka magodoro, ndoo za plastiki, nguo na vitu kama hivyo.

Wanasema kwamba sababu pekee wao huvaa nguo hazieleweki ni kwakua huko kwao nguo ni bei ghali so wakifika hapa wanakuta nguo ni bei ya kawaida na huchukua zile za bei ya kawaida kabisa na kujikuta wanavaa mno midosho.

Hata hivyo competency ya uhamiaji is very questionable. Wakitia timu sehemu ni wawe wameshtuliwa ili kuja kuchukua hela.
Uhamiaji wanalipwa na hawa jamaa itakuwa wanapewa "hush money". Tunahitaji kuboresha sheria ya kudeal na rushwa vema ili tuweze kudhibiti watendaji wala rushwa na kuwatokomeza.
 
Ni sehemu gani nimeandika kwa kupaniki zaidi ya kueleza hali halisi kati ya Tanzania na Malawi.
Kwa anayejua historia ya Tanganyika na Malawi kabla ya uhuru chini ya mwingereza hashangai uwepo wa wamalawi hapa nchini kama ilivyokuwa wanyakyusa kusoma shule nchini Malawi bila kuulizwa na mtu.
Sasa sisi tunaongea habari za wamalawi kujaa Mwenge wewe unazungumzia habari za Kyela na Malawi?
Nini maana ya kuitwa taifa?
Nini maana ya kuwa na mipaka?
Nini maana ya watu kuitwa wahamiaji haramu?
 
Unafikri uhamiaji hawajui? Au ukienda USA au UK unadhani hutawakuta wahamiaji ambao hawana vibali? Kila taarifa na habari zao zipo sana tu sema jamaa ni watulivu hawana vurugu,udokozi, uharamu wala uhalifu ndomana unaona wanaachwa.. ila siku usikie wamefanya uhalifu ndo utaijua uhamiaji vzuri
 
Mwananyamala,tandale,msasani,kawe,mikocheni malawians are on top and they just relax like they are in their homeland they drunk bananas (beer) too much
Wamalawi hawana shida na mtu Tanzania

Raia wakorofi ni wa Burundi,Rwanda na na Kenya na Kongo .Wajeuri na ujuaji na silaha nje nje

Ndio.maana nchi iko makini na strict sana

Wamalawi,wazambia,na wa msumbiji watanzania tunaiiva nao sana hawans shida na mtu na wako wengi na uhamiaji wanawajua vizuri.Hawana madhara kwa mtu binafsi wala nchi huendesha maisha yao vizuri tu bila shida na wenyeji na wenyeji wa maeneo husika wanawajua kabisa kuwa ni wageni wa kutoka hizo nchi.Lakini hufurahi sana kuwa nao mitaani ni watu wema wasio na tatito lolote na mtu awaye yeyote
 
Unahangaika na maskini mwenzako asiye na hatia ambaye amekuja kutafuta ugali na kupunguza umaskini uliokithiri kisa mpaka uliwekewa na mzungu ukasahau hao ndiyo walioipa Uhuru Zanzibar .Aman Abeid Karume. Mbona haujadili hao Wachina na Wahindi waliokuzunguka hapo ulipo na muda wote wanajificha ndani. Acha umbumbumbu .
Popote umuonapo Mtu mweusi ujue tu ni Mtumwa Mwenzako anahangaika kupata chakula tu.Maana elimu aliyopewa ya kitumwa tu wala haina Msaada kwa jamii yetu.
Acha chuki zidi ya Maskini mwenzako
 
Habari,

Nimejaribu sana kufuatilia na kugundua sana sehemu ya Mwananyamala kumejaa sana wakimbizi au malawi au wamalawi wengi wano ishi bila ya kua na vibari.

Sijajua Uhamiaji wanafanya kazi gani. Maana imekuwa kawaida sana kukuta wamalawi wakiwa wengi sehemu hiyo pamoja na Mbezi Beach wakiwa kama wafanyakazi wa ndani.

Sijajua shida ni nini ila naomba serikali ifanye jitihada. Maana nipo na rafiki yangu wa kike mmalawi.
Amekudanganya huyo. Hao siyo wakimbizi bali ni wahamiaji na hilo lipo tangu miaka ya 2007.
Wengi walikuja kwa sababu za kibiashara Kariakoo, baadaye wakaanza kufanya kazi za kama house girls/boys, Shamba boys hasa kulima mbogamboga, pia biashara nyingi Kariakoo.
Kutokana na uaminifu wao na uwezo wao wa kazi, wabongo wakawa wanawatumia kupata cheap labours wanaoaminika kutoka nchini kwao, na hapo ndiyo wakaanza kumiminika kwa wingi huku wengine wakijiita wanyasa hali iliyopelekea wanyasa kuanza kuwa kabila maarufu kumbe ni sababu ya Malawi.
 
Nenda kwao, bila vibari vya uhamiaji, ukauone huo undugu.
Nahonyo kwanza andika vibali na si vibari, hao kuja kwetu ina maana kuna mambo hayapo sawa kwao ndiyo maana wanatafuta fursa Bongo. Na huu ni uthibitisho kuwa Bongo kuna neema ambayo sisi wenyewe hatuijui. Samaki hajui thamani ya maji mpaka atakapotolewa nje ya maji.
 
Ni sehemu gani nimeandika kwa kupaniki zaidi ya kueleza hali halisi kati ya Tanzania na Malawi.
Kwa anayejua historia ya Tanganyika na Malawi kabla ya uhuru chini ya mwingereza hashangai uwepo wa wamalawi hapa nchini kama ilivyokuwa wanyakyusa kusoma shule nchini Malawi bila kuulizwa na mtu.
Chirwa ni jina la Kimalawi
 
Ila hawa ni wachapakazi mno
Alafu wasafi sana pia yani ukimuajiri kazi ya ndani humtumi kitu anajituma mwenyewe unlike hawa wenzetu wa TZ
 
Nahonyo kwanza andika vibali na si vibari, hao kuja kwetu ina maana kuna mambo hayapo sawa kwao ndiyo maana wanatafuta fursa Bongo. Na huu ni uthibitisho kuwa Bongo kuna neema ambayo sisi wenyewe hatuijui. Samaki hajui thamani ya maji mpaka atakapotolewa nje ya maji.
Sijakuelewa kwahiyo kuna vitu wanavifuata ambavyo kwao havipo, waachwe wahamie nchini, bila utaratibu wa uhamiaji.
 
hata malawi kuna wanyakyusa wengi huko huenda ni wengi kuliko hata wamalawi waliopo tanzania hadi kuna mitaa ina wanyakyusa karibu wote , hilo lipo pia upande wa zambaia nazani tuawache tu wajitaftie so long as hawavunji sheria na hawafanyi makosa ya jinai
 
Wamalawi hawana shida kabisa waacheni watajitafutie ridhiki,mbona watanzania wengi wapo kwao wanafanya biashara bila vibali na serikali yao inalitambua kabisa lakini hawana noma
 
Wa Malawi wapo wengi sana Dar es salaam kila mahali, Boko wamejaa, na ni wachapa kazi kweli kweli, kwa ujira wa kawaida.

Sasa sijui wamekukosea nini? Maana hawazuru mtu, na pia unajuaje hawana vibali wote? Una uhakika gani?

Ujaona wazungu wengi maeneo ya Masaki? Mbona hao hujawataja? Mpaka umewasumbua wa Malawi wa watu?

Mbona wa Africa mnachukiana? Kwa hiyo ukiwaona wazungu unajua wote wana vibali ila wa Africa wenzako hawana?
ingia na wewe kwao afu uongee maneno haya , hizi taratibu za kimataifa ndugu watu unapoingia nchi ya watu uwe na vibari halali sababu bajeti yetu ni kwaajiri ya TZ tu hawa wanatumia maji, madawa,umeme huduma zingine za kijamii za watanzania wakati na kwao kuna bajeti yao sijui unaelewa hapo hatujaongelea swala la usalama
 
Kwahiyo Castr: ni mzungu, Masaki ni mzaramo, Mitimingi na Kazimoto ni watanzania, acha hizo mbona wapo Chirwa wasomali na hao niliokuandikia ni wajapani.
General rule ni niliyoisema

Exceptions za general rule ni ulizozisema.

But in its basic Chirwa ni Mmalawi
 
Sijakuelewa kwahiyo kuna vitu wanavifuata ambavyo kwao havipo, waachwe wahamie nchini, bila utaratibu wa uhamiaji.
Bandiko la mleta mada lipo kizushi sana, kwani wakihamia kuna tatizo gani? Wapewe msaada wa kufuata utaratibu wa uhamiaji, kwani tayari wapo nchini na sheria ya uhamiaji ichukue mkondo wake ikiwa kama watatoleshwa faini au watapewa vibali au hata uraia ikiwa hawatakuwa na historia ya uhalifu. Hii ni fursa ya nguvu kazi iliyotayari nchini kama si wahalifu ni watafutaji wa riziki hakuna haja ya kuwadhalilisha waafrika wenzetu, kumbuka kuwa pengine hata wazee wako huko nyuma walikuja sehemu hii ya nchi kwa kutafuta maisha mazuri.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-08-24 at 11.55.31.mp4
    18.8 MB
Back
Top Bottom