Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
sio mimi boss, unakosea unvyojibu kama vile mimi ndio nashawishika na hao wanasiasa..Hapa nazungumzia wananchi walivyo, wananchi wengi uelewa wao ni mdogo kuhusu kuchanganua utapeli na ukweliNi hivi boss, hao wanasiasa wanaweza kufanya watakacho na kwenda watakako, ila pia hawana haki ya kupata imani yetu pindi wanapokwenda tofauti na matakwa yetu. Kama ww unataka kuvumilia wanachotaka wanasiasa wasio na misimamo, hiyo ni haki yako. Huyo Lowassa unayemtaja sio kila mtu alikubaliana na uhuni ule, na nina hakika upuuzi kama ule hautakaa urudiwe.
Tunasema ccm haina ushawishi sio kwamba haina kabisa, bali haina ushawishi iliokuwa nao huko mwanzo, na haina uwezo wa kuwa nao tena zaidi ya kutegemea vyombo vya dola. Na
huko kushinda sio kwa ushawishi bali ni kwa nafasi yao ya kumiliki dola. Hivi leo ccm ikitumia huo ushawishi unaotaka tuamini inao, inahitajika chaguzi mbili tu kuiweka ccm pembeni. Hii sio rocket science bali ni uhalisia wa kibinadamu. Ufahamu CCM sio chama cha kizazi hiki bali ni cha kizazi kilichopita, ndio maana inatumia nguvu kubwa kubaki madarakani kuliko ushawishi.
Kuitisha maandamano sio lazima ufanikiwe mara moja kulingana na nature ya watu ilivyo. Ilitakiwa kusiwe na vitisho kisha uje na ushuhuda kuwwa watu wamegoma kujitokeza. Ila kupanda mbegu ya kuandamana iko siku itazaa matunda. Huko Egypt, Sudan, Zimbabwe nk walitawaliwa kibabe zaidi ya miaka 30 wakiwa wanaogopa kuandamana, ila ilifika siku hofu iliondoka na leo tawala zile za wababe ni historia.
Hiyo join the chain inasuasua maana wachangiaji ni watu waliopigika na hawana uwezo wa kutoa, isitoshe haikuwa deni bali ni jambo la hiyari. Kodi yenyewe tu ya nchi watu wanadaiwa kisheria inakuwa mbinde kutoa, ndio itakuwa huo mchango wa hiyari?
Mfano hilo la Lowassa, baada ya Chadema kumsimamisha Lowassa ikawa ndio uchaguzi wenye ushindani zaidi kwa CCM ambapo walipata kura nyingi na wabunge wengi zaidi, japo Lowassa anafahamika ni fisadi na hakuwa hata na sera za maana, hili linakupa picha akili za wananchi zipo vipi kuhusu kujua uwongo wa wanasiasa, na sio siasa tu, hata kwenye dini,au mpira huko
Pointi hapa sio kutetea Chadema kuchukua watu kama Lowassa , ila ni kuwa pragmatic ama utaishia tu kudumaa, mtu kama hana historia chafu sana, na alikuwa mwanachama mzuri mwenye ushawishi tu eneo alilokuwepo kabla ya kuhama, kumpokea haina ubaya, ukizingatia na siasa za awamu ya 5 zilivyokuwa...Sasa mkitaka watu pure mtaishia kuwa kakikundi kadogo tu ka mtandaoni