Kurejea kwa Elia F. Michael, CHADEMA iwe makini

Kurejea kwa Elia F. Michael, CHADEMA iwe makini

Lazima arudi huko
Kwani atafanya shuguli
Gani
Washazoea kuishi kwa blah blah

Ova
 
Kabisa mkuu. Kwa nionavyo mupo watu mnakipigania chama hata iwe Magufuli au bashite hamkuogopa, bado mkabaki mmesimama kwenye mstari kwa ajili ya uhai wa chama. Japo sijajua wewe ni Mnyika au ni nani kwenye chama. Ila unastahiri pongezi mkuu
Nashukuru ila mimi siyo Mnyika , naitwa Erythrocyte natokea Kyela , Mbeya
 
Cdm hakuna watu wakati alikuwa cdm akaahidiwa na shetani kupewa fahari ya dunia hii? Saa hii shetani yuko ahera madukani ameamua mwenyewe kurudi chama la wana, maana ameona huko cha la wazee hakuna vibe kabisa zaidi ya kutegemea vyombo vya dola.
sasa nyie ndiyo mjione wapumbavu yaani mtu mwenye tamaa za aina hiyo mnakubali awaendeshe kishenzi namna hiyo? hicho siyo chama ni saccos ya mbowe akiamua ameamua hakuna mtu wa kudindisha hapo
 
Hawa vijana waliondoka CHADEMA wenyewe kwa kununuliwa baada ya kushawishiwa , huku wengine wakihamia ccm baada ya vitisho, yeyote anayeogopa vitisho vya watawala hafai kwenye siasa za upinzani.

Ninatambua msululu wa wasaliti wanaoomba kurejea CHADEMA, wakiwemo Wakuu wa Wilaya wawili ambao wako tayari kuachia vyeo na kurudi walikotoka (Haifamiki walichokisahau), Bali naitahadharisha sana Chadema kuwa makini inapowapokea watu hawa , ni kweli kwamba mtaji wa chama cha siasa ni watu, Lakini ni lazima WATU HAO WAWE BINADAMU.

View attachment 2176348
Karibuni CDM hatuna chuki wala kinyongo.
 
mtoto wa Alipipi kasyupa
Hapana , Kasyupa kwao ni Maeneo ya Mundamba , ni Talatala au Mwaya au ilopa , mimi kwetu ni Kajunjumele barabara ya kwenda Itungi Port , sina uhusiano wowote wa Kindugu na Mzee Kasyupa , uhusiano wetu ni Chadema tu
 
Chadema mkitegemea hizi siasa zenye uaminifu kama kwenye ndoa, mtasubiri sana....Wanasiasa wote wanaongozwa kwa maslahi kwanza, itikadi ndio inafuata, mwanasiasa hatajiunga na chama kama akiona hiki chama hakina possibility ya kumpa ushindi, hata kama ndio chenye itikadi yake.. Chadema wenyewe waliona kulijua hilo kipindi kile walipomchukua Lowassa na kumpa agombee urais badala ya Slaa

Na CCM bado ina ushawishi mkubwa tu, inatumia vyombo na taaisi karibu zote kufanya propaganda zake na wananchi wengi bado wanashawishika.

na hapa mnaposema CCM haina kabisa ushawishi ndipo Chadema mnafanya kosa kubwa, la kui underestimate CCM, mnajioa mna ushawishi sana na CCM haina ushawishi, matokeoa yake mkienda kwenye uchaguzi mnapigwa, mkiitisha maandamano hakuna anayekuja, mkiaznisha join the chain ndio hiyo inasuasua... Jengeni chama kwa kuvutia watu wote, wawe moderate au msimamo mkali, mkitaka extremists tu, mtakuwa nao kule Twitter na JF, sio mtaani

Ni hivi boss, hao wanasiasa wanaweza kufanya watakacho na kwenda watakako, ila pia hawana haki ya kupata imani yetu pindi wanapokwenda tofauti na matakwa yetu. Kama ww unataka kuvumilia wanachotaka wanasiasa wasio na misimamo, hiyo ni haki yako. Huyo Lowassa unayemtaja sio kila mtu alikubaliana na uhuni ule, na nina hakika upuuzi kama ule hautakaa urudiwe.

Tunasema ccm haina ushawishi sio kwamba haina kabisa, bali haina ushawishi iliokuwa nao huko mwanzo, na haina uwezo wa kuwa nao tena zaidi ya kutegemea vyombo vya dola. Na
huko kushinda sio kwa ushawishi bali ni kwa nafasi yao ya kumiliki dola. Hivi leo ccm ikitumia huo ushawishi unaotaka tuamini inao, inahitajika chaguzi mbili tu kuiweka ccm pembeni. Hii sio rocket science bali ni uhalisia wa kibinadamu. Ufahamu CCM sio chama cha kizazi hiki bali ni cha kizazi kilichopita, ndio maana inatumia nguvu kubwa kubaki madarakani kuliko ushawishi.

Kuitisha maandamano sio lazima ufanikiwe mara moja kulingana na nature ya watu ilivyo. Ilitakiwa kusiwe na vitisho kisha uje na ushuhuda kuwwa watu wamegoma kujitokeza. Ila kupanda mbegu ya kuandamana iko siku itazaa matunda. Huko Egypt, Sudan, Zimbabwe nk walitawaliwa kibabe zaidi ya miaka 30 wakiwa wanaogopa kuandamana, ila ilifika siku hofu iliondoka na leo tawala zile za wababe ni historia.

Hiyo join the chain inasuasua maana wachangiaji ni watu waliopigika na hawana uwezo wa kutoa, isitoshe haikuwa deni bali ni jambo la hiyari. Kodi yenyewe tu ya nchi watu wanadaiwa kisheria inakuwa mbinde kutoa, ndio itakuwa huo mchango wa hiyari?
 
sasa nyie ndiyo mjione wapumbavu yaani mtu mwenye tamaa za aina hiyo mnakubali awaendeshe kishenzi namna hiyo? hicho siyo chama ni saccos ya mbowe akiamua ameamua hakuna mtu wa kudindisha hapo

Tamaa au kusalimisha usalama wake? Hata hivyo nani anaunga mkono yeye kupewa madaraka? Hilo neno la Sacco's ya Mbowe ww unalitamka kwa kufuata mkumbo wala huna ujualo. Huyo Mbowe alitaka cdm ishiriki mkutano wa TCD unaofanyika hivi leo, mbona kwenye kikao watu wamemkatalia na amekaa kwa kutulia?

Labda ww ujiulize ccm imefakaje leo kwa kina Kinana, Makamba, Membe nk wakati waliitwa wasaliti wa nchi, na wale wazalendo uchwara wa sukuma gang wanalambishwa mchanga?
 
Ahaa, wewe una julikana kuwa una chuki na hayati bila sababau za msingi.

Nina sababu za kutosha za chuki dhidi yake, ila ww kwakuwa alikuwa mjomba wako huwezi kuona msingi wake. Kwa hiyo umesema Elia ni boya maana ww una chuki naye zisizo za msingi?
 
Aachwe arejee lakini asipewe nafasi yoyote ya uongozi. Yeye kazi yake iwe kubeba briefcase za viongozi.
Hapa ndipo upinzani mnapojidanganya
Huyu si miongoni mwenu
Ukisoma alichoandika utagundua jambo
Ni mnafiki mchafuzi mharibifu
* Akae mbali na viongozi
Eti abebe briefcase ! Huyu ni wa kufanana na akina musiba
Endeleeni kujidanganya
Arudi kufanya nini? Akaanzishe chama chake mrundi huyu
 
Back
Top Bottom