Kurejea kwa Elia F. Michael, CHADEMA iwe makini

sio mimi boss, unakosea unvyojibu kama vile mimi ndio nashawishika na hao wanasiasa..Hapa nazungumzia wananchi walivyo, wananchi wengi uelewa wao ni mdogo kuhusu kuchanganua utapeli na ukweli

Mfano hilo la Lowassa, baada ya Chadema kumsimamisha Lowassa ikawa ndio uchaguzi wenye ushindani zaidi kwa CCM ambapo walipata kura nyingi na wabunge wengi zaidi, japo Lowassa anafahamika ni fisadi na hakuwa hata na sera za maana, hili linakupa picha akili za wananchi zipo vipi kuhusu kujua uwongo wa wanasiasa, na sio siasa tu, hata kwenye dini,au mpira huko

Pointi hapa sio kutetea Chadema kuchukua watu kama Lowassa , ila ni kuwa pragmatic ama utaishia tu kudumaa, mtu kama hana historia chafu sana, na alikuwa mwanachama mzuri mwenye ushawishi tu eneo alilokuwepo kabla ya kuhama, kumpokea haina ubaya, ukizingatia na siasa za awamu ya 5 zilivyokuwa...Sasa mkitaka watu pure mtaishia kuwa kakikundi kadogo tu ka mtandaoni
 
Kosa kubwa Sana chadema kupokea watu aina hii. Bora ya hata covid-19 ni bora wapokelewe na sio hao waunga juhudi
 

Arudi ila cheo kwa sasa hapana, kuanzisha chama ni utashi wake. Kama ni wabaya hata sasa ndani ya chama wapo. Huu ni mtazamo wangu, I stand to be corrected.
 
Wapokeeni....

Acheni siasa za chuki na hasama....

Vijana wenu hao....wapokeeni wawapigie kazi.......

#Siempre JMT 🙏
 

Ni kweli wananchi hawana uelewa, ila sio kwa wingi huo unaousema ww. Huyo Lowassa hakupata kura kama yeye, bali alipata kura nyingi maana alikuwa cdm, na kwa taarifa yako cdm wangemsimamisha Dr. Slaa wangepata kura zaidi. Isitoshe Lowassa hakupokelewa na kupewa nafasi ya kugombea na wafuasi wa cdm, bali genge dogo la viongozi kwa maslahi yao binafsi. Juu ya wananchi kuchanganua utapeli tumeona wananchi kukifanyika midahalo na mikutano mbalimbali hupata uelewa wa kutosha. Kama 2010-2015 walielewa ina maana sasa hivi ndio wamekuwa wajinga?

Sina popote ninapokataa mtu kupokelewa regardless aliondoka vipi, ila ninachokataa ni mtu kurejea na kupewa tena cheo au nafasi ya kugombea. Anaweza kukaa nje ya nafasi za uongozi sio chini ya miaka mitano chini ya uangalizi kabla ya kuaminiwa tena.
 
Haka kanyigu kabishi sana.
 
Tatizo lako unasiasa za chuki, wewe unavyosema walinunuliwa, kutishiwa au kushawishiwa haya nambie, sasa hivi wanarudi chadema je wamefika bei? mewashawishi au mmewatisha? Mwache mtu atumie uhuru wake na hiyo ndio Democracia.
 
Kiukweli huyu kijana siyo kwamba alihama chama kwa kupenda,zipo tetesi kuwa alitishwa! Wakati anashiriki uchaguzi wa marudio jimbo la Buyungu kufuatia kifo cha Bilago MP alishinda lakini matokeo yakabadilishwa harafu akalazimishwa kuyakubali.
Kwa muktada huo mimi nadhani kijana aruhusiwe kurudi kundini bila masharti.
 
Arudi ila cheo kwa sasa hapana, kuanzisha chama ni utashi wake. Kama ni wabaya hata sasa ndani ya chama wapo. Huu ni mtazamo wangu, I stand to be corrected.
Asirudi
Hawa wapo kimaslahi zaidi
Hawana uchungu na Taifa
Mnawapokea wa nini?
Biblia inasema ' mtatangatanga hata lini?
Chagua kuwa moto au vuguvugu

The guy anaonekana kabisa yupo kwa mission maalum
Action speaks louder
Hamuoni tunachoona

Asipewe hata hii promo
Ni trash

Mtayakumbuka maneno haya
Walikuja akina Sumaye wapo wapi
Kosa si kufanya kosa kosa ni kurudia kosa
 

Tunaheshimu mawazo yako, ila Sumaye hakuwa mwanacdm bali alikuwa mzee mwanaccm aliyeondoka ccm kwa kuzira na kupata hifadhi ya muda mfupi. Ni tofauti na Elia ambaye ni kijana na alikuwa mwanacdm. Cheo siafiki apewe, ila kubeba briefcase za viongozi na kupanga viti wakati wa mikutano, ni sehemu ya kitubio chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…