Kusema Majaji ni maCCM ndiyo kauli mbaya kuliko zote kwenye kesi ya Mh. Lissu


Mpuuzi wewe, unaongea nonsense tu.
 
Kesi nyingi za wapinzani huwa zinafutwa kwasababu ya kudumisha mshikamano wa kitaifa tu, lakini sio kwamba zinafutwa au kuondolewa mahakamani kwakuwa walibambikiwa. Kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu huwa wanavunja sheria kweli.

Uongooooo!!!
 
Sasa uongo ni upi hapo men?. Ili uwe judge lazima uteuliwe na Raisi lazima file lako lipitiwe kama ni kada mtiifu
 
CCM hamjawahi kushinda uchaguzi ni wizi tuu na kutumia mfano wa menu kama Trump unaonyesha ulivyo buyu huko kichwani
 
Kwani uongo , kwamba majaji sio maccm?

Nikuulize wewe 1991 kurudi nyuma chuoni ukiingia huulizwi kadi ya CCM?.

Baada ya 1991 ni majaji wangapi wa umri wa sawa na Lissu walirejesha kadi za CCM na kufanya declaration kuwa sio wanachama.

Mlezi wa mahakama kimkoa ni mkuu wa mkoa hii alianzisha Magufuli.

Mkuu wa mkoa ni mteule wa mwenyekiti wa CCM na pia ni kada wa CCM hivyo anaweza kupindisha maamuzi aidha kwa simu ya boss wake au kwa kuona chama chake kinaguswa maslahi yake.
 
Majaji ni maccm kwani hapo kuna uhaini?
 
Apeleke mahakamani kama ameona kuna ukiukwaji umefanywa. Utawala wa sheria unataka hivyo
 
Mpigie simu ROSTAN Muulize jinsi simu zinavyofanya maamuzi atakuambia, umeshahu kesi ya Mwabukusi kule Mbeya kuhusu dipiwedi?
Rostam ni nani hadi awe rejeo lako? kwangu mm ni raia kama raia mwingine, hiyo haiwezi kuhalalisha kutoa a general statement ya majaji ni maCCM. Lengo la statement hii kuwafanya watu watafasiri kwa namna watakavyoona wao; wako ambao wataacha kwenda mahakamani kudai haki zao na wako ambao watajichukulia sheria mikononi mwao kwa waliowakosea na kwa wanasiasa na wafuasi wao wako ambao watataka kuiondoa serikali ya CCM na CCM na majiji: hivyo kumuondoa Rais, na hivyo basi kufanya uhaini!!!.
 
Kwenye katiba ni ibara gani inasema jaji lazima awe na kadi ya CCM? Lakini Lissu akiwa Rais (Mungu apishie mbali) unadhani Jaji Mkuu atakuwa mwanachama wa chama gani? Ni ibara gani inasema mtu akishakuwa jaji haruhusiwi kuwa Rais wa tanzania?
 
Mimi nilikuwa mkosoaji mkubwa wa waliomfanya Lissu awe mkimbizi. Kwa hali hii sasa ndio najua walimaanisha nini. Lissu hakubali kila kitu, anakosoa kila kitu, hapendi kila kitu, analalamikia kila kitu na anapinga kila kitu. Hakuna mzazi, kiongozi, ndugu au rafiki atapenda hilo. Anapinga bila kutoa njia mbadala. Njia mbadala kwake ni yeye kwenda Ikulu!! Nyoooooo!!

Nadhani hata Rais Samia anajilaumu sana sasa hivi kwa kujifanya yeye anajua kuliko magufuli.
 

..mahakama zetu zimeyumba sana miaka ya karibuni.

..na kuyumba huko kumesababishwa na kutumika vibaya na watawala wa Ccm.

..kinachopaswa kufanywa ni watawala, na mahakama, KUJISAHIHISHA.
 
Kwenye katiba ni ibara gani inasema jaji lazima awe na kadi ya CCM? Lakini Lissu akiwa Rais (Mungu apishie mbali) unadhani Jaji Mkuu atakuwa mwanachama wa chama gani? Ni ibara gani inasema mtu akishakuwa jaji haruhusiwi kuwa Rais wa tanzania?


Typical akili za kiCCM zero reasoning mnaficha kichwa kwenye mchanga mnaacha mwili juu mkifikiri hamuonekani.

Mimi sijaongelea katiba popote nimeeleza mfumo wa chama kimoja alioasisi Nyerere 1965 hadi 1991 , mtu alipokua akiingia chuoni kadi ya CCM ni moja ya vitu vilivyokua vinatakiwa kama kiambatanisho.

Hata jeshi ni 1993 ndio waliondoa makamisaa wa dawati la siasa, tukija katika katiba ndio maana tunataka iwe mpya maana katika hii ni mbovu kwa sababu kimuundo ni katiba ya chama kimoja na iliandikwa na makada 12 wa CCM kwa kutumia utashi wao vyote hivi unavyoona vimeongezeka kuhusu upinzani vilikuja baaade kama marekebisho tu ndio vile wanaita "viraka"


Picha ya kwanza ni aliyewahi kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar [ZEC] ambaye alifuta uchaguzi wa Zanzibar kwa ngazi ya urais 2015 baada ya Maalim Seif kushinda, huyu alienda kuomba ridhaa kugombea urais kupitia CCM 2020

Picha ya pili ni jaji mkuu mstaafu kuanzia 2007 -2010 , Agustino Ramadhani akiomba ridhaa kugombea urais kupitia CCM 2015

Sasa nakuuliza swali kwa majaji ambao 90% kiumri walikua wamezaliwa na kujitambua hadi 1991 wangapi walirudisha kadi za CCM baada ya 1991?

Maana hawa wakina Jecha hawakuwahi kurudisha na walijificha katika kivuli cha kutokua na chama ila baadae wakaibuka je wako akina Jecha wangapi ambao tutawaona baade


 
Wewe ni mgeni Jerusalem.
 
Punguzeni Ushamba

Kuwa Jaji
Sio mwisho wa ndoto zako ktk kujitafutia

Nimewapa mfano wa Kenya lkn

Lkn mlivo Mayumbu bado Mnajionesha vichwani weupe au
Mnafanya Propaganda za kitoto

HOJA yangu ‼️

Mbona Kenya aliekuwa Jaji mkuu
DAVID MARAGA
kwasasa yupo Upinzani
Tena kawai kutengua Matokeo ya Urais wa Uhuru Kenyata

Kwanini Tanzania ndio iwe dhambi Majaji kuamua kugombea chama Tawala 🫎🫎🫎🫎 nasasa nawapa na Picha πŸ‘‡
 

Attachments

  • CJ_Maraga_(cropped).jpg
    19.4 KB · Views: 7
  • CJ_Maraga.jpg
    76 KB · Views: 8
  • IMG-20260330-WA0000-1774867123.jpg
    71.7 KB · Views: 6
  • images-19.jpeg
    10.7 KB · Views: 4
  • images-20.jpeg
    36 KB · Views: 8
Waliowaita Nyumbu 🫎🫎🫎🫎🫎🫎🫎🫎🫎 yumkin wakaenda peponi
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…