Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Ni kweli tuwasaidie wazazi wetu....lakini wanaomba kwa kutumia nguvu kama vile kuna kitu alikuwekesha....
Mzazi hatakiwi kuomba, yani inatakiwa aweze kumlea mtoto wake vizuri kiasi huyo mtoto aweze kumsaidia mzazi kabla mzazi hajaomba.

Ukishaona mzazi anaomba ujue kakosea sehemu fulani kubwa mbili.

1. Kwanza kakosea hajajipanga kujitosheleza yeye mwenyewe.
2. Pili kakosea hajajipanga kuwa karibu na mtoto na kumuwezesha mtoto kusaidia kabla hajaombwa.
 
Unaiandika kama mtu ambaye hajasoma au ambaye hujapata exposure yoyote kuna umri unafika pesa c chochote zaidi ya watu nyumbani tulikuwa 17 kipindi nakuwa, nyumba ilikuwa na vyumba 9 Leo hii kabaki Bibi na dada yake na mfanyakazi na mtoto WA mjomba ana kila kitu pesa gari mashamba analimisha na anapata mazao kibao Tu Ila kila siku anataka wajukuu wake akakkae nawo Ila ndyo ivyoo ata ujipange VIP kuna umri utafika utaitaji watu wa Kula nawo meza, kucheka nawo, na kujifariji hasa pale unapoumwa ndyo maana wahindi au waarabu wengi wanakaa kama familia wengi tunaona kama ushamba Ila lile ni Jambo jema sana kwenye kutunza wazee wenu
 
Nimeandika mengi, zaidi ya pesa.

Kuwa tegemezi ni tatizo pia, hata ukiwa na pesa.

Mtu kuwa needy, yani huwezi kuwa peke yako ukafanya mambo yako, kuhitaji hitaji watu kila saa, ni tatizo la kisaikolojia pia.

Na tatizo hili ni zaidi ya pesa, ni mindset problem.

Yani mtu kukaa nyumbani peke yake, au na mkewe tu, anaona tatizo tayari.

Maana yake mtu huyu hana uwezo wa kuwa self contented, hawezi kusoma kitabu, hawezi kuanzisha urafiki mpya na watu wapya.

Watu wako tegemezi sana, na hili ni tatizo lililozidi pesa.

Tatizo la self confidence, tatizo la kushindwa kuwa na utashi, tatizo la kushindwa kuwa na hobby, ni tatizo la watu wenye akili ndogo.

Sasa kati ya mimi mtu anayejua kwamba unaweza kuondoa upweke kwa kusoma na wewe unayekubali mtu kuingia upweke kwa kuwa peke yake, unaniambia mimi sijasoma, kati yetu nani hajasoma?
 
Uzuri wa JF hata Baba yako aliekuzaa,akakulea,akakusomesha unaweza kumwambia hajasoma na hana exposure.
 
Tamaduni za wahindi hizo.
 
Kila Kona shimo kuu wewe😳 huko uani si ulozi wake ndo unampeleka.Na hatosameheka na Mwenyez Mungu 😏
Haaaya, nilitaka kujua tu unaongelea nyoka au nyoka?

Sasa nishakufahamu. Sasa unataka nyoka kila kona na watoto kibao nyumbani uzeeni itakuwaje hapo?

Huoni hatari?
 
Huu uzi umekaa kibaguzi sana
 
Wewe hujamuelewa mtoa mada upweke na huduma ni vitu viwili tofauti mtoa mada kaelezea upweke hajaelezea kukosa huduma unaweza kuwa na kilakitu ndani lakini upweke ukakusesha faraja, na unaweze kua na upungufu wa huduma lakini maliwazo yakakupa faraja
 
Haaaya, nilitaka kujua tu unaongelea nyoka au nyoka?

Sasa nishakufahamu. Sasa unataka nyoka kila kona na watoto kibao nyumbani uzeeni itakuwaje hapo?

Huoni hatari?
Hata Ivo nimeghairi...uzee nitapanga then nyumba yangunitapangisha😔
 
Wewe hujamuelewa mtoa mada upweke na huduma ni vitu viwili tofauti mtoa mada kaelezea upweke hajaelezea kukosa huduma unaweza kuwa na kilakitu ndani lakini upweke ukakusesha faraja, na unaweze kua na upungufu wa huduma lakini maliwazo yakakupa faraja
Upweke kuupata uzeeni wakati maisha yote ulijua upweke wa uzeeni unakuja ni ujinga fulani hivi.

Maana yake mtu kashindwa kujiandaa vizuri na maisha ya uzeeni.

Yani kashindwa hata kununua vitabu ambavyo hakuwa na muda wa kusoma ujanani akavisoma uzeeni?

Upweke mwingine ni dalili ya mtu kukosa hobby na kutokuwa mtashi/ interesting.Mtu mwenye hobby na aliye mtashi/ interesting hawezi kuwa mpweke.
 
Mimi sitojutia na nimejiandaa kwa hilo,kwani mtaani hakuna vijiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…