Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Inafikia kipindi hela haifanyi kazi katika kukuondolea upweke; bali unakuwa unataka uwe karibu na uzao wako, ila inashindikana kutokana na uzao wako kuwa mbali kwenye maisha mengine
 
Umeona mbali mkuu; nilikuwa najiuliza kwa nini wahindi huwa wanakaa kwenye boma moja? mwisho wa siku nikagundua, ni kuweka mazingira ya kutokuwa wapweke huko mbeleni
 
Ukiwa na miaka 70+ ni mtihani mkuu
Ukiwa na maiak 70+ unatakiwa uwe unafurahia pensheni na wenzako walio 70+.

Sio unalazimisha watu wakutoe upweke. Hii ni tabia ya ubinafsi sana.

Wewe unaweza kujiona unapenda watu, kumbe ni mbinafsi unataka attention yote iwe kwako.
 
Wazo lako linaweza kuwa suluhisho kwenye hili tatizo; na ndivyo wenzetu wa Asia wanafanya.
 
Mwanaume atawaacha wazazi wake naye ataambana na mkewe...

Hapa neno la Biblia linaonyesha kuwa kuna wakati wazazi watabaki peke yao maana watoto wataenda kuanzisha familia zao...
Inaumiza sana, ulishazoea kelele za vijana wako, hatimaye wanakuja kukutenga
 
Ni kweli tupu mimi nilifikiri hali ya upweke kwa wazazi ni tatizo la Ulaya na lingechukua muda mrefu sana kufika Africa lakini tayari lipo sana tena linakuwa hatari kuliko hata Ulaya kwani umaskini hulifanya tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.
Tena nyinyi wazazi wa kizazi hiki ambao watoto wenu mnawapeleka wakakulie kwenye vituo vya Day Care kisa nyie mpo busy kutafuta pesa ndio mjipange kisawasawa. Msipojipanga vizuri na wao lazima wawapeleke kwenye elderly centers.
 
Mi napenda nikizeeka tujenge nyumba eneo kubwa Ili tufuge mifugo yote mpaka nyoka ... nikiwa Mimi na mume wangu🤸🤸🤸🤸😘
Kwa mazingira hayo; mkiwa na miaka 70+ upweke hautawatatiza?
 
Wazo lako linaweza kuwa suluhisho kwenye hili tatizo; na ndivyo wenzetu wa Asia wanafanya.
Mzee Mengi alifanikiwa kwenye hili pia, hadi anafariki vijana wake walikuwa ni Watumishi kwenye biashara zake pale IPP.

Muda wa kuweza kujiandaa na kufika huko upo, muhimu kujipanga na kuomba uhai tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…