Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Uko sahihi
 
Hii ni akili ya kitoto sana.upendo unazidi kushuka siku zinavyozidi.ilawewe ukiugua na kuwa kilema kabisa ukafilisika unataka mzazi aendelee kukulea mpaka kifo chako?
 
Ukiwa na familia na ukawaza kwa mapana hayo mambo lazima uyaone.mfano mm nimeshajua chanzo Cha kwa nn watoto wa kiume huwatelekeza wazazi wao wa kiume na kumjali mama yao.wakipiga cm inaanzia kwa mama kwanza .nikajiuliza kama mm nafanya hv Ina maana na mm nitafanyiwa na watoto wangu.hvyo nilibadilisha mfumo wa maisha kuwa rafiki wa watoto wangu na kuwatekelezea mahitaji Yao kalibu 80% nawapatia mm mwenyewe Moja kwa Moja sio kumpatia mama Yao.
 
Solution ni kuchelewa kuzaa mtoto wa mwisho ,au kuchukua wajukuu kuishi nao au watoto wa ndugu ,pia watoto hata kama wameshakua na familia zao wajitahidi kua karibu na wazazi wao ikiwemo kwenda kuwatembelea mara kwa mara hata kuwajulia hali pia inasaidia kuwaondolea upweke.

Ni kweli upweke upo kukaa bila uzao wako karibu,ndio mana ndoa inayokosa mtoto lazima iwe na migogoro sababu ya upweke ,watoto wanasaidia kuchangamsha nyumba.
 
Somesha ila zaa katika interval fulani itakayokufanya muishi na katoto kenu ka mwisho muda mrefu mpaka kufikia kaoe mnakuwa mmeshafariki
[emoji23][emoji23] mawazo hayo mda huo yanatoka wapi, ? Mnakua mnawaza kuzaa tu
 
Tena nyinyi wazazi wa kizazi hiki ambao watoto wenu mnawapeleka wakakulie kwenye vituo vya Day Care kisa nyie mpo busy kutafuta pesa ndio mjipange kisawasawa. Msipojipanga vizuri na wao lazima wawapeleke kwenye elderly centers.
Ndio janga lijalo!
 
Hii ni akili ya kitoto sana.upendo unazidi kushuka siku zinavyozidi.ilawewe ukiugua na kuwa kilema kabisa ukafilisika unataka mzazi aendelee kukulea mpaka kifo chako?
Kwanza kabisa, umewanyanyapaa watoto kwa kauli yako "hii ni akili ya kitoto sana".

Watoto mara nyingine wana mawazo mazuri sana, mpaka hapo umejionesha unaishi kwa kukariri.

Upendo ni pamoja na kujua kwamba watoto nao wana maisha yao na hawakuzaliwa ili kutumikia wazazi wao.

Kila mtu anatakiwa ajiandae kujitosheleza kwa maisha ya uzeeni, familia iwe na option ya kumsaidia au kutomsaidia.

Hizi habari za kuzaa kama investment ili watoto wakusaidie baadaye, kwa hali ama mali, ni mfumo wa ujima.

Kwa sababu, inawezekana kabisa mtoto wako akatangulia kufa kabla yako.

Sasa mtoto akifa kabla yako atakuhudumiaje uzeeni?

Watu wa familia waachiane uhuru, bila kunyanyapaa mtu.

Mtu akitaka kusaidia wazazi, sawa. Mtu asipokuwa na uwezo wa kusaidia wazazi, sawa. Mtu akiwa na uwezo wa kusaidia wazazi halafu asisaidie, sawa.

Watu wasaidiane kwa sababu wanataka kusaidiana, si kwa sababu kuna wajibu, au kwa sababu wanalipa fadhila za kulelewa na wazazi, au wanaweka kitegauchumi kwa watoto ili waje wawasaidie baadaye.

Hiyo ni biashara, hiyo si familia.
 
Watoto ni faraja pia furaha ya wazazi, mimi binafisi mama yangu alikuwa anahuzunika likizo yangu ikiisha

Sembuse uzeeni ..upweke kweli unatafuna
 
Yasije yakatokea kama yale ya Arusha......mzee kafungiwa ndani, hapewi chakula siku nyingi, mpaka kaanza kula haja yake. Yote hiyo mtoto anataka kurithi. Anyway, yote ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
 
Labda uchelewe kuzaa ndio utaishi na watoto mpk uzeeni wako karibu
 
Yasije yakatokea kama yale ya Arusha......mzee kafungiwa ndani, hapewi chakula siku nyingi, mpaka kaanza kula haja yake. Yote hiyo mtoto anataka kurithi. Anyway, yote ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
Kwani watoto si ni baraka?🤣au imekuaje tena?
 
Mbona hujamuelewa Kiranga? Yeye kaongelea upweke na faraja, hayo mambo yakunipanga sijui nini....
umeleta wewe na hii inapaswa kuwa maada nyingine. Ukiweza anzisha.
 
Mbona hujamuelewa Kiranga? Yeye kaongelea upweke na faraja, hayo mambo yakunipanga sijui nini....
umeleta wewe na hii inapaswa kuwa maada nyingine. Ukiweza anzisha.
Hata hayo ya upweke na faraja mbona nimeyaandika, hujasoma?

Na upweke ni matokeo ya kushindwa kuwa na hobby, mwenza, marafiki.
Ni tatizo unalolisababisha wewe mwenyewe unayejisikia upweke.

Sasa utasemaje upweke utenganishwe na kushindwa kujipangia maisha vizuri?

Mtu aliyejipangia maisha yake vizuri atakuwa na tatizo la kuwa na marafiki wengi, kuwa anatafutwa na watu wengi, kuwa ana hobby nyingi, kuwa ana mambo mengi ya kufanya,.

Yani, mtu huyu tatizo lake litakuwa ni kuchagua afanye nini, aonane na nani, aende wapi, ili awe productive zaidi, ili apumzike zaidi.

Mtu huyu hawezi kuwa na tatizo la upweke.

Watu wengi wanapata tatizo la upweke kwa sababu hawajui kupanga maisha yao ya uzeeni yatakuwaje.

Mtu anayejua kupanga maisha yake hata akiumwa vibaya na akiwa hana uwezo, hawezi kuwa na upweke, atapambana au kukubali hali yake tu kwa kuelewa "the human condition".

Sio kusumbua watu wengine kwa upweke wake.
 
Ukimfuatilia mtoa mada, unaweza kuishi na wanao kama mifugo.

Wasisome shule, wakae nawe nyumbani mnatizamana mpaka unakuwa mzee, ili uwatumie kama vitu vya kukufariji usiwe mpweke.

Yani kama unafuga ng'ombe ili upate maziwa au nyama!

What a selfish and medieval way of thinking.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…