Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

NAJUA CCM MMEUMIZWA SANA LEO NA NDIO MAANA MNATUNGA UZUSHI. Teh Teh Teh....kura zetu ni kwa LOWASSA.
mkuu naona wewe upo kiutani zaidi. watu tuko serious tunataka kujua nini hasa wagombea wataenda kufanya ikulu. haya sio mambo ya masihara. hivi wale ndugu zako kule kijijini wanaweza kuwa na access ya internet? mbona mnaleta utani hata kwa mambo yanayohusu mustakabali wa maisha yetu?
 
Hakuna mpya aliloongea yote tunayajua!!atuambie atatusaidiaje sio blah blah za elimu bure wakati wamasai wako porini wanachunga ng'ombe!HATUDANGANYIKI
 
Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.


11951204_1068783333154019_992321555451370143_n.jpg




zuzu, mharoooooooooo
 
Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.


11951204_1068783333154019_992321555451370143_n.jpg


HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA
CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA
YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na
tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya
upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana
chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania
uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea
mmoja katika ngazi zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM
na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio
hodhi madaraka na mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko
ya kweli nchini.
a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo
wa uchumi, haki na sheria nchini.
b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama
elimu, afya, maji na makazi.
c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha
matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za
maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania
imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa
linakuwa.
5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali
kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara
bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa.
Wanataka makazi bora.
7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta
mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu
uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga
inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya
fikra, uongozi, sera na utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-
uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo
ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini.
Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko
na siyo ahadi zile zile kila mwaka.
11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya.
12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya
wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia
maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu
kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata,
Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya
maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa
wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza
umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati
sahihi na siyo nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta
bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na
utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini
utakuwa na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na
kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na
misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza
katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka
wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni
pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika
sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na
kuondoa kodi kwa wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji
na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria
chini ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa
kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu
kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu
itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka
elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi
inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko
la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa
ni pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za
wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa
ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na
zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata
AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia
bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga
kupunguza gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa
watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija
na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga
hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na
jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea
kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na
usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya
bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya
kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa
Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya
wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji
na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu,
ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima
kutoka jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na
kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda
vyanzo vya maji.
6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima
elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na
kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa
kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza
kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana
na adha ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima
na wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia
maslahi ya nchi na ya Watanzania.
10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao
asilia ya Tanzania hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama
vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara
tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa
zile za vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha
kwa misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha
misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es
salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme
vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya
Watanzania
VIWANDA
1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa
uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya
kilimo, uvuvi na ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi
zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje
ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda
UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha
kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa
soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa
serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma
za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa
kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi
cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani.
Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika
manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya
biashara na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara
kwa masharti nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka
udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa
Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta
binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na
kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa
njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila
kujali wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa
Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na
wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha
kuboresha makazi kwa mpango wa kushirikiana kujenga
nyumba bora
7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa viwanda
vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha
na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa
kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa
wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na
kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi
upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
1. Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa
nishati
2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera
yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na
ubia kati yao na wageni.
3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa
maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe
kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele
namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji
wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji
uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za
kigeni.
5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na
madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye
raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini
kama rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya
ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa
wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa
wageni wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.
8. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo
lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake
itawekeza kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za
madini.
9. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke
kutokana na adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za
Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na
kijacho
2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa
hifadhi za taifa na mazingira
3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha
mafunzo
4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo
2020.
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA
1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za
wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya
serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
2. Tutaboresha miundobinu ya sheria na kuimarisha
utendaji wa Mahakama na maslahi ya wafanyakazi
3. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria
kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar
hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
4. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa
wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa
kusimamia utoaji wa haki.
5. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo
na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze
kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika
Sekta ya Umma
3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake
na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea
mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya
Umma na binafsi
5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni
pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini
zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga
marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa
madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za
serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni
pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia
upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi
asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio
stahiki.
2. Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia
nishati ya gesi na mafuta.
3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia
vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato
yake.
4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa
kwa misingi ya faida na uadilifu.
5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na
kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa
mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa
kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa
kudhibiti makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za
kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu
kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa
Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu
na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi
na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na
kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi
zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini
ifikapo 2020.
5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu
inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi
kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na
jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na
michezo
2. Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje
zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili
kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania
inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa
ya soka na riadha
6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili
kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA
1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na
Ujirani mwema.
2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na
kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya
kimataifa.
3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika,
Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na
kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi
shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua
nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu
na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi
mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja
tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza
uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika
kuondoa umaskini.
3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya
hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni
za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi
ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na
sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha.
Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti.
Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba
hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa
kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa
tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo
yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi
nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi
kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake kujiendeleza na
siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania
watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa
ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa umaskini kama
joho la fahari.
6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na CCM.
Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi
walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi.
Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.
7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu
Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua
kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa
mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako.
Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana
 
Ilani CCM wanayo na haitusaidii Kitu
Bado na Escrow, EPa,na Twigs wanapanda ndege,ilani ni wajibu tu lakini hajasaidia kitu Watanzania
 
Kikwete kweli amewalevya watz kwa vijembe, leo Hotuba ikiwa fupi mnalalamika, Tunapenda kuishi maisha ya kisanii kwanini? Hizi ndio hotuba za watu wenye nia njema hawezi kutoa hadithi na story zilivoanza Tangu unapanda ndege kwenda kutibiwa tezi dume mpaka unapakwa dawa za upasuaji mpk unafanyiwa operetion, unatolewa thieta.

Lakini niwambia mwanzo wa Watz kubadilika umefika sasa sio zamu ya wasanii ni uchapakazi kwenda mbele kinachofata, Wengine hawapendi hadithi nyingi zinawachocha. Mabadiliko yanakuja.

well said!!
 
Lowassa ulikuwa wapi masaaa yote?

WEWE UMESHINDWA KUSIMAMA KWASABABU NI MGONJWA, HALAFU UNAKUJA KUDANGANYA WATU KWENYE TV.

MLIKUWA MNA SIKU NZIMA JANGWANI SASA MNAKUJA NA VISABABU NJAA ETI MUDA HAUTOSHI?

ULIKUWA WAPI TOKEA SAA NANE MCHANA?
Itabidi sasa Lowassa azunguke mikoani na studio ya ITV. Akimaliza kuwasalimia wapiga kura anaingia studio kusoma sera na ilani ya UKAWA. Mpaka kieleweke.
 
  • Thanks
Reactions: snn
wiki moja imepita nilisema chadema hawana ilani ya uchaguzi panya road wakatoa matusi lakini nikajua hawajui hata maana ya ilani ya uchaguzi
mkuu hiyo ilani anaandika nani wakati wamefukuza vichwa? Prof. Mkumbo ndo aliyeandika ilani yao ya uchaguzi uliopita na Zitto ndo alikuwa mtu wa kwanza kutoa mrejesho wa hiyo ilani. leo hii wote wamefukuzwa. akina Prof. Lipumba na Dr. Slaa wamejengewa mazingira ya kufukuzwa ikabidi wajitoe wenyewe, unafikiri ataandika nani? sugu? wao wako bize kuwaondoa vichwa na kuwakaribisa akina Prof. Jay!
 
Ni jambo ambalo lipo wazi pengo la Dr. Slaa ndani ya CDM bado lipo wazi hadi sasa. Huyu ni mzee aliyefanya kazi kubwa katika kusukuma gurudumu la chama hadi leo kilipofikia hapo. Sifa kuu iliyomfanya hadi aheshimike ni kusema kweli bila uoga wala kupepesa mcho au kuuma maneno.

Ni jambo lisilopingika tena, kuondoka kwa Mh. Sumaye ni kama kulipuzwa na wanaCCM wengi kuliko alivyoondoka Mh. E. Lowasa. Lakini katika sintofahamu ya hali ya juu, leo Mh. Sumaye ameushangaza ulimwengu kwa kutoa speech ambayo ni kama imevua viraka vyote vilivyoweka na serikali ya CCM na kuiacha uchi. Amegusia karibu kila kashfa angalau kwa mapana na marefu yake tena bila mbwembwe nyingi na watu wamemuelewa vya kutosha.

Katika kufanya hivyo, amejikuta akiwafuta machozi wanaCDM ambao walikuwa nafikiria kama angekuwepo Dr. W. P. Slaa basi ni wazi mambo ambayo yamepatikana leo kwa Sumaye huenda yangepatikana kwake yeye Slaa. Hili ni faraja kubwa kwa wapenda mabadiliko na kwa kiasi kikubwa na kama kifuta machozi kwa wanaCDM kwa ujumla.

Hongera sana Mh. Sumaye kwa kuiweka bayana serikali na kufanya wanaUKAWA na CDM kwa ujumla kumsahau mzee wetu ambaye bado yupo likizo.

Nategemea uwepo wako utakuwa na umsingi zaidi katika siku za usoni.

Mungu akubariki na ni wakati muafaka sasa wa Dr. Slaa kukaa na kujitathmini juu ya hatma yake kisiasa kuliko kuendelea kukaa kimya. Ni aidha aungane na kundi la wanamabadiliko kuliko au aachane na siasa maana siku zinavyozidi kwenda ndivyo nae nafasi yake itavyozidi kupotea na siku atakapokuja kutaka kuonyesha umuhimu atakuwa kama Tabwe Hiza.

Nawasilisha.
 
lowassa ni mjanja na wakubwa zako pale lumumba na kuu street kule dodoma wanalijua hilo. Kakwepa kuongeza muda iki watu watawanyike kabla ya muda. Anajua sheria za nchi hazina favor kwa opposition na wafuasi wake, hivyo saa 3 usiku huu kashusha ilani yote kupitia itv! Ilani iko bomba ile mbaya! Naamini kesho itaandikwa kwenye magazeti na au kurudiwa itv.

Lizabon alijiapiza kuwa akihutubia tukate makalio yake, yuko wapi tuyakate makalio!

acha kusema uongo wewe, mmemuachia 20 minutes, lakini katumia nane tu anatetemeka, na kurudiarudia maneno, kwanini mnashindwa kuwa wakweli tu mka-admit kuwa mbowe kawaingiza cha kike kumuacha slaa kumweka huyo fisadi
 
Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.



Kwani wewe ulivoandika huku unategemea nani aje kusoma kama siyo sisi malofa
 
Yuko ITV anataja vipa umbele vyake,vimeshiba kweli kweli na sio porojo za mapimb.i wa CCM!

Tatizo la chama ambacho ni ONE MAN SHOW, Acheni upumbavu na ulofa, mlimleta jangwani kuuza sura? mimi nimejaribu kuingia hiyo tovuti naona tu mapicha ya mtu anayetetemeka sijui kwanini mnataka kutufanya watanzania ni wageni wa tovuti. nendeni kawambie hao vibaka na madereva wa bodaboda mliowakusanya toka sehemu mbalimbali za jiji kwamba tovuti ipo tayari na sidhani kama wana muda huo, maana leo wameshinda jangwani bila kukaba wala bila kupakia abiria. watu makini nadhani kila mtu anawajua, wanatangaza sera jukwaani. huu uchafu mliotuletea leo jangwani, sijawi kuuona mahali popote duniani kwenye kampeni. marekani Obama wengi hawakumjua, walimjua through his speeches alipokua nominee kwenye chama chake, eti leo mnasema tukaangalie kwenye tovuti nenda kawambie kule kwetu ngopyolo kwmba hotuba ya mgombea wa urais ipo kwenye tovut ya chamai. shame on you Mbowe and your Colleagues,
 
Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.


11951204_1068783333154019_992321555451370143_n.jpg



Naona akili zako zimehama kuhusu Babu seya na Balali ni mabango ndio yaliyokuwa yameandikwa na Mh.Lowasa alikuwa anasoma tu
 
Kwani mengine yote hujasikia? Hukusikia elimu elimu elimu? Hujasikia kilimo? Hujasikia afya?

Hujasikia miundombinu? Reli ya kati, air tanzania? Kweli mwaka huu mmekamatika vibaya

Miundombinu ndiyo mdudud gani?

Reli ya kati? Ina maana kadandia trni kwa mbele> Tazama hiki nini?

IMG_4006.JPG


Unajuwa Kikwete alikuwa anafanya nini hapo na akina nani?

Air Tanzania ni jina tu? Ayafanya nini?

Usafiri wa anga Tanzania kipindi cha Kikwete wa ndani na wa nje umekuwa mara kadhaa kuliko wakati wowote ule.

Aliyemdanganya aseme hayo itakuwa ni mpumbavu kuliko yeye.
 
Back
Top Bottom