WanaJF,
Nipo njiani kuelekea nyumbani kwangu nikiwa natoka hapa viwanjwa vya jangwani.
Kusema ukweli, siku ya leo nilitaka kumsikiliza ndugu Lowassa kwa umakini mkubwa sana, ili kama nikishawishika nimpe kura yangu.
Lakini kwa masikitiko makubwa sana ndugu zangu wanaJF, nimeishia kuambulia website ya CHADEMA!!!
Shauku yangu kubwa ya kupata mabadiliko kupitia UKAWA imeyeyuka ghafla, kwa mantiki hiyo, sina budi kuwapa CCM kura ya urais kwa kuwa bila shaka yoyote nilitathmini yale aliyosema Magufuli na nikaona yanatekelezeka.
Kwa wale ambao hamkupata fursa ya kwenda jangwani, nawahakikishia kuwa hamjapoteza lolote. Sisi tuliokuwa hapa jangwani tumeondoka vichwa chini, Lowassa ametuangusha tena kwa mara nyingine.
Aidha, huyu Lowassa anasema Watanzania wana shida na umaskini mkubwa. Je, huo uwezo wa Watanzania kuwa na vifaa ikiwemo smartphones na Laptop, au kwa maneno mengine, huo uwe