Watu wengine sijui mnawazaga kwa kutumia nini?!!Kila mtu anayo kinga ya kisheria ya faragha zake, ikiwemo biashara zake, Afya yake, maisha yake, familia yake, shughuli zake, mshahara wake, mapato yake, account number zake, vinalindwa na sheria mbili
1. The right to privacy
2. Data protection act.
Mtu usiye husika, huruhusiwi kufuatilia mambo binafsi ya maisha ya mtu anaishije, anafanya nini, ana biashara gani, ni none of your business!.
Ila wewe kama raia mwema ukimuona mtu anaendesha maisha yake kwa namna ya kuleta mashaka kuhusu utajiri wa mtu, unayo haki ya kufanya search Brela kuhusu kampuni yoyote, imesajiliwa vipi, inamilikiwa na nani, wakurugenzi ni kina nani, haki hii pia iko kwenye ardhi, nyumba au gari lolote.
Kuna makampuni mengine wamiliki wake wanaitwa silent partners, mfano Pap ile ya Singasinga iliyoinunua IPTL inamilikiwa 50% na Singa Singa 50% na Simba, huyu Simba ni silent partner hata uki search Brela hukuti majina, majina ya wamiliki yamehifadhiwa chini ya kinga iitwayo "the corporate veil" ukitaka kuwajua kwanza lazima uwe na sababu genuine, pili lazima uombe kibali mahakamani to unveil hiyo corporate veil.
Hivyo nakushauri dogo, deal na mambo tuu yanayokuhusu, acha kufuatia maisha ya watu!, wengine ni ma mafia!, utakuja kupotezwa bure!.
P
Kwa nini mleta mada hajataka kujua chochote kukuhusu wewe Bwana Manjaa?!
Ukishakuwa mtumishi wa umma, lazima ukubali maisha yako kuwa wazi kwa Umma pia.
Kama ukiona unataka privacy sana, basi kakae nyumbani na mkeo/mmeo halafu uone kama kuna mtu atakuja kukufuatilia