Kuuliza si Ujinga; Maharage Chande anafanya biashara gani na TTCL? Kwanini Biashara hiyo inafichwa?

Nikipata mtoto wa kiume nadhani naweza kumpa jina la "MAHARAGE" nimetokea kumuelewa sana jamaa anaonekana ni mtu smart sana

Kuna Maharage mwingine aliokoka kuliwa na papa alipotupwa baharini na mabaharia wa kigiriki baada ya kuzamia meli miaka ya nyuma kidogo( Deo Maharage).

Baada ya hapo akawa anajulikana kama “Mr Survivor”.

Anyway, what’s in a name?

Huyo dogo akiwa Mr Survivor itakuwa heri pia.
 
Mkuu! Angalizo lako ni zuri na lenye wema kwenye nia. Ila sidhani kama 'silent partner' is meant not to be known.
Silent partner huwa ana majukumu fulani limited lakini si kutojulikana
 
Data za BRELA ziko wazi kwa umma?
 
Mkuu! Angalizo lako ni zuri na lenye wema kwenye nia. Ila sidhani kama 'silent partner' is meant not to be known.
Silent partner huwa ana majukumu fulani limited lakini si kutojulikana
Be it for whatever reason silent partners hapaswi kujulikana!, ila kwa viongozi wenye kada ya viapo vya maadili, lazima a declare kwenye tamko la mali.
P
 
Paschal , don't sell us fear, men. Kama Kuna mtu anaweza kufuatilia afuatiliye tu. Kupotezwa ni kawaida kwa sababu we will all die. Hata hivyo , kufia ukweli ni the highest good of individuality.

Au nasema uongo ndugu mayala?
 
Ufisadi hautaisha Tanzania. Wananchi wenyewe wanatetea mafisadi. Mtu ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Umma anateuliwa kusimamia hiyo Taasisi anavyofanya nayo biashara. Halafu Kuna Wana CCM wanatetea kisa tu kuitetea serikali. Tuna safari ndefu.
Halafu rais anajua kila kitu ndio cha kushangaza
 
Bro acha kujipendekeza na vitisho vya kishamba. Umafia autoe wapi, sema ana vijipesa vya wizi anavyoweza kuhonga ili alipe majobless wa kumdhuru.
 
Mambo mengine yote umetupasha vema. Lakini kama sheria Iko hivo, kwanini utoe angalizo la 'kupotezwa' tunapotaka kujua jambo kama hili? Yaonyesha Kuna udanganyifu mwingi katika biashara zifanyikazo ndani ya mashirika yetu ya umma kupitia watumishi wetu wa umma!
Kama hawataki kujulikana biashara zao, basi waendeshe biashara zao nje ya mashirika yetu. Hapo ndo tunakuja kuona umuhimu wa miiko ya viongozi enzi za Arusha Declaration! Nyerere alale pema peponi, maana Sasa karibu Viongozi wetu wote ni wafanya biashara, tena mirija mikubwa wameelekeza kwenye Taasisi za umma!
Ingekuwa Siri kiasi hicho nadhani Mkuu wa nchi asingeweza kusema hadharani jambo hili. Kwahiyo Mimi naunga mkono kwamba umma unayo haki ya kujua biashara za Maharage Chande ndani ya TTCL.
 
Sasa mbona huyu anajulikana? Ila mwiko uko Kwa Maharage tu?
 
Biashara yake umeshaandikiwa humu kwenye comment japo hawaja kuweka wazi Ila Kuna mdau kaizungumzia tayari ili kuijua ni ipi aidha

1.uchambue comment kwa umakini

Au
2.usubiri siku ikijulika uje urudi kwenye huu uzi
 
Ina maana mama Samia huwa anateua bila kufanya vetting? Kabla hajamteua ndugu maharage alitakiwa awe na hizi taarifa zote,sasa tengua teua hii inaonyesha wasaidizi wa Rais hawapo makini
 
Hiyo ni siri haitakiw kusemwa hadharan mkuu hivyo bas kikubwa sisi tuna utaratib wa kulindana kweny teuzi na madili pamoja na biashara zetu!! Ishi humo
Mwalimu Nyerere na Ujamaa ilikuwa mtu anaambiwa chagua kitu kimoja kama unataka biashara tuachie kazi yetu !!
Kwa sasa tunapuyanga tu hakuna miiko wala vijiko 🙏🙏 !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…