Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Sote tunajua kuwa mchakato wa kuwapata viongozi wa Serikali unaanzia huko kwenye vyama vya siasa. Chama cha siasa kikishinda uchaguzi, aghalabu, nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali hushikwa na hao viongozi wa chama kilichoshinda uchaguzi. Hii ina maana mkiwa na viongozi wa hovyo ndani ya chama, halafu chama hicho kikashinda uchaguzi, ina maana pia mtakuwa na viongozi wa hovyo ndani ya Serikali.
Leo nimesikia kauli ya viongozi wa vyama vya siasa 13 visivyo na wabunge kuhusiana na utekwaji na mauaji ya watu wanaoikosoa Serikali.
Kwa kweli kwa aina ya viongozi wa vyama hivi, unapata jibu la haraka ni kwa nini vyama hivi haviwezi kupata mbunge hata mmoja kwenye uchaguzi wa haki na huru.
Fikiria kiongozi wa chama analinganisha tukio la kukoswakoswa kwa risasi kwa Rais Trump, na tukio la utekwaji na mauaji ya Ally Kibao!! Unajiuliza, huyu kiongozi kweli ana akili?
Ni ukweli kwamba hakuna nchi yoyote Duniani ambayo ni free from criminals. Lakini umakini na utofauti wa mataifa upo katika namna criminals wanavyoshughulikiwa, na mifumo iliyopo katika kudhibiti criminality.
Angalia kule Marekani, siku Trump alivyoshambuliwa kwa risasi. Mshambuliaji aliuawa pale pale. Ile inathibitisha kuwa mshambuliaji alikuwa ni mhalifu, na vyombo vya dola, licha ya kushindwa kuzuia uhalifu, lakini angalao mhalifu alidhibitiwa na kuuawa. Ule ni ujumbe tosha kuwa kwenye shambulio lile, serikali na vyombo vyake vyote havikuwa na mkono wake kwenye shambulio lile, na ule ulikuwa ni uhalifu wa mtu, siyo uhalifu wa dola dhidi ya Trump.
Lakini linganisha tukio lile na shambulio dhidi ya Lisu na utekaji na kisha mauaji ya Ally Kibao.
Shambulio dhidi ya Lisu, mashuhuda wanasema baada ya shambulio, washambuliaji waliondoka kwa gari lao aina ya Nissan patrol, rangi nyeupe, huku polisi wakiyazuia magari na boda, kupisha gari hilo lipite. Halafu baada ya siku kadhaa, CCTV camera zilizokuwa kwenye nyumba ya Waziri Kalemani, zinazoaminika kuchukua picha za shambulio, polisi walikwenda kuziondoa.
Kwa upande wa utekwaji wa Ally Kibao, baada ya kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi, na ndani ya gari kukiwa na askari polisi, mwenye gari aliripoti tukio kituo cha polisi, familia ya Ally nayo wakaripoti kituo cha polisi na kufungua jalada. Mara baada ya mwenye gari kuripoti polisi, akieleza mazingira yote na magari yaliyotumika kuwa yalikuwa hayana namba, hakuna shuhuda hata mmoja ambaye anaeleza labda sehemu yoyote jijini Dar es Salaam, magari yasiyo na registration number au magari yote yalikuwa yakisimamishwa kwaajili ya kuchunguzwa.
Hivi kama una akili timamu, unawezaje kulinganisha tukio la Trump kushambuliwa na kisha mara moja mshambuliaji kuuawa na vyombo vya ulinzi, Vs haya matukio ya mashambulio ya hapa kwetu Tanzania, ambayo wahalifu wanapewa njia ya kupita?